Wakati umefika kwa CHADEMA kutangaza tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu kuwa tukio la kigaidi

ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,064
2,014
Ni miaka sasa tangu Mbunge Shujaa wa taifa Tundu Anthipas Mughwai Lissu (TAML) kupigwa risasi hadharani mchana kweupe huku dalili zikionyesha kuhusika kwa baadhi ya watu wenye mahusiano na serikali ya CCM na vyombo vya usalama.

Ushauri wangu ni kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulitangaza tukio hili la kipekee kuwa ni kitendo cha kigaidi dhidi ya taifa zima. Ugaidi ni ugaidi tu hata kama utafanyika au kuamriwa na rais wa nchi.

Hatua ya pili ni kuwaahidi wananchi na wanachama kuwa endapo CHADEMA watapewa ridhaa ya kuongoza dola basi watawasaka wahusika wote na kuwashtaki kwa kutumia sheria za ugaidi.

Chama pia minashauriwa kiombe rasmi msaada wa kimataifa wa ulinzi dhidi ya ugaidi unaoweza kutendwa au kuamriwa na magaidi hasa wale wenye nyadhifa za kimamlaka au hata wanaoongoza vyombo vya usalama.

Nawasilisha
 
Wewe unaunga mkono magaidi? Siku boko haram wakivamia na kuanza kushambulia watu mitaani kwa risasi utaona ni sawa?
Hapana siungi mkono ugaidi.... Ila hapo ni kupanda pandikizi la chuki baina ya raia na serikali kwa manufaa yenu wenyewe... Bila kujali athari zitakazotokea baadaye...
 
Hapana siungi mkono ugaidi.... Ila hapo ni kupanda pandikizi la chuki baina ya raia na serikali kwa manufaa yenu wenyewe... Bila kujali athari zitakazotokea baadaye...

Kupigwa risasi mchana kweupe Mh Mbunge na serikali kukaa kimya huku dalili zote zikionesha mhusika ni serikali , Je, hiyo si kupanda chuki na ghadhabu kwa WATANZANIA?
 
Lile ni tukio la tatu la ugaidi nchini baada ya lile la ubalozi wa Marekani na yale mauaji ya baada ya uchaguzi mkuu Zanzibar 2001. Marekani alishawaadhibu wale waliofanya tukio hilo kwenye ubalozi wao ila hawa waliofanya matukio mawili yaliyobaki bado wako huru wakiendelea kutunisha vifua vyao. Lazima nao washughulikiwe.
 
waweza kuwa wewe ndiye mjinga , hivi ni mwananchi gani asiyewajua waliomshambulia Lissu na aliyewatuma ?
Hemu kaa utulie ufanye mambo yako,kwa taarifa yako tu ni kwamba Le Mutuz ni rafiki na mshauri mkuu wa Bashite,halafu Bashite ni mtoto na mshauri mkuu wa baba yake Sasa angalia hiyo chain halafu uniambie sisi Kama taifa tunaelekea wapi!!!! No wonder rais anawaambia wananchi wafyatue watoto maana elimu ni bure, development partners anawaita mabeberu eti wanatuonea wivu tunanunua ndege kwa cash. Teh
 
waweza kuwa wewe ndiye mjinga , hivi ni mwananchi gani asiyewajua waliomshambulia Lissu na aliyewatuma ?
Kwamba mpewe ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano kisa tu risasi za Tundu Lissu? Mnadhani mahitaji ya wananchi na taifa kwa ujumla ni risasi za Tundu Lissu? Kama hamjui priorities kwa kiasi hiki basi ni ngumu sana mkashika dola.
 
Madaraka tutapewa na wananchi hilo halina shaka , ila nadhani uliniquote bila kuelewa nilichoandika
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom