Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,301
- 3,411
Wafilisti ni watu walioishi Kaanani ambao waliokuwa maadui wakubwa sana wa Israeli enzi za agano la Kale. Hawa walikuwa ni kundi mojawapo la wenyewe wa nchi ile kabla ya Israeli kuifikia kutoka Misri.
Lakini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.
Kipindi baada ya kipindi walikuwa wakiwashambulia waisraeli, na walipomlilia Mungu, (Waamuzi 10:7-8 ), basi Mungu aliwanyanyulia waamuzi wa kuwaokoa kutoka katika mateso yao, mfano Samsoni.
Wafilisti kwasasa ndio Wapalestina, unaowasikia pale mashariki ya kati, jina hilo lilizaliwa kutoka katika lugha ya wagiriki, ambao waliwaita wafilisti wapalestina. Na ndio mpaka sasa limezoeleka hivyo.
Walikuwa na wakuu/Wafalme wao watano pia kila mmoja na mji wake soma (Waamuzi 3:3). Sasa Miji hii yote ilikuwa kusini magharibi mwa taifa la Israeli.
Hivyo tuwe makini sana na maagizo ya Mungu, anayotuagiza tusiyapuze hata kidogo,.
Lakini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.
Kipindi baada ya kipindi walikuwa wakiwashambulia waisraeli, na walipomlilia Mungu, (Waamuzi 10:7-8 ), basi Mungu aliwanyanyulia waamuzi wa kuwaokoa kutoka katika mateso yao, mfano Samsoni.
Wafilisti kwasasa ndio Wapalestina, unaowasikia pale mashariki ya kati, jina hilo lilizaliwa kutoka katika lugha ya wagiriki, ambao waliwaita wafilisti wapalestina. Na ndio mpaka sasa limezoeleka hivyo.
Wafilisti ni nchi gani?
Kama tulivyoona wafilisti ni watu waliokutwa Kaanani kabla ya wana wa Israeli, lakini sio taifa au nchi. Japokuwa enzi zile walikuwa na miji yao mikuu mitano nayo ni.- Gaza,
- Ashdodi,
- gathi,
- Ashkeloni, na
- Ekroni
Walikuwa na wakuu/Wafalme wao watano pia kila mmoja na mji wake soma (Waamuzi 3:3). Sasa Miji hii yote ilikuwa kusini magharibi mwa taifa la Israeli.
Lakini Habari za wafilisti zinatufundisha nini?
Yapo mambo ambayo Mungu anaweza kutuagiza kufanya yakayazembea na madhara yake yakawa mpaka vizazi vya baadaye, kama vile tunavyoona hawa wafilisti/Wapalestina, hawakuwa mwiba tu kwa Israeli wakati ule..Bali hata sasa ni mwiba mkali sana..Kama wewe ni mfuatiliaji wa diplomasia za kimataifa utaweza kufahamu ni kitu gani kinaendelea pale Israeli saa hii , kila kukicha ni machafuko.Hivyo tuwe makini sana na maagizo ya Mungu, anayotuagiza tusiyapuze hata kidogo,.