Waitara acha kumchonganisha Rais na walimu,CCM halisi hatuko hivyo

Mleta mada ni mwl wa shule za kata kule dongobesh....Hajui kada zingine zaida ya waalimu, msamehe bure.
Pambanua maelezo ya mtoa mada, amezungimzia walimu kwa kuwa ni agizo linawahusu Walimu tu kwa marejeo ya ya naibu Waziri wala hakugusia field na kada nyigine, maelezo yanajitosheleza tena yapo direct.
 
Habari wakuu,hamjambo?

Naomba kumtolea uvivu Huyu bwana,Leo amenukuliwa bungeni kuwa eti wizara yake imesitisha uhamisho kwa walimu kwa kigezo kuwa sababu za walimu hao kuomba uhamisho ni za uongo.Naomba nikiri kuwa Mh waitara anachokifanya ni kumchonganisha Mh.Rais na watumishi Wa umma ili aonekane kuwa ana vunja taratibu na kanuni za watumishi,ikumbukwe kuwa uhamisho ni haki ya mtumishi na upo kisheria.


Binafsi naona mh kashiba madaraka,kasahau kuwa yeye mwenyewe alihama toka CHADEMA na kuja CCM akidai kuwa ni haki yake kuhama,na sasa anaanza kuvuruga morali ya watumishi kwa matamko ya ajabu ,naomba atambue kuwa uhamisho ambao hauna usumbufu ni ule wa watumishi kubadilushana ,kwani huu hausababishi uhaba Wa watumishi ,kama anaona sababu za walimu hawa ni za uongo naomba serikali iruhusu uhamisho Wa kubadilishana ili kutoa nafuu kwa watumishi au walimu ambao mazingira wanayofanyia kazi sio rafiki kwao.

Naomba nikiri kuwa Mwaka 2015 nilikuwa nafanya kazi serikalini nikiwa Lindi,Liwale,hakika nilikata tamaa na morali ya kazi ilipotea nikawa naenda kazini ilimradi,ilifikia kipindi nikaamua kuacha kazi kutokana na mazingira kutokuwa rafiki,nilipomwandikia mkurugenzi nikimwomba uhamisho alikataa kunipa uhamisho kwa Sharti la kutafuta mtu wa kubadilishana naye,Mungu saidia nilihama.

Maoni Yangu napenda kuitaka/kuiomba Serikali iruhusu uhamisho kwa watumishi wa umma walau kwa sharti la kubadilishana

N.B.Waitara kumbuka sababu zako za kuhama toka CHADEMA kuja CCM ni hizo hizo sabaabu zinazowafanya watumishi kuhama toka Kituo A kwenda B
Yale ni maoni yake tu acheni kumsaidia kuyakuza.....juz tu alisema maafisa elimu wapangiwe vipindi.Hujui levi lile
 
Back
Top Bottom