Ni miaka sasa tangu Mbunge Shujaa wa taifa Tundu Anthipas Mughwai Lissu (TAML) kupigwa risasi hadharani mchana kweupe huku dalili zikionyesha kuhusika kwa baadhi ya watu wenye mahusiano na serikali ya CCM na vyombo vya usalama.
Ushauri wangu ni kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulitangaza tukio hili la kipekee kuwa ni kitendo cha kigaidi dhidi ya taifa zima. Ugaidi ni ugaidi tu hata kama utafanyika au kuamriwa na rais wa nchi.
Hatua ya pili ni kuwaahidi wananchi na wanachama kuwa endapo CHADEMA watapewa ridhaa ya kuongoza dola basi watawasaka wahusika wote na kuwashtaki kwa kutumia sheria za ugaidi.
Chama pia minashauriwa kiombe rasmi msaada wa kimataifa wa ulinzi dhidi ya ugaidi unaoweza kutendwa au kuamriwa na magaidi hasa wale wenye nyadhifa za kimamlaka au hata wanaoongoza vyombo vya usalama.
Nawasilisha