Kwa mzungu mwanzo wa siku ni saa sita usiku hivo hadi "kunakucha" keshahesabu masaa sita. Sisi waswahili siku mpya inaanza jua linapochomoza saa kumi na mbili(mwisho wa usiku wenye jumla masaa kumi na mbili) Mchana nao masaa kumi na mbili hadi jua linatua. Kimsingi mfumo wa saa wa kiswahili una reflect hali halisi ya muda kuliko mfumo kizungu,hayo mawazo yangu tu.
Mkuu
Simplemind hilo ndilo jibu sahihi kabisa.
Unajua kiswahili kimetohoa maneno mengi ya kiarabu na baadhi ya Culture za kiarabu na za middle East kwa ujumla
utamaduni uliokuwepo middle East ni kuwa siku inaanzia asubuhi
(Mchomoko wa jua) na kuishia jioni
(Mzamo wa jua) hiyo huwa ni siku moja, na kuanzia jua kuzama mpaka kuchomoza ni siku nyingine,
kwa hiyo hesabu yao inaanzia asubuhi na kuishia jioni (refer to Sabath day), huo utaratibu ndio ulikuja Tanzania kupitia Waarabu kuwa siku inaanzia asubuhi, hivyo inakuwa saa moja asubuhi na kuishia saa kumi na mbili jioni na kisha siku nyingine inaanza na saa moja usiku na kuishia saa kumi na mbili alfajili,
Wazungu wao siku yao inaanzia saa sita usiku na kuishia saa tano na dakika 59 na sekunde kadhaa usiku,
Sasa Watanzania tukazichukua taratibu zote mbili (za kizungu na za kiarabu/Middle east), hivyo basi siku ya kizungu inapoanza na saa moja (
Saa saba ya usiku kiswahili) mpaka inapokuja kukutana na saa moja ya Kiarabu(Kiswahili) yeye atakuwa na
0700hrs na Waswahili tutakuwa na
1.00kamili Asubuhi Hapa ndipo kwenye hoja ya mtoa mada
na sababu sio saa za mishale wala Crockwise na Anticrockwise kamawachangiaji wengine walivyosema