Mapigano kati ya Israel na Palestina yalianza tangu enzi za vita kati ya Mfalme Daud Muisrael na Goliati Mfilisti (Mpalestina)

Boi Manda

Member
Oct 26, 2023
30
36
Miaka ya nyuma kabla ya kuzaliwa Kristo (BC) kulitokea mapigano kati ya Waisrael na Wakaanani ambao ndio wenyeji wa eneo hilo wa kabila la Wafilisti ambao ndio Wapalestina wa sasa

Waisrael walikuwa wakiaminika kuwa ni wacha Mungu na Wafilisti walidaiwa kuwa wapagani kwa wakati huo

Katika vita hiyo nabii Daudi alipambana Goliati ambaye alikuwa Mfilisti na Daudi kufanikiwa kumuua Goliati kwa kumpiga na kombeo kichwani

Inaaminika kwamba Wafilisti walikuwa ni mijitu yenye miili mikubwa hivyo Daud Muisrael alikuwa na kamwili kadogo lakini alimshinda Goliati kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye na ndugu zake Waisrael

Pia kwa kuwa kwa mujibu wa maandiko ya dini Mungu aliwaahidi Waisrael kuwapa mji huo wa Kanani wa Wafilisti (Wapalestna) ndio maana kila wakati kwenye vita kati ya pande hizo mbili Wasrael ndio wanaoshinda na kuungwa mkono na mataifa makubwa ya dunia hii

Awali maandiko kwenye misahafu na maandishi ya wanazuoni wa dini vinasema kuwa wana Wa Israel walikwenda utumwani nchini Misri kwa kipindi kirefu takribani miaka elfu nne

Mungu alisikia kilio cha Israel kutokana na mateso waliokuwa wakiyapata nchini Misri baada ya ndugu yao Yusufu aliyekuwa akiaminiwa na mfalme Farao (Firauni) kufariki dunia

Hivyo Mungu akawahidi wana wa Israel kuwapa nchi ya maziwa na asali ambayo ni Kanani

Ndipo Mungu alipomuinua Musa aende kwa Farao kuwapa ruhusa watu wake Israel watoka utumwani hapo Misri ili waende kumuabudu Mungu na kumtolea sadaka kwenye nchi hiyo ya ahadi Kaanani

Firauni alikuwa mbishi kuwaachia wana wa Israel lakini mapigo aliyopigwa na Mungu hatimaye mwenyewe alisalimu amri akawapa ruhusa Waisrael watoke Misri

Aidha kutokana na Waisrael kutokuwa wavivu na kuwa watu wanafanyakazi nyingi vizuri na ngumu pale Misri na kuifanya nchi hiyo kujitegemea kwa chakula ukilinganisha na Waarabu wenyeji wa Misri

Lakini nabii Musa alimkera Mungu ndipo Mungu alipomwambia hataingia Kaanani hakika atakufa kwa hiyo Waisrael waliingizwa nchi ya ahadi ya Kanani na nabii Joshua

Waisrael walipoingia Kaanani wakauteka mji huo kwa kushinda vita dhidi ya wenyeji wa mji huo ambao ni Wafilisti (Wapalestina) na kuwafurusha na kukaa eneo hilo

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia Adolf Hittler alilisambaratisha Taifa la Israel na kuwaua Wayahudi wengi wale wachache waliosalia wakakimbilia uhamishoni kwenye nchi mbalimbali duniani

Ndipo kipindi hicho Wapalestina wakarejea kwenye mji wao huo wa zamani wa asili wa mababu zao wa Kanani

Baadaye kwenye miaka ya 60 Waisrael wakajiunda tena wakazaliana wakaongezeka na kudai kurejea eneo la Mahariki ya kati kwenye miji yao ya asili waliyopewa na Mungu ya Jerusalemu, Kanani na maeneo mengine ya wakiamini ndio asili yao wakitumia ramani ya kwenye kitabu chao cha dini ya Kiyahudi

Ndipo Umoja wa Mataifa wakagawa baadhi ya miji wakapewa Wapalestina na baadhi wakapewa Waisrael mfano kwenye mji mkongwe wa Jeusalemu upande wa mashariki wa mji huo wamepewa Wapalestina na magharibi wanapewa Israel lakini bado kila mmoja haridhiki na eneo alilogawiwa

Hivyo sababu hiyo ya kugombea ardhi ndio uhasama ulipo kati ya Israel na Wapalestina tangu enzi za nabii Daudi hata kabla ya Kristo mpaka zama hizi za kizazi cha kisasa cha dot com na kistaarabu bado tu hakuna uelewano kati yao

Aidha inasemekana ugomvi huu wa pande hizi mbili kati ya Israel na Palestina hauwezi kwisha mpaka MASIHI WA BWANA YESU KRISTO ATAKAPO RUDI TENA MARA YA PILI DUNIANI UKIONA UGOMVI HUO UMEISHA UJUE KIAMA KIMEKARIBIA TUTUBU DHAMBI ZETU
 
Kama nitakuwa sahihi,wana wa Israel hawakwenda utumwani Misri Bali utumwa uliwakuta wakiwa misri.Kuna sababu nyingi za wao kufanywa watumwa pale misri ila kubwa nikutokana na mfalme aliyekuwa anamfahamu Yusuph kufariki.

Nina swali; Ikiwa Mungu aliahidi kuwapeleka waisrael kanani(ambapo kweli aliwapeleka), alitaka wale wenyeji wa Kanani wakaishi wapi?

Na je, Mungu ni wawote?
 
Yalianza wakati Yoshua kiongozi wa jeshi la Israeli walipozipiga na Wakanaani ambao kiasili ni Wapalestina.

Walizichapa sana ili Waisraeli warithi nchi ya ahadi waliyoahidiwa babu yao Abrahamu, maana Wakanaani walikuwa wakiishi hapo kwenye nchi ya ahadi.
 
Nina swali; Ikiwa Mungu aliahidi kuwapeleka waisrael kanani(ambapo kweli aliwapeleka), alitaka wale wenyeji wa Kanani wakaishi wapi?
Na je, Mungu ni wawote?
Mungu alimuahidi Ibrahim miaka mingi sana kuwa wazao wake au kizazi chake kingerithi nchi hiyo. Mpaka anakufa hakuona ahadi hiyo ikitimia.

Baadaye WAKANAANI wakaenda kuishi hapo kabla ya ahadi ya Mungu kutimia.

Inaweza kusemwa kwamba Wakanaani walikuwa wakaaji wa nchi ambayo haikuwa yao, tayari Mungu alipanga Waisraeli waishi hapo

Kizazi cha kipindi cha YOSHUA ndicho ambacho kiliona utimizo wa maneno ya ahadi hiyo aliyopewa babu yao Ibrahim miaka mingi iliyopita

Mungu aliruhusu Wasraeli wakiongozwa na jemedari Yoshua kuwaangamiza WAKANAANI na kutwaa eneo hilo.

Moja ya WAKANAANI waliopona kwenye shambulizi hilo ni yule kahaba RAHABU na familia yake

NB: WAKANAANI walikuwa wavamizi kwenye eneo ambalo tayari Mungu alipanga kimbele Waisraeli waende kuishi. Kwa hiyo natives ni watu wa kizazi cha Ibrahim (Waisrael)
 
  • Thanks
Reactions: Eco
Yalianza wakati Yoshua kiongozi wa jeshi la Israeli walipozipiga na Wakanaani ambao kiasili ni Wapalestina

Walizichapa sana ili Waisraeli warithi nchi ya ahadi waliyoahidiwa babu yao Abrahamu, maana Wakanaani walikuwa wakiishi hapo kwenye nchi ya ahadi
Kama wapalestina ni wa Caanani basi na waisrael pia ni wa Caanani scientifically wana Dna Moja ambayo imechanganyika na damu za kiroma, kigiriki, kiarabu etc.
 
Kama wapalestina ni wa Caanani basi na waisrael pia ni wa Caanani scientifically wana Dna Moja ambayo imechanganyika na damu za kiroma, kigiriki, kiarabu etc.
Waisraeli sio Wakanaani.

Ugiriki (Greece Empire) na Roma (Roman Empire) zilikuja baadaye sana Mashariki ya kati. Hawana vinasaba (DNA) yoyote na Waisraeli

Unajua Waisraeli waliambiwa wasioe au wasiolewe na wa Kanaani walipoingia nchi ya ahadi

Lakini baadhi ya Waisraeli walianza kuoa na kuolewa na Wakanaani

Inamaanisha kuna damu ilichanganyika ya Waisraeli na Wakanaani (Wapalestina)
 
Kama nitakuwa sahihi,wana wa Israel hawakwenda utumwani Misri Bali utumwa uliwakuta wakiwa misri.Kuna sababu nyingi za wao kufanywa watumwa pale misri ila kubwa nikutokana na mfalme aliyekuwa anamfahamu Yusuph kufariki.

Nina swali; Ikiwa Mungu aliahidi kuwapeleka waisrael kanani(ambapo kweli aliwapeleka), alitaka wale wenyeji wa Kanani wakaishi wapi?
Na je, Mungu ni wawote?
Mungu ni wa wote ndo maana anawapa chakula, maji n.k wema na waovu. Waliokuwa kaanan waliondolewa kwa sababu ya uovu wao, na hata Israel ilikuwa wakifanya maovu kwa mfano kuabudu miungu mingine na wasipomrejea Mungu walikuwa na wao wanaondolewa Kaanani
 
Waisraeli sio Wakanaani.

Ugiriki (Greece Empire) na Roma (Roman Empire) zilikuja baadaye sana Mashariki ya kati. Hawana vinasaba (DNA) yoyote na Waisraeli

Unajua Waisraeli waliambiwa wasioe au wasiolewe na wa Kanaani

Lakini baadhi ya Waisraeli walianza kuoa na kuolewa na Wakanaani

Inamaanisha kuna damu ilichanganyika ya Waisraeli na Wakanaani
Kama mdau hapo juu alivyosema Wapalestina wa sasa wana vinasaba 40-60% vya wayahudi wa zamani, hii imepatikana kwa
1. Kupima mabaki ya zamani ya wayahudi waliozikwa
2. Kupima Dna za sasa za Wapalestina

Kuna study mbalimbali ndio maana ukapata percent zinazo vary.

Na Waisrael/Jews wapo waarabu na wengine kama wazungu mfano hao waarabu (Mizrahi) hawana tofauti yoyote na wapalestina ama waarabu wengine ambao ni Levant.

Kuna waisrael wengine kama hao Ashkenaz Dna zao zina Uzungu zaidi kuliko hata Dna za Middle East.
 
Wapalestina siyo wafilisti
Acha kupotosha umma wa watanzania. Wafilisti (Philistines) ni jamii nyingine kabisa ambayo iliishi katikati ya Gaza na Ashkelon. Jamii hii kwa kuwa ilikuwa Hila za kuwaangamiza Wana wa Israel, Mungu alimtumia mfalme Nebkadnezer kuwa chukua utumwani na Wengine kuwaua katika vipindi hivyo hivyo wana wa israel alipochukuliwa utumwani. Tofauti na wana wa israel ambao Mungu aliwarudisha katika nchi yao, Mungu alihakikisha Wafilisti hawarudi kwao na hivyo walipotelea huko huko utumwani Tafadhali soma Amos 1:8, Ezekiel 25:16,17 Jeremiah 47:4 and Isiah 14:29 kuhusu uangamizo wa Philistines.

Wapalestina wa sasa hivi kiukweli ni Waarabu. kuna clip nitakurushia hapa hata wenyewe baada ya kuona wenzao wanawaacha solemba kwenye hili sakata, Mpalestina huyo analamika kuwa Jamani sisi ni ndugu zenu na KAMA UTATUFUATILIA SISI WOTE TUNA ASILI YETU EGYPT, SAUDIA NA NCHI NYINGINE ZA KIARABU.

Land of Palestine neno hilo lilitumika kwa mara ya kwanza na mwandishi mgiriki akimaanisha ile nchi yote takatifu ambayo kwa wakati anatamka neno hilo nchi hiyo ilikuja mpaka huku Jordan. Warumi (waroma) walipojenga himaya yao kwenye eneo la kusini mwa syria na eneo la Judea katika karne ya 6 CE wakaamua kuliita eneo hilo palestine.

Kuhusu taifa la Palestine, hiyo ni hila ya Waislamu waarabu wakisaidiwa na KGB ya Urusi katika miaka ya 60 kuanzisha Taifa hilo na kuwabatiza Waarabu wa eneo hilo kuwa ni wapalestina ili wajenge uhalali wa kudai nchi yote ikiwa na maeneo wanayoishi wayahudi. Kiujumla nchi hiyo wala haijawahi kuwa ya Waarabu bali ilikuwa ya Wayahudi na Wafilisti
 
Kama mdau hapo juu alivyosema Wapalestina wa sasa wana vinasaba 40-60% vya wayahudi wa zamani, hii imepatikana kwa
1. Kupima mabaki ya zamani ya wayahudi waliozikwa
2. Kupima Dna za sasa za Wapalestina

Kuna study mbalimbali ndio maana ukapata percent zinazo vary.

Na Waisrael/Jews wapo waarabu na wengine kama wazungu mfano hao waarabu (Mizrahi) hawana tofauti yoyote na wapalestina ama waarabu wengine ambao ni Levant.

Kuna waisrael wengine kama hao Ashkenaz Dna zao zina Uzungu zaidi kuliko hata Dna za Middle East.
Baada ya Roman Empire kuisambaratisha Israeli miaka karibu miaka 2000 iliyopita, Wayahudi wengi waliondoka eneo lao kama wakimbizi na watumwa

Wengi walikimbilia maeneo ya Ulaya, baadaye Marekani na Canada na hawa walichanganyika na jamii za huko ndio maana wana mwonekano kama wazungu.

Wengi waliokimbilia Ulaya na Amerika walirudi miaka mingi baadaye kuanzisha taifa la Israel kwenye ile movement ya Zion Movement na rasmi kuunda taifa lao mwaka 1948.

Kuna wale ambao walibaki Mashariki ya Kati wakachanganyika na jamii ya Wapalestina na Waarabu ndio hawa wana mwonekano wa Kiarabu.
 
What happened kwa ambao hawakuondoka? Don't tell me nchi nzima iliondoka, wayahudi waliomkubali Yesu wakawa Wakristo nao waliondoka?

Hao wanaoitwa Levant Arabs sasa hivi hawafanani na waarabu wowote wana muonekano wao unique hivyo inaondoa ile conspiracy theory kwamba wapalestina ni waarabu waliohamia hapo. Wametoka wapi hawa?
 
Back
Top Bottom