Wajumbe bunge la katiba: Mpokeeni Amos Wako kwa tahadhari kubwa

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
kama tulivyoelezwa hapa jamvini leo, wale nguli walioalikwa kuja kuwapiga msasa wajumbe wa wa bunge la katiba walikuwa ni pamoja na omar mapuri, msekwa na kutoka nje ya nchi ni amos wako. nimefurahishwa sana kwa jinsi sita alivyopokea mawazo ya wengi na kuwaondoa wanapropaganda akina mapuri na msekwa, ingawa ingekuwa ni uwezo wangu angalua msekwa angeruhusiwa.

hofu yangu ni huyu ngulu mwingine aitwaye amos wako, mwanasherisa mkuu wa zamani wa kenya, ambaye alifanya kazi wakati kenya ikiwa kwenye mchakacho wa katiba unaolandana na siyo kufanana na huu wa kwetu.

mtakumbuka jinsi wako alivyoharibu rasimu ya kwanza ya katiba ya kenya kwa tabia yake ya kujikomba kwa kibaki, kitu kilichoelekea waanchi kuipigia kura ya hapana rasimi hiyo. kama siyo watu mahirikama profeso patrice odhiambo lumumba wakenya leo wasingekuwa hapa walipo. nani asiyejua kuwa uhusiano wa amos wako na andrew chenge ni mkubwa sana kwa kuwa wote walikuwa wanasheria wakuu wakati huo? kwa hiyo yawezekana huu ni mwaliko wa chenge na wala siyo sita!

kwa amos wako hapa siyo kenya, ukileta ule ujinga wa ukuu wa watawala iliupotoshe mchakacho wetu utajikuta unatolewa mzobe mzobe kwa kuwa kuna wajumbe wameapa kulinda mchakacho huu.
 
Mleta mada unachokifanya ndicho unachokataa Wako asikifanye yaani una mawazo yako ambayo kama wako akiwa kinyume chako basi ni mvurugaji akiwa upande wako je? Tafadhali kumbuka wao wanatoa mawazo yao tu kwa uzoefu lakini mwisho wa yote maamuzi yanabaki kwa wananchi wa Tanzania. Ni sawa na ilichofanya tume ya Warioba na Bunge la katiba watafanya wafanyayo lakini mwisho Wenyenchi ndiyo wapiga kura kama sivyo basi alichotoa Warioba kiidhinishwe kuwa katiba kamili.

Tukumbuke demokrasia ni ghali na mara nyingi inabalance ili wengi wafaidi wachache wakose kabisa.

Tuache kupotosha wengine. Katiba siyo serikali moja mbili au kumi ni muunganiko wa mambo mengi. Hivyo tuache dharau na kejeli tutoe mawazo yetu kwa uhuru na pia tuwaache wengine nao watoe maoni yao kwa uhuru. Katiba si yako ni ya wote.
 
NDUGU Mabulangati umeielewa mada vizuri? Kinachoelezwa ni tahadhari ya kabla wayachukulie kama maoni tu
 
huyu hajui maana ya tahadhari, kwani aliyetaja serikali tatu ni nani?
 
Kwanini wasimualike Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta anayeheshimika kimataifa na kitaifa kwa weledi wake, kama kweli wanataka kujifunza juu ya katiba?
 
Kwanini wasimualike Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta anayeheshimika kimataifa na kitaifa kwa weledi wake, kama kweli wanataka kujifunza juu ya katiba?

Kumbukumbu zangu zinaonyesha Profesa Shivji ni nguri mkubwa katika katiba.
 
Kumbukumbu zangu zinaonyesha Profesa Shivji ni nguri mkubwa katika katiba.

Kwa bandiko lako kama vile unawafananisha na humjui vizuri Samatta kama unavyomjua Shivji!!! You will be well advised to find out about his credentials.
 
Kwa bandiko lako kama vile unawafananisha na humjui vizuri Samatta kama unavyomjua Shivji!!! You will be well advised to find out about his credentials.

Wajummbe wanahitaji mtu wa kuwaelimisha ni Prof Shivji tokea ujana wake mpaka anazeeka alikua akifanya kazi kama hiyo, nashangaa wanachukua watu mpaka nje ya nchi lakini yeye awala hawamtaji.
 
Hizi semina ni upuuzi tu na uthibitisho wa ubadhirifu wa fedha za umma anaopenda kufanya Sitta. Ni Sitta huyu huyu aliyetumia zaidi ya milioni 500 kujenga ofisi ya spika Urambo! Leo anatumia tena zaidi ya milioni 200 kuandaa semina zisizo na kichwa wala miguu. This guy is disgusting
 
Kuna upotoshaji mwingi kuhusu Bwana Amos Wako, anayetajwa kwamba atakuwa Kiongozi wa wanenaji kutoka Kenya, katika Semina ya Bunge Maalum la Katiba, Alhamisi, 20.3.2014. Kwa mfano, Gazeti la Mwananchi, Jumatano 19.3.2014, limeandika katika Uk3,"Semina....itatolewa kesho na magwiji wa Katiba wa nchi hiyo (ya Kenya), akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi hiyo, Amos Wako." Je, ni kweli kwamba Amos Wako alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Kenya? Na je, ni kweli kwamba Amos Wako, alikuwa mstari wa mbele katika kuisaidia na kuiwezesha Kenya, kuwa na Katiba Mpya? Tujadili.
 
Katika habari za mtandao, Mwenyekiti wa Tume ya Utekelezaji wa Katiba Mpya ya Kenya, Charles Nyachae, alimtaja Amos Wako, kama Mwanasheria Mkuu wa Kenya, aliyekuwa kikwazo katika mchakato wa Katiba Mpya ya Kenya. "The Chairman of the Commission for the Implementation of the Constitution (CIC), Charles Nyachae said, "The Attorney General, Amos Wako, is becoming an impediment, and is not helping the process."
 
Huyo alikuwa "counterpart" wa Chenge. Analetwa na Chama Cha Magamba, ili kudanganya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. UKAWA, beware!!!!!!!!!!!!!
 
Mbona huyu aliongoza tume iliyoitwa 'Tume ya Wako' kwa ajili ya kuandaa uazishaji upya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki? Tume hiyo ilikuwa inaundwa na wanasheria wakuu wa Kenya, Tanzania na Uganda, mwenyekiti akiwa Amos Wako.

Nadhani Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya Kenya alikuwa gwiji wa constitutional law, Prof. Yash Pal Ghai, ambaye ni mkenya mwenye asili ya India.
 
kwen huyo amos ndio anaandika katiba???

bado ni majanga tu mtu aliyezuiwa na marekani kuingia usa kwa sababu alikuwa kwenye orodha ya watu waliokuwa wanazuia mabadiliko siasa nchini kenya
 
Attachments

  • Banned Kenya official.pdf
    157.8 KB · Views: 46
Wamuondoe Amos Wako wamualike Charles Nyachae. Vingine UKAWA wa protest/e.g., watoke nje ya ukumbi
 
Wajummbe wanahitaji mtu wa kuwaelimisha ni Prof Shivji tokea ujana wake mpaka anazeeka alikua akifanya kazi kama hiyo, nashangaa wanachukua watu mpaka nje ya nchi lakini yeye awala hawamtaji.

Kama rtungezungumzia mchakato wa kutengeneza Katiba wakati wa uandaaji wa sheria Prof. Shifvi ni the best, lakini kwa sasa ameshaonesha upande wake hivyo labda aalikwe kujibizana na presentation ya Warioba. Heri Wako kuliko Shivji kwa hapa tulipofikia. Shifvi aweza kuwachanganya zaidi wajumbe kuliko kuwasaidia maana kwa mtu kama Kibajaji aka bingwa wa kutukana sidhani kama anaweza kumuelewa Prof!.
 
Kuna upotoshaji mwingi kuhusu Bwana Amos Wako, anayetajwa kwamba atakuwa Kiongozi wa wanenaji kutoka Kenya, katika Semina ya Bunge Maalum la Katiba, Alhamisi, 20.3.2014. Kwa mfano, Gazeti la Mwananchi, Jumatano 19.3.2014, limeandika katika Uk3,"Semina....itatolewa kesho na magwiji wa Katiba wa nchi hiyo (ya Kenya), akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi hiyo, Amos Wako." Je, ni kweli kwamba Amos Wako alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Kenya? Na je, ni kweli kwamba Amos Wako, alikuwa mstari wa mbele katika kuisaidia na kuiwezesha Kenya, kuwa na Katiba Mpya? Tujadili.

Amos Wako hakuwahi kamwe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Kenya. Amos Wako, alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, kwa miaka 20 (1991-2011), tangu enzi za Rais Moi. Huyu alikuwa ana kasumba nyingi za Watawala wa kwanzakwanza wa Kenya, na alihangaika sana kuzuia Mabadiliko yaliyotokea leo Kenya. Huyu ameletwa na CCM katika Bunge Maalum la Katiba, ili kuwapotosha Watanzania wasioijua Kenya.
 
Kama rtungezungumzia mchakato wa kutengeneza Katiba wakati wa uandaaji wa sheria Prof. Shifvi ni the best, lakini kwa sasa ameshaonesha upande wake hivyo labda aalikwe kujibizana na presentation ya Warioba. Heri Wako kuliko Shivji kwa hapa tulipofikia. Shifvi aweza kuwachanganya zaidi wajumbe kuliko kuwasaidia maana kwa mtu kama Kibajaji aka bingwa wa kutukana sidhani kama anaweza kumuelewa Prof!.

Huyo wako nimewai kumuona kwenye mjadala akimnukuu Prof Shivji kama kuwashawishi waliokuwepo kukubaliana na anachokiongea, sasa leo anaonekana bora kuliko nguri. Shivj anajua jinsi ya kufundisha hata wenye vichwa vigumu wakaelewa.
 
kwenye bunge la katiba sasa hivi kuna strife kama Huyu akileta za kuleta watamtoa baru hata hivyo serikali mbili zimepoteza legitimacy kuwepo tz
 
Back
Top Bottom