Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Hata Kama Mr kuku alikuwa Ana Nia mbaya ya kuwabamiza watu,lakini kwa kijana wa miaka 29,kuweza kuanzisha kitu,na kukusanya bilioni 17!hiyo ni akili kubwa!
Kuna watu wapo serikalini,bungeni kwa miaka 40,hawana hata kakampuni ka kufunga maji.
Vijana kawa ilibidi wakusanywe,wapewe msaada,watumike vzr,ujuzi wao utumike vzr kuanzisha mambo makubwa,
Bahati mbaya,hii nchi Haina thinkers wanaoweza kuwatumia vijana Kama Hawa,ni hakika huyu kijana,akili inachaji kweli kweli!
Sasa atakutana na system ilyojaa,mizee mivimba macho,atahukumiwa,atapigwa faini,atafilisiwa,Kwisha habari,
Serikali yenyewe,ilishindwa kwenye Ishu ya korosho,ikawapa hasara wakulima,
Huyu ilibidi awekwe sehemu,apewe mwongozo,kwa kutumia bichwa lake,alete vitu ,mipango,business plans,ambazo zitainufaisha nchi.
China,kila kijana anafundishwa,lengo lake liwe kuifanya China iwe superpower,achangie anavyoweza,ndio maana wafanyakazi wote wa kichina,waliopo USA,ulaya,lengo lao ni moja tu,iba Siri za kila kitu,uchumi,kilimo,sayansi,pereka nyumbani,China.
Hebu fikiria Kama kila MTZ,popote alipo duniani atakuwa anafanya udukuzi kwa ajiri ya nchi!
Tutakuwa na maspy kibao,na vyanzo kibao vya taarifa/Intel.

Nimesoma mpaka machozi yamenitoka kwa uchungu.

Ni kweli kabisa mkuu, 29yrs kijana anaweza kukusanya 17bil bila kushika bunduki wala kuuza unga just using his good brains na kwa kufanya kitu kinachoonekana... Baada ya watu kukaa naye kuweka naye mambo sawa na kumsimami kijana huyu ambaye nina uhakika uwekezaji ungefanyika kwake in his 35yrs angekuwa level za juu sana.

Kijana kama huyu kumfunga au kumfilisi ni hatari na hasara kwa Taifa aisee, Wapo vijana wengi ambao kipindi hiki au miaka hii ya karibuni wamekuwa wabunifu na kutengeneza hela nyingi wakiwa below 30yrs lakini matokeo yake huitwa matapeli...

Wazee wetu wengi wana akili za kijamaa na hawaamini kama kijana mdogo hawezi kushika mamilioni ya hela na kuwa tajiri huku wakisahau dunia imebadirika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom