Wakati mwingine wanasiasa wawe wakweli, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa hakuwa na ziara rasmi Tanzania

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ana ndege yake ninafsi wala haitaji ndege za kuungaunga kama unavyodai acha kutudanganya.
Hujui unachokiongea mkuu!!Kwa hiyo hata juzi usiku alikuja na ndege yake pale walipoonana na Mahiga?
Kwa taarifa yako alikuja na Ndege ya Swiss,ambayo ni ya abiria,na si special flight,na ilikuwa Airbus 330

Usiwe unaongea vitu usivyovijua
 
Usitegemee mgeni maarufu kama huyu kuwa na ratiba ya kutembelea kwenye nchi ya kichovu kama hii yenu , sasa inapotokea golden chance kama hii ni lazima muishobokee ili angalau mpate uchochoro wa kuzungumza naye .

Si kila wakati mtaulizwa kuhusu wizi wa kura wa Zanzibar .
 
image.jpeg
image.jpeg
Umedanganya,Swiss air huwa inashusha abiria wa Kenya na kupeleka abiria wa Tanzania tu mpaka dar, hupakia abiria wapya dar na Kurdi tena na kupakia abiria tena Nairobi,na pia piloti na wahudumu wa ndege huwa wanashuka na kuingia wengine Ikiwa Nairobi,so katibu Mkuu alipandia wapi ndege
Mkuu hii nayokupa mimi ndio schedule ya uhakika,ni current schedule ya Swiss...Kwanini ubishe wakati unaweza kuangalia "Online" ratiba ya Swiss LX294 hii hapa...,Msiwe wabishi kama vitu hamna uhakika navyo
 
View attachment 479741 View attachment 479742
Mkuu hii nayokupa mimi ndio schedule ya uhakika,ni current schedule ya Swiss...Kwanini ubishe wakati unaweza kuangalia "Online" ratiba ya Swiss LX294 hii hapa...,Msiwe wabishi kama vitu hamna uhakika navyo

Wewe unaangalia online, Mimi nimesafiri na Swiss toka dar back to dar recently, Kumbe unaandika Mada kwa kugoogle information Halafu bado unabisha tu,Halafu nikusaidie kitu, abiria wengi wa Swiss flight wanashuka na kupanda Nairobi na nikuulize, ndege huwa inafanyiwa usafi Ikiwa dar au Nairobi?
 
View attachment 479510


Naona watu wameibeba hii ya Katibu Mkuu wa UN kama "ajenda" tena,huku namuona Mtatiro akirusha makombora,na huku Mbunge Msigwa akirusha kwa upande wa pili.Vijana nao wamebeba mitandaoni kama ajenda ya kumalizia week kimjadala.

Watu wanatakiwa kuelewa tu,mambo mengine sio lazima tuingize siasa saaaanaa.António Guterres hakuwa na ratiba ya ziara ya Tanzania.Ziara yake ilipangwa kufanyika Somalia ili kuonana na Rais mpya kuhusu baa la njaa na ukame unaolikumba eneo hilo.

Sehemu ya pili ikawa Kenya kukutana na Kenyatta,na hii ni kwa sababu,nchini Kenya kuna kambi kubwa sana ya wakimbizi ya Dadaab, inayokaliwa na Wasomali,ambao sera ya Trump ya katazo la Wasomali kuingia US imewaathiri...Umoja wa Mataifa lazima iwahikikishie Kenya ushirikiano ktk kipindi hiki cha mabadiliko ya sera za uhamiaji nchini Marekani.

Maana hivi karibuni,wakimbizi wengi wenye asili ya Somalia ambao walikuwa wafanyiwe "resettlement" na Shirika la Wahamiaji la Kimataifa (IMO),kutoka kambi ya Dadaab kwenda Marekani wamezuiliwa kutokana na sera mpya ya Marekani,hivyo kuwafanya waendelee kusalia Kenya.

Hapa Tanzania alikuwa tu "On Transit",sababu ndege aliyotumia kusafiri ni SwissAir.Schedule ya SwissAir ni Zurich-Nairobi-Dar-Zurich.Na inapotoka Nairobi kuja Dsm kabla ya kwenda Zurich,ndege huwa inakaa Dsm zaidi ya saa moja na nusu.Sasa mtu mkubwa kama Antonio hawezi kukaa muda wote huo ktk ndege wakati anaweza kushuka na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi wa Tz kama wadau wa Umoja wa Mataifa.

Aina hii ya ugeni ni ya kawaida sana katika viwanja vya ndege ambayo hutumika kama "connection centre".Ukienda Jomo Kenyata International Airport VIP Lounge utakutana na Marais wengi na viongozi wengi maarufu wakipiga soga na Mawaziri wa Mashauriano ya Kigeni wakati wakiwa "on transit".Bole International Airport pale Addis Ababa VIP-Lounge humkuti Waziri Mkuu wa Ethiopia,lakini toka mawio mpaka machweo ya jua,viongozi wa kimataifa huwa "On Transit" kuelekea katika safari zao tarajiwa.

Hata kwa kumtazama tu,wale waliowahi kupanda SwissAir First Class,watakubaliana kuwa alichokuwa amekivaa Guterres ni zile pyjamas (pajama) za abiria wa daraja la kwanza ambao hupatiwa ndani ya ndege kwa ajili ya kupumzikia kwa safari ndefu.Dressing code tu ya pyjamas za SwissAir zinaashiria Katibu Mkuu alikuwa "On Transit".Ratiba na Tanzania haikuwepo.

Sio wa kwanza Guterres kupita tu bila kuonana na Rais,wapo viongozi wengi hupita kama "On transit" hapa Dsm,na husalimiana na viongozi wa chini wa serikali.Mfano King Mswati,yeye "refueling point" yake huwa ni Dsm,katika safari zake za kutoka Mbabane kwenda ama Abu Dhabi shopping au sehemu nyingine,kituo chake cha Cattering na refueling ni Dsm.Toka enzi za JK mpaka sasa,huwezi kumkuta JK anakimbizana kumpokea Mswati,bali utamkuta Membe kwa minajili ya kidiplomasia akimsubiri King Mswati.

Uwanja wetu wa Dsm hutumika kwa ajili ya "On Transit Passengers" na "On Transfer Passengers"."On Transit Passengers" ni wale abiria ambao hupita uwanjani wakiwa ndani ya ndege bila kushuka na kuchukua abiria wengine au kushusha na kuunganisha na ndege hiyohiyo kuelekea "destination" iliyokusudiwa.Mfano wa ndege zenye safari ya aina hii Julius Nyerere Int'nal Airport ni SwissAir (Zurich-Nairobi-Dsm-Zurich),Ethiopia Airways (Addis Ababa-Dsm-Znz au Addis-Dsm-Hahaya Comoro),Oman Air (Muscat-Znz-Dsm-Muscat),Mauritius Air nk.

Siku kadhaa kiongozi wa Mauritius alipita Dsm na Mauritius Air na kuunganisha kuelekea Addis Ababa kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika.Toka Sir Seewoosagur Ramgoolam Port Louis kupitia Julius Nyerere International Airport mpaka Addis Ababa.

Walikutana tu na Rais wetu ndani ya ndege,wakapeana mkono na kila mtu akarudi kwenye presidential Suit room yake ya "First class".

Hii ni dalili ya uwanja wetu kukua na kuanza kuwa moja ya "Connection" kubwa ya sehemu mbalimbali za Afrika na dunia.Sasa tunapokea abiria wote wa kutoka Msumbiji kwenda Dubai kupitia Dsm,abiria wa Mayote na Comoro kwenda Dubai.Abiria wa kutoka Mauritius kuja Afrika ya Mashariki na Mashariki ya kati ya Asia.

Tuanze kuzoea,kuwa sio kila abiria ni "mgeni rasmi" wa nchi,wengine wanakuwa wapita njia.Waziri Mkuu wa Ethiopia angekuwa anashinda Airport kama kila kiongozi anayepita Bole Int'nal Airport atamsubiri kumpokea.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm angekuwa anajipanga kila siku kupokea viongozi na mawaziri mkoani kwake,maana ofisi zote kubwa zipo kwake.Waziri wa Mambo ya ndani akiwa Simiyu ni "mgeni",ila kwenye viunga vya Dsm ni mpita njia tu.

Hence;haikuwa sehemu ya ratiba,ndio maana ni Balozi Mahiga badala ya Rais JPM
Kwa hiyo kapita Bahati MBAYA?,,,,GHAFLA?,nilikuwa na janga gani mpaka aje ghafla?.
 
Wewe unaangalia online, Mimi nimesafiri na Swiss toka dar back to dar recently, Kumbe unaandika Mada kwa kugoogle information Halafu bado unabisha tu,Halafu nikusaidie kitu, abiria wengi wa Swiss flight wanashuka na kupanda Nairobi na nikuulize, ndege huwa inafanyiwa usafi Ikiwa dar au Nairobi?
Kaka wewe unataka kubishana...Hiyo screen shot nimekuletea ili uone status ya movement ya Swiss ya leo,na kipindi chote cha Low Season.

Kwa kipindi hiki hiyo ndio schedule yake,inatoka Zurich inapita Nairob wanakuja Dsm wanabadili Crew then wanaelekea Zurich.Crew na usafi unafanyiwa Dsm...Chakula kinachukuliwa Nairobi kwa ajili ya ku-accomodate wale waliopanda Nairobi kupitia Dsm kwenda Zurich.

Wakati wa high season,ndege hutoka Zurich,Nairobi then Dsm na baadae Nairobi na kuelekea Zurich.Suala la kusema kupanda ndege,hapa sio mahali pake,wengine hata kuhesabia tumepanda mara ngapi hatukumbuki!!Usiwe mbishi wakati unaweza kuangalia LX294 ratiba yake ikoje.

Sasa unabisha wakati nimekuonesha movement ya tarehe 12/03/2017 na inakuonyesha Zurich-Nairobi-Dsm-Zurich then bado unabisha??I sign off to argue with u
 
USAHIHI.
1/Katibu mkuu wa UN alikutana na waziri wa mambo ya nchi za nje katika mazungumzo ya kidiplomasia. Halikuwa tukio la kushtukiza au kubahatisha. Tanzania ilijua ujio wake na Katibu mkuu wa UN alijua. (Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka UN zinazoizungumzia ziara hiyo).

2/Tanzania ilishindwa kuzingatia matakwa ya itifaki kuu za Kidiplomasia. Itifaki ilimtaka mkuu wa nchi ya Tanzania awe ndio mwenyewe wake. Hili kwa sasa ni tatizo katika serikali ya Awamu ya Tano, itifaki kuu za kidiplomasia kwao sio issue kabisa.

3/Katibu mkuu wa UN hawezi kufanya mkutano au mazungumzo yoyote ya kiofisi na mtu yoyote yule kama hayajapangwa na ofisi yake. Hilo jambo haliwezekani kamwe kwa sababu ni hatari katika itifaki kuu zinazoongoza UN. Uwepo wa Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania katika mazungumzo yake na katibu wa UN ulikuwa kwa niaba ya mkuu wa nchi ya Tanzania.

4/Lawama zote katika suala hili zinapaswa zielekezwe kwa Ikulu na wala sio kwa mheshimwa rais, maana Ikulu ndio inayopaswa kupanga na kuratibu kazi za mheshimiwa rais za kila siku. Ni ajabu kama Ikulu haikulijua hili mapema au ililijua na ikaamua kulipuuzia kwa makusudi.
 
Wewe umewahi panda Swiss flight au umewahi Fanya stop over yeyote, ningependa hili kukaa Liwe na Watu Wenye uelewa wa mambo, Swiss flight from Nairobi to dar inachukua masaa mangapi, ukijibu hilo ntakuelimisha
 
Mkuu wa Mkoa wa Dsm angekuwa anajipanga kila siku kupokea viongozi na mawaziri mkoani kwake,maana ofisi zote kubwa zipo kwake.Waziri wa Mambo ya ndani akiwa Simiyu ni "mgeni",ila kwenye viunga vya Dsm ni mpita njia tu.

Hence;haikuwa sehemu ya ratiba,ndio maana ni Balozi Mahiga badala ya Rais JPM
Ahsante brother nazani... Watakua wamejifunza jamaa
 
Msigwa akiona hii post atajiona kilaza sana
Ni uhuru wa kutoa maoni tu. Ukilaza ni kushindwa kutoa maoni kwa kufikiri kuwa yatakosolewa. Msigwa na Mtatiro wametoa maoni na hata kama walikosea ni afadhali hivyo kuliko kutokutoa maoni wanayofikiri ni sahihi hata kama yataonekana kuwa kinyume.
 
Back
Top Bottom