Wajue Wafilisti/Wapalestina

Wajue Wafilisti/Wapalestina

Israeli walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu, haki ya Bwana ilitumika kwao kama inavyotumika kwa mataifa mengine. Haki ya Mungu haionyeshi upendeleo. Katika Kumbukumbu la Torati 20:18, Bwana aliwaambia Israeli kuwa moja ya sababu za msingi kwamba jeshi lake lilikuwa kuangamiza mataifa mengi mbele yao ni ili wasiwafundishe kufanya kulingana na tabia zao zote za kuchukiza ambazo wamezifanyia miungu yao. na kuwafanya wamtendee
Mnazidi kuwamegea tu shavu, inamaana wengine wote wakimkosea mungu waangamizwe na watoweke Ila waisrael tu ndo hupewa nafasi baada ya kuazibiwa?, pengine Palestine nao waliazibiwa na wakapewa nafasi ya Israel kuondoka kaanan Tena, mmi naamin mungu hutoa nafasi ya msamaha kwa watu wake wote na so kwa waisrael pekee , haiwezekani kizaz Cha palestina kipotee duniani...ok naskia kunamkataba gan sijui unaazimia kuifuta palestina dunian uliazimiwa Karne ya 20 mwanzoni, hivi ni kwel upo? Wajuvi mnijuze
 
Kaka Mungu sio mjinga kama binadamu, Mungu haangalii sura anaangalia ndani ya moyo. Mpaka afanye maamuzi hayo alishaona mioyo yao sio ya kubadilika.

Ungekuwa wewe ungeangalia sura na kuanza kubagua
Ibadilike kiaje wakati waliumbwa hivyo?
 
Agano la Kale linaonyesha kwamba Wafilisti waliabudu miungu mitatu: Ashtorethi, Dagoni, na Baal-Zebubu-kila mmoja alikuwa na madhabahu katika miji mbalimbali (Waamuzi 16:23, 1 Samweli 31:10; 2 Wafalme 1:2). Matokeo ya akiolojia yanaonyesha kuwa askari wa Wafilisti walibeba sanamu za miungu yao katika vita (2 Samweli 5:21). Inaonekana, pia walikuwa watu washirikina

Wakanaani, walikuwa wamemkataa Mungu na sheria yake. Kulikuwa na mashahidi katika nchi hiyo kwa Wakanaani: Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na familia zao. Walikuwa watu waliomfuata Bwana. hawakuwa wasio na hatia; Wakanaani walikuwa wamefilisika kimaadili na hawawezi kubadilika katika uovu wao.

Israeli walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu, haki ya Bwana ilitumika kwao kama inavyotumika kwa mataifa mengine. Haki ya Mungu haionyeshi upendeleo. Katika Kumbukumbu la Torati 20:18, Bwana aliwaambia Israeli kuwa moja ya sababu za msingi kwamba jeshi lake lilikuwa kuangamiza mataifa mengi mbele yao ni ili wasiwafundishe kufanya kulingana na tabia zao zote za kuchukiza ambazo kuabudu miungu yao. na kuwafanya wamtendee dhambi Bwana.
Kwa nini Mungu muweza wa yote anapata shida saana kuwarudisha wanadam ktk njia sahihi wakati kawaumba yeye mwenyewe.? Si angeagiza tu kuanzia sasa ufahamu wa maovu ondoka...! Teyari pakawa na amani anayoitaka.
 
akini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.
Ina maana Mungu alikuwa na chuki na wafilisti? au ni sababu gani ilimfanya Mungu awatake waisrael kuwaua binadamu wenzao?
 
Alikua na kusudi lake,ila kwa sasa kashatoa pazia lile la kutenganisha binadamu. Kwa sasa kila mtu anafuata sheria zake anakubalika naye
Basi Kama ni hivo tukubaliane kwamba wale wafilist wachache walosalia kaanan baada ya uvamizi walikuwa wema hivo huyo huyo mungu aliewaagiza israel ndo aliewalinda, logic ipo hapa ....Kama mungu alimponya nuhu na watu wachache katika ghalika ndipo alivowaponya waphilist wachache katika uvamiz kaanan, Kama mungu alivoiponya familia ya rutu pale sodoma kwakuwa ni watakatifu na SI waovu Basi ndipo alivofanya kwa waphilist ...... Kupinga hivo ni kukubali kuwa mungu ni mbaguzi?,
Hivi haturuhusiwi kumuabudu mungu kwa lugha yetu na nabii wetu mwingine ambae nae alimtangaza mungu?,
Mbona wajapan wanaabudu mungu japo kupitia vifaa alivoviumba mungu na sjawah sikia wameazibiwa na ni wastaarabu na wanamaadili kuliko Israel wenyewe, vipi kuhusu Korea kaskazini ambako hata wapenzi hawaruhusiwi kushikana mikono hadharan ?.
Vipi kuhusu United Arab Emirates na waislam wote kumuabudu mungu na ni wastaarabu kuliko waisrael na wazungu na wanawaamini mitume wa mungu wote akiwemo yesu mwenyew na wanaishi poa tu?..je mungu atawaazibu Tena Israel wakishinda kumfuta parestina ulimwenguni?...mawazo yangu ni haya yafuatayo
👉Mungu aliumba dunia na vitu vyote
👉Mungu anapenda tumwabudu , tumtumikie na tuwe na huruma na ustaarabu dhidi ya wengine
👉Mungu ameseti dunia kujibalance yenyewe (balance of nature)
👉 Mambo waliopitia Israel sio kwasabab ya uteule wake, kwa mujibu wa dini yangu hakuna wateule mbele ya mungu Wala mungu Hana mtoto Ila Kuna mitume , na manabii wa mungu akiwemo yesu
👉Shida alizopitia Israel na kutafta makazi ni Kama kusurvive Kama ambavo mataifa mengine hufanya, ambapo Vita walivyopigana, wanavyopigana na watavyopigana huko mbeleni vinatokana na mvutano wa kisiasa:mfano yesu alihubiri neno la mungu, watu wakakifuata neno , nae aliwahimiza watu kulipa Kodi kwa mtawala Kwan shughuli za kiutawala zjnagharama mfano chakula cheshini ("vya kaisari mpe kaisari na vya mungu mpeni mungu" kwa uelewa wangu hapa ni kuwa tumikieni utawala wenu Ila msisahau mungu na SI Kama wanavotafsiri wachungaji waliooteshwa na kuuza mafta ya upako ")!.
👉Yesu aliathiri utawala baada ya kundi kubwa la watu kumfuata na yeye kuwa ndio msemaj (imagine watu elfu tano aliowalisha chakula)
Ilikuwa lazima achukiwe na watawala japo alikuwa mwema kwa tuliompendeza mungu
.
Kwa mujibu wa dini yangu mungu hakuzaa , hakuzaliwa, hakuna wa kufanana nae na Wala hatuwezi kuassume yupoje
👉 Msinitukane, hizi no hoja na maswali yangu, hoja inapigwa na hoja
👉Wahadha ssalaam
 
Ina maana Mungu alikuwa na chuki na wafilisti? au ni sababu gani ilimfanya Mungu awatake waisrael kuwaua binadamu wenzao?
Inashangaza Sana mkuu,
Sometimes naambiwa kuwa iliandikwa mapigo kumi pale Egypt ni lazma yatokee, yaani mungu aliwafanya wa Egypt kuwa wagumu nyoyoni ili wawaisrael wajifunze ,je watapata msamaha kwakuwa ilipangwa lazima wawe hivo ?, Nini kiliendelea jamii za watu weusi wakati huo?
Maana na sis tunamhusu mungu
Naambiwa tuliabudu mizimu mbona kizazi hakikupotea Kama ilivopangwa kupoteza wafilisti??

Naamini mungu sio mbaguzi
Hizi stori za kujimegea shavu ili mataifa flan yaogopwe hazimpendezi mungu pia
 
Kwahiyo Mungu alitaka wafilisti wafe wote kama wahutu walivyotaka watutsi wafe wote
Wapalestina ndio wakolofi wanawashambulia islael islaeli imejikingasana sasawao waislael wanawapiga wapalestina kipigocha mmbwakoko
 
Wafilisti ni watu walioishi kaanani ambao waliokuwa maadui wakubwa sana wa Israeli enzi za agano la Kale. Hawa walikuwa ni kundi mojawapo la wenyewe wa nchi ile kabla ya Israeli kuifikia kutoka Misri.

Lakini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.

Kipindi baada ya kipindi walikuwa wakiwashambulia waisraeli, na walipomlilia Mungu, (Waamuzi 10:7-8 ), basi Mungu aliwanyanyulia waamuzi wa kuwaokoa kutoka katika mateso yao, mfano Samsoni.

Wafilisti kwasasa ndio Wapalestina, unaowasikia pale mashariki ya kati, jina hilo lilizaliwa kutoka katika lugha ya wagiriki, ambao waliwaita wafilisti wapalestina. Na ndio mpaka sasa limezoeleka hivyo.

Wafilisti ni nchi gani?

Kama tulivyoona wafilisti ni watu waliokutwa kaanani kabla ya wana wa Israeli, lakini sio taifa au nchi. Japokuwa enzi zile walikuwa na miji yao mikuu mitano nayo ni.

  1. Gaza,
  2. Ashdodi,
  3. gathi,
  4. Ashkeloni, na
  5. Ekroni
(1Samweli 6:17, Yoshua 13:3).

Walikuwa na wakuu/Wafalme wao watano pia kila mmoja na mji wake soma (Waamuzi 3:3). Sasa Miji hii yote ilikuwa kusini magharibi mwa taifa la Israeli.

Lakini Habari za wafilisti zinatufundisha nini?

Yapo mambo ambayo Mungu anaweza kutuagiza kufanya yakayazembea na madhara yake yakawa mpaka vizazi vya baadaye, kama vile tunavyoona hawa wafilisti/Wapalestina, hawakuwa mwiba tu kwa Israeli wakati ule..Bali hata sasa ni mwiba mkali sana..Kama wewe ni mfuatiliaji wa diplomasia za kimataifa utaweza kufahamu ni kitu gani kinaendelea pale Israeli saa hii , kila kukicha ni machafuko.

Hivyo tuwe makini sana na maagizo ya Mungu, anayotuagiza tusiyapuze hata kidogo,.


View attachment 1792182
Acheni nadharia za kufikirika tu.
Hivi umbali wa kutoka Misri mpaka Israel ni kilomita ngapi mpaka ichukue miaka Arobaini?
Ondoa Porojo.
 
Kaka Mungu sio mjinga kama binadamu, Mungu haangalii sura anaangalia ndani ya moyo. Mpaka afanye maamuzi hayo alishaona mioyo yao sio ya kubadilika.

Ungekuwa wewe ungeangalia sura na kuanza kubagua
Mungu muweza ya yote anashindwaje kuwafanya wabadilike?
Hakuna binadamu anashindwa badilika endapo atabadilishiwa mazingira yake,hao watu hawakutaka kubadilika sababu Mila na desturi zao haziwaruhusu kufanya hivyo,Mungu alishindwaje kuwabadilisha wakati ni Muweza wa yote?
hii ndio point yangu muhimu!
 
1. Yaani MUNGU alitaka wapalestina wafe wote ili Israel akae kwa raha mustarehe?
2.Je MUNGU wa UPENDO ndo huyo huyo ?


NB: Imani ni jambo gumu
yaani kumbe tupo wengi mimi nikiwaga nasoma biblia huwa najiuliza maswali kama haya haya nashangaa duh
 
MUNGU SIO DIKTETA AKULAZIMISHE UMUABUDU KINGUVU

Halafu watu hawabadiriki kwa ishara

Mathayo 12:38-41 BHN​

Kisha baadhi ya waalimu wa sheria na Mafarisayo wakamwambia Yesu, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. Jinsi Yona alivyokaa siku tatu kutwa kucha tumboni mwa nyangumi, ndivyo naye Mwana wa Mtu atakavyokaa ndani ya ardhi siku tatu kutwa kucha. Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!
nadiliki kusema huyo Mungu ni kichaa yaani kumbe hatumii jitihada zozote kuwaokoa hao waliopotea na hapo hapo anatumia nguvu kuwaadhibu et kisa hawakumjua yeye na hawamfuati?

Duu huyo Mungu ana double standard na contradictions za kutosha hafanyi jitihada kuwakomboa kwa njia yoyote ila anatumia nguvu kuadhibu!
😥😥😥
 
Ni kwamba mwanzoni, tunapaswa kuzingatia asili ya Mungu. Yeye ni Bwana aliye huru na ana haki kamili ya kutumia nguvu zake kwa njia yoyote atakayochagua. Yeye ndiye Muumba wa vitu vyote; kwa hivyo, ana haki kamili ya umiliki juu ya kila kitu. Ni hamu ya Mungu, na kusudi la Israeli kurithi nchi ya Kanaani. Mungu, ana haki za Muumba. Ni nani awezaye kumwambia, "Kwa nini umenifanya hivi? Je! Unafanya nini? Unafanya nini?"

Pili, Wakanaani hawakuwa watu wasio na hatia kwa njia yoyote ile waliposimama mbele za Mungu na Israeli. Je! Wakanaani walikuwa watu wa amani, waadilifu, na wanyofu?

Hiyo sivyo ilivyo. Wakati Mungu alimuahidi Abrahamu kwamba uzao wake utarithi nchi ya Kanaani, alisema haitafanyika hadi kizazi cha nne baada ya Ibrahimu kwa sababu uovu wa Waamori bado haujakamilika.

Walifanya mambo kama dhabihu ya watoto, uchumba, uasherati, ukahaba wa hekaluni, na matendo mengine mabaya.

Wakanaani, walikuwa wamemkataa Mungu na sheria yake. Kulikuwa na mashahidi katika nchi hiyo kwa Wakanaani: Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na familia zao. Walikuwa watu waliomfuata Bwana. hawakuwa wasio na hatia; Wakanaani walikuwa wamefilisika kimaadili na hawawezi kubadilika katika uovu wao.

Israeli walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu, haki ya Bwana ilitumika kwao kama inavyotumika kwa mataifa mengine. Haki ya Mungu haionyeshi upendeleo. Katika Kumbukumbu la Torati 20:18, Bwana aliwaambia Israeli kuwa moja ya sababu za msingi kwamba jeshi lake lilikuwa kuangamiza mataifa mengi mbele yao ni ili wasiwafundishe kufanya kulingana na tabia zao zote za kuchukiza ambazo wamezifanyia miungu yao. na kuwafanya wamtendee dhambi Bwana.
sasa mambo ya mpende adui yako kama unavyojipenda wewe si Mungu alisema kupitia mwana Yesu kristu Swali kubwa na gumu ilikuwaje Mmungu huyu huyu aamrishe wengine wawaue halafu tena aje kusema mbeleni mpende adui yako??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom