Wajumbe katika uchaguzi wa wabunge wa Viti Maalum kupitia kundi la vijana wa UVCCM wamewachagua wagombea sita akiwemo Jesca John Magufuli kuwa wabunge wa Viti Maalum kupitia kundi hilo kwa Tanzania bara.
Katika matokeo yaliyotangazwa alfajiri ya leo, Agosti 2, 2025, kwa upande wa Tanzania Bara zilipigwa jumla ya kura 2466 ambapo washindi ni Ng'wasi Kamani aliyeongoza kwa kura 409 akifuatiwa na Jesca Magufuli aliyepata kura 391, Halima Bulembo kura 320, Lulu Mwacha kura 316, Juliana Masaburi kura 282 na Timida Mpoki kura 280.
Uchaguzi huo umefanyika kuanzia Agosti 01, 2025 na kumalizika Agosti 02, 2025 Mtumba, Jijini Dodoma.