Wakati wa mimi kusema umefika

Wakati wa mimi kusema umefika

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2011
Posts
705
Reaction score
442
Salaam!

Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.

Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.

Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.
 
Mkuu wewe ndio uliyemuua Chacha Wangwe au Mallya mwingine?
 
Salaam!
Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali. Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!. Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.

Move yako na Dialo ndio imeanza ama tusubiri ingine?

Kuna thread ulishajibu kuhusu kifo cha Kamanda Chacha Wangwe.

Ndg. Kimbuka ndugu wa Chacha ni binadamu kama unamtumia marehemu ili kujijenga ama kupata pesa inawauma sana.

Why usitafute kick zingine?

Ok weka hiyo move CHADEMA ni mpango wa Mungu.
 
Siasa ni nzuri sana hasa zikiwa upande wako...Inaonekana dogo sasa anataka kutengeneza headline kama za Mahimbo wakati ule wa uchaguzi...

Kila la heri na siasa zenu!! Tunachotaka sisi ni kuona ni kwa kiasi gani gesi na madini yetu zimeweza kuwaletea maendeleo Watanzania.., ni jinsi serikali imeweza kuwazuia wakwepa kodi na kuweza kuongeza makusanyo ya mapato...etc
 
Mkuu unaandika humu JF kututishia au? Mbona JF sio mahali pake? Usisemee humu JF. Nenda kwa DPP au kwa IGP au kwa Werema, au Jaji Mkuu. Hao ndo watakusaidia. Watayapima maneno yako, wakiona yanafaa kwa lolote watayachukulia hatua.

Kutishiwa mbona jambo la kawaida tu. Hata kuuawa, mbona jambo la kawaida tu. Hujasikia binti aliyefanyiwa unyama wa kutisha wiki ilopita halafu bado wakauchukua na uhai wake, na kumweka uchi mtaroni?

Usiogope, sema lakini semea mahali stahiki, na ni kwa hao nlokuambia. Kama ulifungwa kwa kuonewa, nenda kwa walio tofauti na serekali. Tafuta msaada, Haki za Binadamu. Usitishie watu na weye kuwa unajua kuchonga. Amka asubuhi, chonga sana ila chongea penyewe wala usipotee njia mchongo wako ukapotea tena.
 
Siasa ni nzuri sana hasa zikiwa upande wako...Inaonekana dogo sasa anataku kutengeneza headline kama za Mahimbo wakati ule wa uchaguzi...

Kila la heri na siasa zenu!! Tunachotaka sisi ni kuona ni kwa kiasi gani gesi na madini zimeweza kuwaletea maendeleo Watanzania.., ni jinsi serikali imeweza kuwazuia wakwepa kodi na kuweza kuongeza makusanyo ya mapato...etc

Mkuu ndenga;
Nimelitafuta lile lidude la like nikalikosa. Nakupa like langu kabisa. Siasa za maji taka hazitufai tena. Hebu tufike mahali tukue, tukomae, tuseme sasa taka taka baasi tunataka "Utaleta maendeleo gani Tz??" Full stop.
Deus Mallya is nothing today. Kama walikunyang'anya leseni yako ya udereva waombe wao si huruma zetu.
 
Ulikuwa na nafasi ya kueleza kila kitu mbele ya mahakamani iweje hakufanya hivyo??

Nani ataamini utakachokisema sasa?

Wenye kuamini ukweli wataamini ndio maana bado wanasubiri
 
kULIKUA NA HAJA GANI YA KUSEMA UNATAKA KUSEMA HILI HALAFU HUSEMI?

Huna tofauti na mtusa anaetaka kujiua halafu eti anaaga, aaagh wapi!! anayejiua mnakuta tu keshajitundika na wala hua haagi mtu.....mimi nilidhani nakuta bonnnngeeeeeeee la ujumbe umetiririka mbaya kumbe nii huu upuuzi. ok ok kwahio una mpango kusema lini?
 
Jaribu kwanza kupima matukio yaliyopita,kuna watu waliibuka na hoja za ugaidi,wengine walikuja na habari za wake za watu je ya kwako itakuwa kubwa zaidi ya hiyo?
 
Kama unatumika kwa vile kipindi cha uchaguzi ndani ya chama kimefika basi umepotea njia. Kumbuka humu JF watu walikutetea sana na hoja nyingi za kizushi kuwa ile haikuwa ajali bali ni mpango wa mauaji ulioandaliwa na Chadema.

Wewe binafsi ulisema mengi sana na tena hoja zako nyingi ulimshirikisha MUNGU kuwa anaujua ukweli wa jambo hilo unalojitetea dhidi ya wanaCCM waliokutuhumu mengi. Hata mahakama ya sheria iliiona ile ajali kama ajali zingine tuu.
Hivi karibuni kuna vijana wanaotumika na CCM kama Mchange, Mtela na Shoza wamekuwa wakitoa taarifa za ajabu ajabu na kwa vile tuu serikali hii inaendeshwa ki mazabe mazabe basi ndio maana hao vijana hawako Segerea.

Huwezi kujitapa hadharani kuwa umeshiriki mauaji ya mtu ukapona. Wewe utakaa ndani na uliyemtaja atachunguzwa ili kupata ushahidi.

Tetesi kuwa ulikuwa na mawasiliano ya siri na Mratibu wa "CHAFUA CHADEMA" yule mzee fisadi wa Elimu na mali za umma Bw Diallo ulipaswa uzitolee ufafanuzi na kujisafisha. Kama ni kweli anakutumia nakuhakikisha utajijutia siku moja na hao wanaokutumia (CCM) watakutosa.

Nakushauri kama kuna njama zilifanyika kati yako na baadhi ya watu ili ile ionekane ajali wakati sio ajali bali ni njama mbaya basi funga safari na hilo tamko lako kalitolee kule TARIME. Kisha ndio uje hapa JF kutufahamisha kilichotokea kama utakuwa hai.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Unatwambia wakati wako wakusema umefika,mbona husemii lakini naamini ipo siku utasema sababu naamini damu ya mtu ina mateso sana kama mtu amehusika kuimwaga,hata asipofungwa anaweza kuishia kuwa chizi hata kama siyo leo,kesho ama mtondogoo...!
 
Back
Top Bottom