Waislamu wapigana msikitini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu wapigana msikitini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 23, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,916
  Trophy Points: 280
  Date::11/22/2008
  Waislamu wapigana msikitini

  Mussa Juma, Arusha
  Mwananchi

  VURUGU kubwa zilizohusisha waumini wa dini ya Kiislamu ziliibuka jana katika mikoa miwili tofauti na kusababisha damu kumwagika.

  Makundi mawili ya waumini wa dini hiyo yalipambana kwenye Msikiti Mkuu wa Arusha ambako mtu mmoja alichomwa kisu wakati jijini Tanga mabomu ya machozi yakitumika kutawanya Waislamu waliokuwa wakiandamana kupinga tamko la maaskofu kuhusu IOC.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka mjini Arusha chanzo cha vurugu hizo ni kugombea msikiti na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa baada ya viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) kuvamia viongozi wa kamati mpya ya msikiti huo wakipinga kushika madaraka ya kuongoza msikiti huo.

  Katika vurugu hizo zilizotokea majira ya saa 6:30 mchana, mtu mmoja, Abdulaziz Shabani alichomwa kisu ubavuni na mwingine, Hussein Bakari akijeruhiwa baada ya kudaiwa kung'atwa kidole na mmoja wa viongozi wa Bakwata.

  Mwalimu Athuman Yunus wa Shule ya Sekondari ya Bondeni, inayomilikiwa na msikiti huo, akiongozana na Mhasibu wa Bakwata wa mkoa, Ramadhani Nyagawa wanadaiwa kumvamia Sheikh Jamal Shaban alipokuwa akiadhini (kuita watu msikitini kusali) kwa kumrukia kwa kichwa na baadaye ndipo vurugu zilianza.

  Inadaiwa katika vurugu hizo, Mwalimu Yunus alikuwa akisaidiwa na kundi la wanafunzi wake wa Bondeni ambao inadaiwa walikuwa na silaha mbalimbali, walipambana na kikundi kingine ndani ya msikiti huo ambao ni mkubwa kuliko yote mkoani Arusha.

  Hata hivyo, baada ya waumini wengi kujitokeza kutetea viongozi wa kamati ya msikiti waliowateua, viongozi wa Bakwata wa mkoa walilazimika kuomba msaada polisi ambao walifika na kuingia ndani ya msikiti huo kutuliza ghasia, kwa mujibu wa watu waliokuwepo kwenye eneo hilo.

  Polisi, wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), Leonard walitinga katika msikiti huo wakiwa na makachero kadhaa na kufanikiwa kutuliza vurugu na kuondoka na watu watatu.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kueleza watu watatu, Yunus, Abdulaziz na Hussein Bakari kuwa wanashikiliwa kwa mahojiano.

  Akizungumzia vurugu hizo, Sheikh wa Mtaa wa Bondeni ambaye anatambuliwa na Bakwata, Abdalah Omar alisema baada ya kuona msikiti huo hauna uongozi wa kikatiba kwa miaka 17, waliamua kuchagua kamati ya mpito ya waumini 15 kuuongoza.

  Hata hivyo, alisema walishangaa jana kuona viongozi wa mkoa wa Bakwata wakiupinga uongozi halali wa msikiti huo wakati wakijua kikatiba kila msikiti unapaswa kuendeshwa na kamati ya msikiti ya mtaa.

  "Kwa miaka 17 hawataki viongozi wa msikiti...waumini hawataki kwa kuwa kumejaa ubadhirifu hapa... hapa kuna mambo ya EPA ndio sababu wanang'ang'ania," alisema Sheikh Omar.

  Hata hivyo, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Abdulrahman Salum alidai Bakwata inaung'ang'ania msikiti huo kwa kuwa ni mali yao tangu mwaka 1972 walipokabidhiwa na waliokuwa viongozi wa msikiti huo.

  "Sisi ndio tunapaswa kuendesha msikiti kwa kuwa ulitolewa kama wakfu na wazee walioujenga msikiti huu ili utumike kwa manufaa ya mkoa mzima," alisema Sheikh Salum.

  Hata hivyo, alikataa kufafanua zaidi juu ya mgogoro ulioibuka hivi sasa kwa maelezo kuwa katibu wa Bakwata wa Mkoa wa Arusha, ambaye ndiye kaimu katibu mkuu wa baraza hilo, Ally Mzee alikuwa njiani kuja Arusha kuzungumzia mgogoro huo.

  Licha ya kuwa na msikiti, eneo hilo lina viwanja, shule ya sekondari na maduka zaidi ya 20 ambayo kwa wastani huingiza kila mwaka zaidi ya Sh100 milioni, lakini taarifa za mapato hayo hazijawahi kutumwa Bakwata.

  Mwaka 1998 viongozi hao wa BAKWATA walivunja moja ya majengo ya ghorofa yanayozunguka msikiti huo kulipokuwa na chuo cha Kiislamu na kumkodisha mfanyabiashara mmoja maarufu kwa miaka 30 ili ajenge kitega uchumi, lakini baadhi ya waumini walikwenda mahakamani na kushinda kesi ya kupinga upangishwaji wa eneo hilo.

  Kutoka Tanga, Burhani Yakub anaripoti kuwa, jiji hilo jana mchana liligeuka kuwa uwanja wa mapambano baada ya askari wa kikosi cha kuzuia ghasia kutumia mabomu ya machozi na risasi kutawanya Waislamu waliokuwa wakiandamana kupinga kauli iliyotolewa hivi karibuni na Baraza la Maaskofu kuhusu Taasisi ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) na kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.

  Maaskofu waliitaka serikali kutojiunga na taasisi hiyo kwa kuwa ni ya kidini na kuonya kuwa serikali isiachie suala hilo kuwa kubwa.

  Lakini jana Waislamu wa mjini hapa, ambao walikataliwa kibali cha kuandamana, walitekeleza azma yao baada ya sala adhuhuri na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya maandamano hayo.

  Mamia ya Waislamu wanawake kwa wanaume walijitokeza jana katika msikiti ulio Barabara ya 15 ujulikanao kwa jina la Masjid Qubba na baada ya sala ya Ijumaa walianza kuandamana kuelekea Viwanja vya Tangamano ambako walipanga kuwasilisha ujumbe wao kuielezea dunia kutoridhishwa na tamko hilo la maaskofu.

  Baada ya kuuswalia mwili wa marehemu ambao ulikuwa umefikishwa hapo kabla ya kupelekwa makaburini kuzikwa, watu hao walianza maandamano yao.

  “Waislamu, nadhani mmeshaona magari ya FFU yakipita nje kututisha tusitimize azma yetu ya kuandamana... tukimaliza kuswalia mwili huu wa marehemu, tutaanza rasmi maandamano, hivyo kila mmoja aswali akijua kuwa hataswali tena swala ya alasiri,” alisema Imamu wa msikiti huo.

  Alisema pamoja na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na askari wa FFU kwa kupitishaa magari msikitini hapo kama ishara ya kuwaonya, Waislamu hawangesita kwa kuwa wamechoka kuamuliwa mambo yao na viongozi wa dini ya Kikristo.

  Baada ya kufika eneo la kituo kikuu cha mabasi walizingirwa na magari manne ya polisi aina ya Landrover. Polisi waliwaamuru watawanyike, lakini wakakataa na ndipo walipotumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya. Polisi walitumia kama saa moja kutawanya Waislamu wote

  Wakiongozwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Anthony Rutashubulugukwa, askari hao waliwakamata watu 10 wanaodaiwa kuongoza maandamano hayo.

  Baadhi ya Waislamu walioandamana waliilaani serikali kwa kuwazuia kuelezea hisia zao na kwamba haikuwafanyia haki.

  “Hatuwezi kuvumilia uonevu kama huu... tunapigwa hivi kama hatuko katika nchi yetu, huu ni utawala gani hata wakati wa enzi za utawala wa Mjerumani hatukufanyiwa hivi,” alisema Mwanakombo Masia (60), ambaye pia alikuwa miongoni mwa waliopigwa mabomu.

  Katibu wa Baraza la Wanawake wa Kiislamu wa Bakwata, Mkoa wa Tanga, Aisha Kassim alisema ni vema Rais Jakaya Kikwete atangaze kuwa Tanzania ni nchi ya Wakristo na kwamba Waislamu hawana haki.

  Habari zilizopatikana baadaye jioni jana zilieleza kuwa watuhumiwa watatu, Yunus, Abdulaziz na Hussein Bakari waliokuwa wanashikiliwa kwa mahojiano waliachiwa huru jana jioni.

  Baadaye jioni kamati ya msikiti iliuteka msikiti na kuurudisha mikononi mwao huku ikiwatimua maafisa wa Bakwata na hatimaye kubadilisha vitasa vyote vya msikiti huo na kuuweka chini ya ulinzi wao.

  Mwananchi liliwashuhudia kamati hiyo ambayo iliongozwa na vijana wa mjini Arusha na ambao walikuwa wakidai kwamba msikiti huo ni wa mtaa na si wa Bakwata hivyo kuwataka Bakwata wasiwaingilie.

  Hali iliendelea kuwa tete huku kila mmoja akimwinda mwenzake kwani Bawata nao walionekana kutokubali kufanyika kwa utekaji huo na huenda vurugu zikaendelea.
   
 2. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2008
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hao ndio BAKWATA!!! Kazi waliyopewa 1968 na Serikali ya Nyerere kuwadhibiti Waislamu na kuwachonganisha nao! kila kukicha BAKWATA na Waumini ni ugomvi usio na mwisho! hakika Serikali yetu ina Dini na wenye akili timamu ndio hutambuwa hili! mbona kunapotokea ugomvi ktk Makanisa hakuna askari hata mmoja anapelekwa Kanisani? mfano, kule Arumeru kulitokea machafuko miongoni mwa Walutheri lakini Serikali ilituma watu muhimu kusuuhisha, huko Mwanga kulikuwa na mgogoro wa Kanisa na Mzee Cleopa Msuya lakini pia ulimalizwa na Serikali bila ya kutuma Askari!
  Kwanini Waislamu wanadharauliwa hivi? ni wazi waumini wa Msikiti wa Arusha hawataki BAKWATA kuingilia mambo yao ya Msikiti lakini kwa kuwa BAKWATA ni chombo cha Serikali basi hawatakubali kuona Waislamu wanapata maendeleo!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tudhihirishie unayoongea tafadhali..tumechoshwa na malalamiko yasiyo na msingi yasoisha..
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Msikiti Mkuu wa Arusha unagombewa kwasababu unaingiza fedha nyingi,makundi yote yanatafuta ulaji tu nasi kuwasaidia waislam.Wazee wanaoendesha msikiti hawataki kufanyakazi nyingine ya kujiingizia kipato halali badala yake wanategemea mapato ya msikitini kwa manufaa yao binafsi.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kumbe tatizo ni rizki kwa hawa wazee,na wale vijana tatizo ni nini, mpaka kwenda kupigana kwenye nyumba ya ibada?
   
 6. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Aloo...!

  Kuna kundi lingine lina madai kwenye hii serikali ya kishkaji? Wakati ndio huu!!!
  Hakuna kulala....  [​IMG]


  Mimi dai langu kubwa ni mabadiliko ya Katiba!
  .
   
 7. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  JEE mapigano hayo yanakaribia yale ya muembe chai ???????????
   
 8. C

  Chuma JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kupigana msikitini ni jambo baya...Kwa waliopo karibu na wahusika ni vema mkaangalia namna bora ya kuumaliza hilo gogoro....

  kwa OIC wananchi wa Tanga wana HAKi ya kuandamana..Jeshi la polisi Tanga yatakiwa ijifunze kutoka DSM namna wenzao wanavyoweza ku-handle maandamano...otherwise mapambano na wananchi yana mwisho!!!!
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wana jambo inasikitisha sana kuona hata hapa JF kuna watu wenye mtazamo wa namna hii. Inafurahisha sana kuona vurugu zinatokea msikitini wanapigana watu kugombea msikiti kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi lawama zinapelekwa kwa wakristo na serikali. Serikali yetu ina dini gani? dini gani hiyo ambayo waumini wake ni kina Kikwete, Membe, Kingunge.....Kama waislamu hawajaendelea ni nani ananufaika? Na kama waislamu wakiendelea ni nani watanufaika?
  Wanajambo mnaofahamu hili kiundani naomba mueleze zaidi ukweli kuhusu shutuma anazotoa huyu mwenzetu.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...inasikitisha, inahuzunisha, inaghadhibisha, na inafadhaisha kuona ni jinsi gani mwana wa Adamu anavyoweza kuacha mafundisho ya vitabu vyote vitukufu kwa manufaa ya tumbo lake.

  "...mtapoona Mwanaadamu anaiacha imani yake kwa kugombea mali,...!"
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  kibaya zaidi anapomshutumu mwenzake wa dini nyingine huku tatizo akiwa ni yeye mwenyewe, na kuwaingiza wenzake wa dini yake kwenye mwamvuli wa kuficha maovu yake. Anasemwa waislamu, lakini ukweli hapa ni yeye mwenyewe na sio waislamu
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...alaah?

  Kumbe hao walokuwa wanashutumiana pale Msikiti Mkuu Arusha sio waumini wa dini ya kiislamu? umekusudia nini labda nilichokosea kusoma between the lines, nielimishe Bongolander.
   
 13. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naaam ndugu yangu... hili ndio tatizo la watu wa kupandikiza.. ila mimi niajiuliza swali moja hawa jamaa "bakwata" wao ni waislamu au ni makafiri wanaojua kiarabu? maana kama wanaswali na kusoma Qur'an sijui kinachowafanya wawe hivyo.. au ndio uthibitisho wa kauli ya Mtume kuwa "wanafiki ni hatari kuliko makafiri"

  Waislam zindukeni na muone namna nyerere alivyoivunja Jumuiya wa Waislam ya Afrika Mashariki na kupandikiza fitina hii bakwata.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Niliogopa kuchangia chochote mwanzoni maana nilijua lazima mchawi atafutwe kutoka nje ya Imani!

  Kadogoo, kule Meru Serikali (Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya ndani) alipeleka vikosi vya FFU baada ya Walutheri kujeruhiana na kuchomeana mali (nyumba na Mashamba). Kule Mwanga wameanza tena. Mbona wao hawajamtafuta mchawi nje ya kanisa lao? Yaani watu mkitofautiana lazima lawama atwishwe mtu wa nje? Jamani, kuweni wakweli kwa nafsi zenu.
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Inakuwaje waumini wa dini ya kiislamu wapambane halafu inakuja argument ya kuwa source ni wakristo. Inakuwaje mtu anapambana na mtu mwingine kwa sababu za maslahi yake binafsi, anasingizia "sisi waislamu" "sisi waumini" lakini ukiangalia zaidi hakuna sisi wala waislamu, ila ni maslahi yake binafsi. Ninachosema ni kuwa mtu anatumia jina la waislamu kwa manufaa yake binafsi.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And we wonder why kwa nini nchi haijaendelea mpaka leo!!!!!!!!!!!
   
 17. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu Chuma, hebu soma hii taarifa kama ilivyoandikwa na Tanzania Daima 29 Nov. 2008 kwenye blue font:- utaona kuwa tarehe waliyoruhusiwa kuandamana si waliyoandamana!

   
 18. M

  Mong'oo Member

  #18
  Nov 24, 2008
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani ulikuwepo kwenye vurugu za Arumeru? Maana mi nilikuwepo lakini unachokisema hapa ni UONGO. Polisi walikuwepo tena na mabomu ya machozi. Kwa kumbukumbu yangu wale walikuwa na vidumu vya maji wakipigwa mabomu wananawa uso na kuendelea na fujo.
  Samahani hii ni ktk kuboresha JF isioonekane tofauti na objective yake
   
 19. u

  under_age JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2008
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  aaakh mchawi wa waislam tanzania ni huyu chui mwenye ngozi ya kondoo anaejiita bakwata.elimu yangu ni ndoooooogo sana lakini chuoni niliambiwa muislam wa kweli hawezi kushirikiana na kula sahani moja na serikali iliojaa dhulma. na tunamuona bakwata jinsi gani anavyoshirikiana na serikali dhalim ya ccm. akili na jibu lipo kichwani mwako.
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mada ilianza vizuri na baadaye inaanza kwa kulaumu watu wengine.
  Waliopigana ni waislamu. Na Bakwata ni mali yao wenyewe. Viongozi wa Bakwata wanajichagulia waislamu wenyewe na si serikali. Kama hawaridhiki nao makosa ni yao wenyewe, wao ndio wamewachagua. Kama waliwachagua baada ya kupewa kitu kidogo au sania la pilau, basi wasibebeshe watu mizigo.
  Ni kama vile sasa sisi tulivyoliwa hapa Tz je tumbebeshe nani mzigo?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...