Mkulungwa01
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 3,979
- 5,295
Mshana Jr natambua uwepo wako kaka yangu, na wote wana-JF.
Wakati nikiwa secondary nilikuwa kijana mpole na mwenye heshima sana kwa kila mtu(japokuwa mpaka sasa nina heshima), ilikuwa kama ni kula nikose mimi mwingine ale, nilikuwa jalala la kila mtu aliyejisikia kutoa matani yake(hata yale ya kumdhalilisha mtu).
Nimeishi maisha haya sana, nilikuwa muoga, na nilipenda kumfurahisha kila mtu, marafiki, jamaa na ndugu. Wanafunzi wenzangu wengi walikuwa wakinibeza na kunikejeli, hata wale ambao walikuwa wadogo kwangu walifanya hivyo.
Niliamini ndio ilikuwa njia nzuri ya kujichanganya na kuishi vema na watu, niliamini nisipokuwa hivyo basi siku nikipata shida nisingepata msaada kwa watu, niliamini siwezi kusimama peke yangu bila " 'kampani' ya watu.
Nilidhulumiwa, nilionewa na kusemwa vibaya kwa vitu ambavyo sikustahili kufanyiwa hivyo. Na sasa nipo chuo kikuu, hata sijui kwa nini nimekuwa 'mkaksi' na naogopwa kiasi hiki, baadhi ya watu wananisema pembeni kuwa sitaki kushirikiana na wenzangu, kuchangamana, sitaki utani n.k.
Sasa nimekuwa katili(kwenye vitu vya kipuuzi), sina huruma za kipuuzi, najipenda, najijali mimi kwanza, ninajiheshimu, sina utani na mazoea ya hovyo na pia ninatambua ninachokifanya. NAFURAHI KUOGOPWA NA KUWA KATILI, BORA KUWA 'MKAKSI' NA KATILI.