yohana charles
Senior Member
- Mar 21, 2013
- 134
- 10
Bunge maalum la katiba linaloanza wiki hii mjini Dodoma ni muendelezo wa harakati za kupata katiba mpya itakayokuwa msingi kwa kizazi cha leo na kijacho kwa takriban miaka 50 ijayo.. Wito wetu kwenu wajumbe wa bunge la katiba ni kwamba kumbukeni mpo Dodoma kwa ajili ya kazi mliyotumwa na watanzania...mapendekezo na matakwa ya watanzania ndio yanatakiwa yatimizwe na siyo misimamo ya vyama...tambueni siku zote mtakazokuwa Dom mnaishi kwa kodi za watanzania na siyo vyama vyenu....KUMBUKENI VYAMA VINAPITA LAKINI TANZANIA ITAKUWEPO HATA MWISHO WA DUNIA...TANZANIA KWANZA VYAMA BAADAYE.!