Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,628
Sheria ya TISS imefanyiwa marekebisho mwaka 1995 ambapo majukumu ya kuchukua hatua 'yaliondolewa' kwao. Hivyo kisheria hawana mamlaka ya utekelezaji. Ingawa sheria hii imekosolewa sana kwa kuwaondolea utekelezaji, kimsingi iko perfect. Inawawezesha kufanya covert operations ambazo zikibuma huwezi kuwashtaki maana watakuambia sisi hatuhusiki na utekelezaji. Mfano wangekuwa hi wao wamemshughulikia Ulimboka au Roma ungewawajibisha vipi kuwa wametenda kosa ambapo kwa mujibu wa sheria zao hawawezi kutenda? Sheria yao ni nzuri sana inampa kinga Waziri au rais kama mambo mabaya yatatendeka. Hata USA, kuna mambo ya covert ops ambayo rais hapewi details ili kumkinga kisiasa.kwa uelewa wangu mdogo ni taasisi nyeti but kikatiba na mwongozo wao haina meno kufikia kusitisha program husika ilihali ime detect fraud..rejea ile act yao ya 1990's..kazi yao ni kuatafuta taarifa(kiuchumi,siasa,ulinzi/usalama,etc), kuzifanyia kazi/kuzihakiki but atlast kuwasilisha taarifa kwa chombo au department husika..either wizara flan,Rais etc wao hawachukui action labda inapolazimu lakini mpaka order itolewe...sasa hapo Raisi akipokea taarifa ni juu yake kuzifanyia kazi au kuzitia uvunguni...
Ndo kusema sheria ya sasa haiwazuii kufanya jambo lolote kwa maslahi ya nchi. Tatizo letu siasa ndo mambo yote hapa Tanzania. Mtu akichaguliwa kuwa rais anakuwa mungu kwa miaka 10, hakuna anayehoji pale rais anapokosea kibinadamu au makusudi. Hao jamaa hawawezi sababu ya siasa zetu. Tuna siasa chafu. Ukiwa upinzan ni mhaini, ukiwa chama tawala ni Malaika.