Ndugu zangu, hakika chama chetu kikongwe kimejaa propaganda za maji taka, makada walijitokeza na propaganda kuwa Lissu hawezi kurudi Tanzania,Lissu aliwathibitishia watanzania kuwa angerudi tu, wakabadili gia kuwa akirudi atakamatwa airport, Jamaa akarudi tena kwa kishindo wakashindwa kumkamata airport.
Wakasema Chadema haiwezi kumpa nafasi ya kugombea Urais maana Mbowe na Lema hawamtaki wanamtaka Lazaro, Chadema ikampa kugombea tena kwa kura nyingi sana. Wakasema tume lazima itamwengua maana ana kesi kwahiyo hatatoboa, akateuliwa kugombea.
Wakasema hana pesa za kufanya kampeni hawezi kuzunguka nchi nzima, leo yupo anazunguka kila kona tena kwa speed ya 5GB. Wakasema hata pata watu kwenye mikutano yake, sasa ni mafuriko.
Mgombea wao akawaambia wafuasi wake kwamba picha za mikutano ya Lissu ni za ku edit, wamegundua kuwa mgombea wao hakuwa sahihi wamekuja na propaganda mpya kuwa watu wanaojaa kwenye mikutano ya Lissu siyo wapiga kura kwa kuwa hawajajiandikisha ila wanafunzi na wale wanaojaa kwenye fiesta ndio wapiga kura. Hakika wajumbe wamezidi kuyeyuka na propaganda za maji taka. Mwaka huu kazi mnayo wajumbe,a.k.a makada a.k.a uvccm walioagizwa kujibu hoja.