wakati huo ukifika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wakati huo ukifika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Apr 2, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Dokta Remmy Ongara aliwahi kuimba:

  "Mwanzo wa mapenzi ni tamu kama chungwa, katikati ni kama ndimu, mwisho wa mapenzi ni chungu kama shubiri"

  Relationships nyingi ziwe ni ndoa au uchumba/galfriend-boyfriend kweli ukizichunguza utaona zinapitia vipindi hivyo.Kuna zinazotoka from chungwa straight to shubiri na zipo zile ambazo huji transform polepole kutoka chungwa kwenda ndimu na hatimaye shubiri au kubakia hapo hapo kwenye ndimu bila kwenda kwenye shubiri.

  Je ni lazima kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingi kwa namna ya kudumu? au je inawezekana kubakia kwenye chungwa muda wote.Ofcourse kuna migongano ya hapa na pale na hiyo ni ya kawaida.
  naomba maoni yenu.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  WoS dada yangu kila kitu kikuwa thro stages na vivyo hivyo ndoa ili ikomae ni lazima ipitie stages hizo zote. Ile inayobakia katika chungwa inawezekana

  1. Upendo wa kweli upo katikati yao ukiongozwa na nguvu za Mwenyezi Mungu.
  2. Either mmoja wao ameamua kujifanya mjinga ili maisha ya amani yawepo
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mj1,
  ninakubaliana nawe kabisa.Ila huu upendo wa kweli kidogo ni kitendawili.Mmojawapo wa wenye uhusiano anaweza kuwa na huo upendo wa dhati ila mwenzie kwa vile ana yake moyoni ikawa vigumu kupokea huo upendo wa dhati na kuwa mkorofi tu.Kwa vyovyote machungu ya shubiri hayakwepeki.Ila pia kuna wale wenye ujuzi wa kuweka mambo sawa kwa maana hata kama ana yake basi anajua namna ya kuweka uwiano na kuhakikisha hakuna migongano mikubwa sana yakuleta machungu yasiyosahaulika.
  Kuna mambo ambayo kwa vyovyote kuhafanya uhusino usitengamae hata ufanyeje:
  - Ukatili hasa wa kisaikolojia
  - Uchoyo uliokithiri na hii ni kwa wote wanaume kwa wanaume
  -kuhamia nyumba ndogo
  n.k
  Migongano mingine ya kawaida huweza kusahaulika na kusamehewa a hivyo kuendelea na maisha.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Kama Remmy Ongala aliimba hivyo, DDC Sikinde ngoma ya ukae waliimba ' MV Mapenzi meli ya wapendanao!'

  Nahodha kajitosa baharini?

  Duniani kuna mengi
  sawa sawa na bahari
  kuna papa na nyangumi
  tena wale wakaali

  hawapendi kuiona
  meli yetu baharini
  watafanya kila njia
  waifupishe safari


  ...mapenzi/maisha ya ndoa yanapitia mawimbi na dhoruba, wakati mwingine shwari,...iwapo manahodha ni 'mimi na wewe', mdhaifu ni yule atayejitupa kwanza baharini :)
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lakini Mbu je hivi ndivyo ndoa zinavyotakiwa kuwa? Kuwa mawimbi na dhoruba ni lazima viwepo?
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Sisy yaani kuna wale wenye agenda ya siri na bado wakashindwa kuficha au kula na kipofu. Wengine mapenzi yanaonyeshwa pale anapojua kuwa kuna kitu unatarajia kumpa mf. Pesa. Lakini baada ya hapo awezakutenda hata asikumbuke kuwa ulishawahimtendea mazuri.

  Lakini utamtambuaje mtu kama huyu?
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mbu ndo ivo!
  hao hao DDC waliwahi kuimba:
  Mwanetu kaza roho uishi na mmeo, ni wewe mwenyewe uliyempenda... tulikufahamisha na mapema kuwa mchumba wako ni mlevi..hukutaka kuyasikiaaa..leo umeyaona mwenyewe mwanetu ehhh...U

  Ukweli ni kuwa kungekuwa na namna ya kumfahamu mtu alivyo tangu mapema, nadhani wengi wasingeoa au kuolewa na hao watu wao.Unapokuja kumjua mtu wako vema..its too late!
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie nadhani hiyo migongano wakati mwingine inadumisha/yanaboresha relationships na wakati mwingine inabomoa, inadumsha pale mnapoweza kutofautiana kwa mambo flani then mtu akalikubali kosa/kukosolewa! ( hakuna perfect) inafanya uone kama patner anajali/anakupenda na alifanya hivi na vile kwa bahati mbaya! yacwe mazito kama WOS alivyoyataja hapo juu.
   
 9. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumbuka mpenzi, mume au mchumba ni mtu mliyekutana ukubwani , mmelelewa sehemu tofauti, kimazingira tabia na hata imani kwa hiyo ni lazima kutakuwa na tofauti tu,
  Nakuhusu hizo stage nadhani kwenye mapenzi lazima ziwepo na ni challenge mkishapitia hizo zote mnarudi kwenye chugwa kinachotakiwa hapo ni uvumilivu ndo maana ukiona wazee wengi sasa hivi wanapendana mf. babu na bibi yangu wanapendana sana siku moja nikamuuliza bibi yangu hivi nyie mmewahi kubombana ? akaniambi we! wanawake wa zamani tulikuwa wavumilivu ingekuwa ni nyie wa sasa hivi mnavyopenda kuondoka msingeweza basi akaanza kunipa story we kwa kweli nisingeweza, lakini yote yalipita sasa wanaenjoy.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Joyceline,
  Alivyosema bibi ni ukweli mtu.
  Unajua ukiweza kuvumilia hadi mkafika umri fulani..inabidi yule mkorofi awe mpole tu maana kama ni uzuri wa sura hakuna tena. Kama ni kutafuta mapenzi nje, mtu anajua kabisa kuwa huko nje hatapendwa kweli bali ni kuchunwa tu.Inabidi ampende tu huyo mzee mwenzake!
   
 11. annamaria

  annamaria Senior Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamani wengine wanatoka kwenye chungwa,ndimu,shubiri halafu yanarudi tena kwenye chungwa mpaka kuzikana.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,875
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Ndoa inataka uvumilivu wa hali ya juu. Hamuwezi kuishi miaka 30, 40, 50 na zaidi bila ya kuwa na majaribu chungu nzima mpaka katika ndoa yenu. Kikubwa ili kuweza kuyashinda majaribu hayo ni uvumilivu tena wa hali ya juu. Unasikia watu walio kwenye ndoa wanagombana na ugomvi wenyewe ni wa hali ya juu. Mke kagundua kwamba mume ana mtoto wa nje au ana mwanamke wa nje ambaye anamuhudumia vizuri sana. Ukisikia ugomvi mkali kati yao na maneno yanayovurumishwa kutoka kila upande pamkoja na jitihada za kuwasuluhisha lakini hakuna mafanikio yoyote basi unajua ndoa yao imefikia tamati. Baada ya muda unakuta wenyewe wamekaa chini wakakumbuka walikotoka hadi kufikia hapo walipo. Wamekumbana na majaribu chungu nzima na kuyashinda yote hivyo wanaulizana kama wanaweza kuendelea na hatimaye wote wanasema bado wanapendana na kuamua kujaribu kuendelea tena kuona kama wataweza tena kuvuka kikwazo kingine ndani ya ndoa yao. Na mara nyingi huwa wanafanikiwa hasa wala wa zamani.

  Kwa maoni yangu ndiyo maana Watanzania wengi walio nje wanapenda kuoa/kuolewa na Watanzania wenzao pamoja na kuwa na utamaduni unaoshabihiana pia kuna hili swala la uvumilivu pindi mnapokumbwa na majaribu katika ndoa yenu. Wenzetu hasa wa nchi za magharibi wengi hawana uvumulivu huo na utamaduni unapokuwa tofauti basi hali ndiyo inakuwa ngumu sana. Inafurahisha kuona watu walioishi miaka chungu nzima na kukumbana na majaribuni mengi katika ndoa yao wakiulizwa kama wangerudi ujana wao je wangeamua kumuoa/kuolewa na yule waliyekuwa naye katika ndoa, wengi husema bila matatizo wangekubali tena kuoa/kuolewa na huyo waliye naye.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  BAK,
  Na ndiyo maana kushabikia ugomvi wa wanandoa mwishowe unabakia na aibu na kuonekana wewe ndiyo mbaya.
  Kuna wale wenye tabia ya kupenda kupeleka maneno ya uchonganishi - mara oh nimemuona mumeo na mwanamke..mara mkeo siku hizi anatembea na fulani.Jamani! Usithubutu kamwe kuwa mchonganishi au shabiki.
   
Loading...