Wakati Rais akilihutubia Bunge alisema kuwateua wanawake kwa wingi ktk teuzi zake, mbona kateua Ma-RC wanawake wachache?

Hivi punde Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa huku wanawake wakiwa wachche mno ktk uteuzi huo.

Akilihutubia Bunge kasema atawateua wanawake kwa wingi ktk teuzi zake. Mbona imekuwa kinyume?
Je hakuna wanawake wenye uwezo wa kuongoza mikoa au kashauriwa tofauti na watu wenye umfumo dume?

Ngoja tusubiri Ma DED, DC, Makatibu Tawala, Mabalozi nk. Vingnevyo wanawake wapoteze tumaini.
NIT-PICKER-wingi haumaanishi wote.
 
Wallahi kaahidi na wanawake walifurahi wakijua awamu yao hii Sasa. Kumbe!!!! Hatari hii.
Mimi nashangaa wanawake wanataka viti maalumu katika serikali kama bungeni haiwezekani hapa ni uwezo wa mtu huko bungeni tu wamepewa upendeleo maalumu na wameonesha uwezo wao, hivi unaweza kuniambia katika lile kundi lote la wabunge wakuteuliwa wamechangia nini la maana zaidi ya mipasho na kupiga meza? sisemi kama hakuna wanawake inawezekana wapo ila hatuwezi kuwa na nchi tuanze kupeana kwa gender hapana tumejaribu bungeni na tumeona michango yao. wajitathmini wao wenyewe.
 
Naunga mkono hoja. Japo nilisisitiza, kwa vile hatukumpangia JPM, tusimpangie mama, ila hakuna ubaya kumkumbusha from time to time. Mimi naamini ule uteuzi wa ma RC, ile ni lineup ya JPM with few changes from Mama. Haiwezekani kati ya ma RC 26, wanawake ni 6 tuu!. Angevuta vuta angalau 10.
P
Mimi napingana na hii hoja ya nafasi zigawanywe kwa Gender kazi zipewe kwa uwezo wa mtu bila kujali jinsia yake ingetokea leo asilimia 60 wanawake mimi nisingetia shaka uamuzi ningeamini wanaweza ila leo hii tunaongelea hata wabunge wakuteuliwa kuwa ifutwe sababu mchango wao ni mdogo sana bungeni ni mipasho tu unaweza nenda kagombanie mbona wako wanawake wameenda majimboni na wameshinda. Hakuna watu naona kama mizigo kama wabunge wa kuteuliwa wamepewa nafasi maalumu ili wapate ujuzi lakini michango yao sasa utashika kichwa.
 
Back
Top Bottom