Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Vipi mkuu ulipitia mso
wakuu mliopitia chuo na kukosa ajira nawafatilia sana....niseme tu naenda kuitimu na sina mwelekeo nikisoma hii misoto ya watu naona kabisa naingia uko uko ukizingatia nina kaboom tu na ndo nalipia ada na kula na kufanya mengineyo....kujichanga apa kwa kupitia aka kaboom inakua ngumu...inafika maaali unawaza nn kitafata baada ya apa ila mda mwingine unaamua kumwachia Mungu na kuamua kudeal kwanza na kusoma nisije kosa vyote then mengine yatafata baada ya kumaliza.....kwa jinsi nilivyopitia hii thread najiona kabisa sijapitia msoto wowote japo kidogo nimepitia....shusheni nondo tu wakuu tuendelee kujifunza kupitia kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app

to baada ya kutoka chuo.
Tujuze
 
Habari za muda huu wakuu, naimani mko poa na January inaendelea kuyoyoma. Naomba niende moja kwa moja kwenye swali langu.

Kwanza kabisa lazima tukubali kuna muda mtu unapigika na life hadi unaanza kuwaza kazi za ajabu au ambazo hukuwahi dhani utayafanya. Wengine wanafikia maamuzi na wanafanya, na wengine wanaishia kuwaza tu na kabla hawajafanya wanabadili maamuzi au wanapaka kazi nyingine ya kawaida.

Binafsi wakati nimemaliza elimu yangu ya hali ya juu Dar es salaam nilipitia wakati mgumu sana kimaisha kwani sikuwa na wakumtegemea. Nilikuwa napenda sana kuingia JF kujipotezea mawazo.

Siku moja nikakutana na uzi wa jamaa fulani akidai kuwa amepata mchongo wa kuigiza video za kikubwa huko majuu na akadai kuwa yeyote atayehitaji yupo tayari kumuunganishia.

Kiukweli nimelelewa vizuri tu lakini ilibaki kidogo tu nimtafute jamaa aniconnect nizame majuu. Lakini huwa napenda kufanya utafuti wa jambo kabla halijafanyika, hivyo nikazama Google kutafuta undani wa industry ya video za kikubwa.

Nikafahamu mengi sana, faida na hasara, gharama wanazolipa na mambo kibao, mwisho wa siku sauti ndani yangu ikawa inakataa sana hizo shughuli, basi nikaacha nikapambana kutafuta ishu nyingine.

Je wewe ni kazi gani ya ajabu kwako ulifikiria kuifanya kipindi ukiwa huna kazi na life limekunyoosha.

Karibuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuendesha IT kwa Mwaka mzima kutoka Malawi Cargo hadi Kasumulu border
 
Dah hatari Sana wakuu wiki xhache zilizopita nilitembeza bahasha kuanzia obey Hadi Salenda Ila hola kuna kampuni moja ya Ulinzi nilimkuta Mlinzi getini Naye akaniletea mapichapicha tu sa wakati natoka Salenda kuelekea coco beach nikajikuta najutia HILI life kinoma Hadi nilitaman wasiojulikana waje wanipe deal aisee.
Wasiojulikana hilo deal si liliisha?, ,Yaani ukatamani uwe unanyofoa roho za watu asee..!!
 
Nilichinja kuku na kuwanyonyoa mwenyewe na kubeba ndoo moja kichwani na nyingine mkononi. Nikakatiza Jangwani hapo(nyumba zilikuwepo kipindi hicho) kutoka Moscow kwenda Kkoo kwenye mabucha kuuza hao kuku. Sikuweza kula kuku kwa miezi kadhaa. Namshukuru Mungu niko hapa leo.
 
Nilichinja kuku na kuwanyonyoa mwenyewe na kubeba ndoo moja kichwani na nyingine mkononi. Nikakatiza Jangwani hapo(nyumba zilikuwepo kipindi hicho) kutoka Moscow kwenda Kkoo kwenye mabucha kuuza hao kuku. Sikuweza kula kuku kwa miezi kadhaa. Namshukuru Mungu niko hapa leo.
Kuku wafu?
 
Ilikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).

Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.

Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)

Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap tukawa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikutana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.,akasema sawa ila kama ni kubeba gunia ndugu yangu wewe hutaweza humo ndani ni kama jehanam,Dullah akaninong'oneza achana nae mama mwenyewe ni kiongozi na ndo kasema tutakua makarani.

Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jehanam..aisee unabeba gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelele nimemwaga korosho na kuchana kiroba(wakuu gunia kuliweka mgongoni sio kazi kazi ipo kwenye miguu namaanisha balance ndo ishu). Ikabidi nihamishiwe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka ukitaka kupumzika wahindi wanapiga kelele .

Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi mikono vidonda vitupu,nakumbuka nilimwambia Yule Jirani dah hapa si tayari tumeshamaliza akasema hapana dogo bado kabisa nikazidi kuchoka na kujuta nikamuuliza tena inamaana maisha yako jirani ndo yako hapa akasema ndio nina miaka 5 na nilianza kama wewe ila kwa sasa nishazoea na wewe utazoea,akaanza kunitajia wengine huyu ana miaka 3,7 mpaka 9 aisee nikastaajabu sana mara akaja muhindi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...

Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapana ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona umebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio(huyo dullah ni mbavu ila alichemka sasa jiulize hiyo kazi ilikua ngumu kiasi gani).

Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.

Ndefu samahani.

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuchinja nguruwe ila baadae nilikuja kupenda Kaz hyo kwani nilianzakuwa maarufu San kwa kuchinja nguruwe na maposhoposho yake nikawa napewa Kam fileti na kichwa na jinsi ya kupunguza nguruwe mwenye mafuta niliaminiwa Sana na watu na pale nikawa mm nataafutwa kwenda kuchinja na kukatata mapande Hadi yatoke kilo 5o Kaz hyo sijajifunza popote nilimuiga mzeee mmoja ahap ktk ile kijij ambae alikuwa anaringa sna wktk wa kuchinja

Nimekuja kustaafu Kaz ile mm mwenye siku moja nataka kumchinya nguruwe akakimbilia katk msikitini
 
Nimeosha sana karoti kwenye mto wa bonite pale moshi mjini.......nikikumbuka nilivyokuwa napambana kwenye yale maji meusi mpaka usiku wa saa mbili najisemea tu kimoyomoyo mimi ni mwamba wa kaskazini
hahahahaha nilikuwa na pita sana hapo miaka ya 2010-2013
 
I
Kuna kipindi nilipigika mpaka nikawa sielewi kesho yangu itakuwaje, basi asubuhi moja nikaenda zangu uwanjani kwenye mazoezi kama kawaida, nilipomaliza akanifuata mshkaji mmoja tunafanya nae mazoezi amezoea kuniita sister T, akaniambia natafuta mdad wa kazi za nyumbani! Nikamuuliza mshahara na kazi zake nikamwambia ngoja nikutafutie then ntakupa jibu...

Nikarudi home nikawaza weeee, kazi za ndani nikafanye ya kwenda na kurudi mpaka hapo nitakapopata uelekeo, basi nikamtext mshkaji kumuuliza kama wanahitaji wa kwenda na kurudi akasema hakuna shida maadam mke wake yupo home maana ndio ametoka kujifungua...

Nikamwambia basi mimi nipe hyo nafasi! Kwanza alimute alafu baadae akapiga kabisa na kuuliza, upo serious? Una tatizo gani? Kwa nini umeamua hvyo? Nikajieleza pale akasema hapana, siwezi kukuweka wewe uwe mtumishi wangu aisee! Nilisononeka pale lkn baada ya wiki akaniambia kuna mahali amenitafutia kwny duka la rafiki yake nikajishikize kwa muda mpaka mambo yangu yatakapokuw sawa!! Nikavuka
I hope Mungu kakupatia na baraka nyingi sana hadi sasa... Wanawake wachache wenye uthubutu huo... Big up
 
Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...


Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.


Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
POLE MWAMBA ALL IN ALL AMINI KWAMBA MUNGU ANASIKIA KILIO CHAKO NA MAOMBI YAKO, NI JAMBO LA MUDA TU UTASIMAMA IMARA... Au ushapata ajira za serikali tayar?
 
Back
Top Bottom