Wakaazi wa jimbo la Alaska hulipwa USD 1500+ kutokana na mapato ya mafuta katika jimbo lao. Kwanini watu wa Kusini hawapati chochote kutokana na gesi?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Jimbo la Alaska USA lina utajiri mkubwa wa MAFUTA.

Sasa serikali ya jimbo hilo kila mwaka hutoa kiasi fulani cha mapato yanayotokana na mafuta na kuwagawia wananchi moja kwa moja.

Nimejiuliza kwanini serikali ya Tanzania haitoi sehemu ya mapato ya gesi ya kusini na kuwagawia wakaazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi?

Au kwanini serikali yetu haifanyi jambo lingine lolote lile la kijamii kwa ajili ya wananchi wa Mtwara na Lindi kutokana na mapato ya gesi yao?

NB
kigezo cha kulipwa fedha za mafuta ya Alaska ni uwe mkaazi wa jimbo hilo kwa mwaka mmoja kabla hujapatiwa fedha hizo, na uishi ktk jimbo hilo mwaka mmoja baada ya kulipwa.

cc Chige, Nguruvi3, tindo, johnthebaptist , Erythrocyte
 
Sisi tunaishi kindugu wao wanaishi kibepari.

Utaratibu mbaya wa matumizi ya rasilimali ndio husababisha kitu wazungu wanaita " resources curse. "

Kwa mfano, kwanini serikali isiwape wananchi wote wa kusini bima ya afya kutokana na mapato yanayotokana na gesi?

Na hili litokane na serikali nje ya utaratibu wa fedha za csr toka kwa wawekezaji.
 
Hata John Walker mwenyewe akiusoma huu uzi atashangaa, wala hajui kwa nini hawalipwi.

Kifupi resources hazipo kwa ajili ya wananchi zipo kwa ajili ya wenyenchi. Ndio maana decentralization ya serikali inapigwa vita. Kifufupi ukiwa na centralized pool ya resources unafanya kama mchezo wa upatu, unawaambia wa kusini leo tumezipeleka kaskazini kwa ajili ya 123, halafu ukienda kaskazini unawaambia tumezipeleka Magharibi kwa ajili ya 456
 
Kaka mkubwa Tatizo ni huu mfumo wa Jamuhuri. Ila tungefanya hivyo tungefika mbali sana

Na amini kuwa ilikuondoa vipengele vya hivyo kwenye mikataba mingi ya wawekezaji nchi hii kuna chama huwa kimejaa madalali ,trust me huko kusini ingewezekana,kanda ya ziwa kwa accacia ingewezekana,kaskazin pia,nyanda za juu kusini pia.

Katikati na Magharibi tungetafta namna ya kupambana
 
Mkuu nilisikia wana mpango wa kuanzisha sovereign wealth fund kwa ajili ya pesa ya gesi. Ambapo ikizaa itatumika kwenye miradi ya serikali so sioni kivipi hizo benefits za Alaska zinaweza kuwa replicated Kusini.
 
Huko Alaska, kwa mabeberu wanaibiana, sisi tunaishi kijamaa.
Wananchi ni wazalendo, hawahitaji kuwa na maisha mazuri. Gesi inachangia vigogo wa serikali kuendeshwa na V8, nyumba, n.k.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Camoooon!!! Sioni vizuri!!
 
Tumpe JPm miaka mingine 5 utapata jibu. Sera ya mwalimu ni "Utanzania sio Ukusini "JPM anasimamia hilo

Hata Alaska wanazingatia Umarekani zaidi.

Cha msingi ni mhusika awe mkaazi na mlipakodi wa Alaska mwaka mmoja kabla hajaanza kupokea malipo toka mfuko wa mafuta wa Alaska.

Kwa hiyo Mmarekani yeyote anaweza kutimiza kigezo hicho ikiwa ataweka makazi yake Alaska. Pia mzaliwa wa jimbo la Alaska anaweza asipate fedha hizo ikiwa ataamua kuhamia majimbo mengine kama Texas, au New York.
 
Hahaha umewahi kuishi Alaska wewe?!

Mi nimeishi Kotzebue nilifanya practical sehemu moja hospitali ya Maniiaq.

Kugumu hata hiyo $1500 haina maana.
Mtwara kama ulaya, yupo Dangote.
 
Hahaha umewahi kuishi Alaska wewe?!

Mi nimeishi Kotzebue nilifanya practical sehemu moja hospitali ya Maniiaq.

Kugumu hata hiyo $1500 haina maana.
Mtwara kama ulaya, yupo Dangote.
..but wananchi wa Mtwara na Lindi are getting usd 0.

..sasa usd 1500 kwa wananchi wa Mtwara na Lindi haiwezi kuwapa afueni ya maisha?
 
Geita imejaa Dhahabu...
Kahama inanuka Gold....
Mwadui pametapakaa Almasi...
Mererani pamejaa Tanzanite.....
Kabanga imesheheni Nickel.....

Ebu ngoja nawao waombe gawio la mwaka kwa kila mwanachi alafu tuone kitakacho fuata...
 
Geita imejaa Dhahabu...
Kahama inanuka Gold....
Mwadui pametapakaa Almasi...
Mererani pamejaa Tanzanite.....
Kabanga imesheheni Nickel.....

Ebu ngoja nawao waombe gawio la mwaka kwa kila mwanachi alafu tuone kitakacho fuata...

Wape kabla hawajaanza kuomba.

Pia kuwa mkweli na muwazi katika mapato na faida zinazotokana na rasilimali hizo.
 
Back
Top Bottom