Wakati yote yanafanyika Usalama wa Taifa walikuwa wapi?

Wakati yote yanafanyika Usalama wa Taifa walikuwa wapi?

Tanzania ina kila kitu, isipokuwa watanzania.

Tofauti na Rwanda ina Wanyarwanda kasoro Rwanda (wamezagaa nchi za maziwa makuu kwa maslahi ya Rwanda..... sisi tumekalia kusema tu "tutashtakiwa") Eee mwenyezi Mungu tuondolee aliyeturoga ambaye yumkini ni UJINGA wetu tu!!!
 
hao wapo kutoa taarifa za kiintelejesia kua wapinzani wasifanye mkutano hapo kutatokea uvunjifu wa amani wengine wanakesha kutetea ccm tu wkt rasilimali zetu zinasepa tu

...wasisahau kwamba na wao ni watanzania wenzetu! Ona Marekani Comey alivyokomaa kwa maslahi ya Taifa hadi kapoteza Ukurugenzi wake?! (Kisa uswaiba wake na Urusi badala ya Marekani na Urusi)
 
tiss buana.wao walikusanya data tu.

Mbona kwa Ulimboka na Mkatoliki walienda mbali zaidi ya kukusanya data! Hata kwingine wafanye hivyo hivyo, Tanzania itabaki lakini watu wake watapita, sasa hata kama ni mtu namba moja anatuyumbisha adhibitiwe tu kwa maslahi mapana ya Taifa!
 
Siielewi Tasisi inakazi gan hasa!...

Ata hivyo baadhi ya Member wana ukwasi uliokithiri....

Naisi sheria bado haijawapa meno na na hisi pia system yao ya kazi inawalakin.... Ni muhimu JPM aifanyie mabadiliko yenye Tija kama kweli ni Mzalendo wa kweli wataifa hili

Wana meno sana ila swala kuendana na upepo ndilo linatusumbua! Hawa jamaa hakuna wasichokijua kinachoendelea na kilichotendeka! Wafanye kazi watz tuwe na imani na nchi yetu!! Mimi tu Ngumbaru huku naona aibu kusema eti tunapewa asilimia nne za mrahaba kwa ajili ya madini, ni mikataba ambayo hata kama hukwenda shule huwezi kuiingia! Je ndugu zangu TISS nyie mnajisikiaje kwamba mpo na hamkuwadhibiti watu wachache kutuletea aibu hii kama Taifa!?
 
wale jamaa walikamilisha taratibu zote za kuingia nchini Na kupakia wanyama ni hao waliopewa dhamana ya kusimamia Sheria walikosa uzalendo ikiwa ni pamoja Na ofisi kuu ambako ripoti zote huwasilishwa
Ndiyo maana nikasema kama tuna hao watu na kati yao kuna wazalendo.... hawa wazalendo kwa kutumia 'ujuzi' wao wangekuwa wanatibua michongo yote ya kuliibia taifa bila kujali ni nani anashiriki, na bila kujali kama 'imefuata taratibu zote'.
 
Kati ya Taasisi yenye weredi mkubwa na nidhamu ya hali ya juu TISS ni namba moja Tanzania.
Hawa jamaa wana mipaka yako katika kutekeleza majukumi yao na always wapo macho katika kila jambo nchini.

Mkiwalaumu mnawaonea na kuwavunja nguvu ya kulitumikia taifa hili..

Naomba kwa heshima yao Tusiwajadili Kama ilivyo kwa Jk na Ben
 
Walikua busy kupita na ma-NOAH full tinted mtaani
 
Nashindwa kabisa kupata nafasi ya kuwasamehe hawa waheshimiwa wastaafu, kwa sababu kulikuwa na kamati nyingi zilizojaribu kuzishauri serikali zao pamoja na wabunge bungeni lakini hazikuchukua hatua yoyote. Yanayosemwa ni yale yale ambayo yanatukumbusha kuwa Katiba mpya ndio mtaji pekee utakaoiwezesha nchi yetu kusonga mbele kwa mwendo unaostahili au unaotegemewa. Bila Katiba mpya na inayoendana na kupunguza ubabe wa chama tawala na madaraka limbikizi hata malipo yatakayolipwa hatutajua faida yake. Tuliambiwa za EPA zilirudishwa, nani anayeweza kutuambia zilivyotumika?
 
hahaha..sasa ndo ikerwe zaid mkuuu..na hayo mapendekezo yako subili miongo kadhaa kwa hiki chombo...na muda mwingine tunapoteza muda kujadili kitu ambacho uhalisia wake halisi ni sintofahamu...hiyo sintofahamu ya chombo hiki kwamwe si leo kuwekwa wazi bungeni...alert mara huwa nying znatolewa mapema lakin wapewa data wanakalia mafail mchagoni...Mh.raisi anapokwenda bandari na ku point vitu kadhaa haviko sawa hajaota,kusema nani alimpigiasimu nani hajaota,raisi kupita airport na kuhoji udanganyifu wa ufanyaji kazi wa machine sio umalaika..kapewa info na ni juu yake kuamua..HII NI KATI YA MADA ISIO ISHA..tuyaache haya
 
mkuuu au sijaelewa neno 'UNIVERSAL"...sheria ya JW,JKT,UHAMIAJI na TISS zinafanana? na kwa u UNIVERSAL unataka sema sheria hizo za hapa nyumbani zinafanana na MOSSAD,M16/M15, CIA, FBI?..na unapoviushisha hivi vyombo na bunge kuna kua hakuna usiri na hizo covert ops zipangwe bungeni?..samahani naomba unitoe tongotongo kwa FACTS na coppy za hizo sheria hapa JF lakin ukitaka amendment ya TISS ya mwaka 1995 imo humu JF.
 
Wao ndo wanajua majukumu yao.....wakisema sio jukumu lao utakataa ???
 
Labda nimekosea kuuliza, hivi system haihusiki kabisa na Rasilimali za nchi hii kwa namna moja au nyingine?

Kama inahusika, wakati yote hayo yanatokea wao walikuwa wapi? Walilisaidiaje Taifa?


Marais wetu wako juu yao, hivyo kuwahonga si hajabu.
 
Tiss wenyewe ni matajiri, wana majumba na maghorofa ya kifalme, wote ni wezi tu.

Huko nako Mh. Rais afanye overhauling
Wewe unadhani hao tiss hawataki maisha mazuri?magari,majumba na mapesaaa.binadamu ni binadamu tu hakuna cha tiss wala cha nani
 
Back
Top Bottom