Waislamu Tunadai nini Kwenye Katiba Mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu Tunadai nini Kwenye Katiba Mpya?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by thatha, Apr 20, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [h=2]Waislamu Tunadai nini Kwenye Katiba Mpya?[/h]Waislamu sehemu mbali mbali nchini wamekuwa wakiliuliza Jukwaa kuhusu ni yepi madai ya waislamu katika utoaji maoni yatakayokusanywa na tume? Yafuatayo ni baadhi ya madai yetu ya msingi kabisa na mengine mtaarifiwa baadae kupitia makongamano na vikao husika;-

  • Mahakama ya Kadhi iwepo nchini na iwekwe kwenye katiba .
  • Usekula wa dola ufafanuliwe maana kimaneno nchi haina dini lakini katika utendaji wa serikali nchini kama vile kuna dini inayopewa kipaumbele.
  • Uhusiano wa kimataifa Tanzania ijiunge na OIC vinginevyo uhusiano na Vatican pia uvunjike.
  • Uhuru wa ibada utambuliwe (hivi sasa kuna uhuru wa imani na si uhuru wa ibada kwani waislamu wanapotekeleza baadhi ya ibada wanabughudhiwa. Mfano, kusali sala tano kwa wanafunzi, maaskari na wafanyakazi, uvaaji wa hijabu, ufugaji ndevu, bunge kuendelea siku za ijumaa, mitihani kufanyika siku za sikukuu za Idi n.k.)
  • Haki za kimakundi ziainishwe, zitambuliwe na zitiwe katika katiba.
  • Sheria za Kiislamu zitambuliwe na ziheshimiwe. Sheria za Kiislamu za ndoa, mirathi na talaka na haki za wanawake ziheshimiwe.
  • Siku za mapumziko zizingatie imani za dini na siyo wakristo peke yao (Jumamosi – Wasabato, Jumapili – Madhehebu mengine ya Wakristo).
  • Ubaguzi wa kidini unaofanywa na serikali usiwepo. Mfano, serikali kuingia mikataba ya kutoa pato la taifa kwa wakristo kupiti MoU.
  Haya ndiyo baadhi ya madai yetu katika mchakato wa katiba. Waislamu tudai madai haya na hayo mengine tutakayoyatoa.
  Imetolewa na;
  Sheikh Muhammad Issa


  source
  jukwaa la waislamu
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mkuu nadhani sasa hivi ingekuwa Watanzania tunadai katiba mpya gani? Na sio waislamu, wakristo, wapagani, haya mambo hayatujengi kabisa charter ya uhusiano wa Tz na Vatican ni tofauti sana na ya OIC, Mahakama ya kadhi haina Tija kwa watanzania bali ni muhimu kwa waislamu tunataka katiba yenye tija kwa watanzania wote na si waislamu au makundi mengine basi.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tunadai kila mmoja ajisalimishe kwa mola wake aliyemuumba. A silim.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pedestrian thinking.
   
 5. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 631
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 80
  Mahakama ya Kadhi iwepo nchini na iwekwe kwenye katiba

  NAUNGA MKONO MAHAKAMA YA KADHI LAKINI ISISHIRIKISHWE SERIKALI, SABABU MAHAKAMA YA KADHI NI MOJA YA IBADA YA KIISLAMU, NA SERIKALI INA WATU AMBAO SIO WAISLAMU NA HAWAJUI JINSI YA MUUNDO NA IBADA YA KIISLAMU.SABABU WASIOKUWA WAISLAMU WAKI TULETEA HELA HARAMU WENGINE WALIDOKEZA YA KITIMOTO, AU HELA YA MSAADA KUTOKA ISRAEL NA KWA WAISLAMU WENGI WANAJUA KUWA WAISLRAELI NI ADUI WA KIISLAMU.
  ISITOSHE WAHINDU, WASINGHA WAPAGANI, WANGONI, WANYAMWEZI, WAZARAMO NAO WAKIJA KUDAI HIVYO JE SERIKALI ITABAKI NA HELA?
  HATA HIVYO JE WAISLAMU WANASHINDWA KUANZISHA MAHAKAMA HII KIYAKE? WENGI WETU TUNAJUA BAKWATA ILIANZISHWA NA SERIKALI NA KILA WAKATI WAISLAMU WANADAI BAKWATA NI CHOMBO CHA SERIKALI, JE HII MAHAKAMA AMBAYO WAISLAMU WANADAI IANZISHWE NASERIKALI,JE WAISLAMU HAWATALALAMIKA KUWA NI CHOMBO CHA SERIKALI NA NI HARAMU??

  Usekula wa dola ufafanuliwe maana kimaneno nchi haina dini lakini katika utendaji wa serikali nchini kama vile kuna dini inayopewa kipaumbele
  SIJAKUELEWA MKUU HAPA


  Uhusiano wa kimataifa Tanzania ijiunge na OIC vinginevyo uhusiano na Vatican pia uvunjike
  KAMA NIJUAVYO MIMI KUWA VATICAN NI NCHI NA SIO JUMUIA KAMA OIC.HIVYO KAMA OIC NI NCHI NA SERIKALI HAIJAFUNGUA UBALOZI WA OIC NAFIKIRI NI MAKOSA

  ]Uhuru wa ibada utambuliwe (hivi sasa kuna uhuru wa imani na si uhuru wa ibada kwani waislamu wanapotekeleza baadhi ya ibada wanabughudhiwa. Mfano, kusali sala tano kwa wanafunzi, maaskari na wafanyakazi, uvaaji wa hijabu, ufugaji ndevu, bunge kuendelea siku za ijumaa, mitihani kufanyika siku za sikukuu za Idi n.k.)

  WAKRISTO NA WAPAGANI NAO WANA SALA ZAO VILE VILE, JE SERIKALI INAWAPENDELEA MADHEHEBU MENGINE KUFANYA SALA ZAO WAKATI WAKIWA KAZINI NA KUWANYIMA UHURU HUO WAISLAMU? KAMA INAWANYIMA BASI HAKUNA HAKI HAPO

  Haki za kimakundi ziainishwe, zitambuliwe na zitiwe katika katiba

  SIJAKUELEWA MKUU HAPA

  Sheria za Kiislamu zitambuliwe na ziheshimiwe. Sheria za Kiislamu za ndoa, mirathi na talaka na haki za wanawake ziheshimiwe
  SERIKALI IMEDHARAU NAMNA GANI SHERIA HIZO? LABDA KTK MAHAKAMA YA MIRATHI ITAKAYOANZISHWA MAMBO HAO YAWEKWE

  ]Siku za mapumziko zizingatie imani za dini na siyo wakristo peke yao (Jumamosi – Wasabato, Jumapili – Madhehebu mengine ya Wakristo
  NAKUUNGA MKONO

  Ubaguzi wa kidini unaofanywa na serikali usiwepo. Mfano, serikali kuingia mikataba ya kutoa pato la taifa kwa wakristo kupiti MoU
  NAFIKIRI RAISI WETU ALISHALITOLEA UFAFANUZI, ALISHASMA KUWA WAISLAMU HAWAJAOMBA HELA HIZO KAMA MOU. NA HAPA NAONA KAMA KUNAKUJICHANGANYA.KAMA HUTAKI WAKRISTO WAPENDELEWE SASA KWA NINI WAISLAMU WADAI HOJA YA MAHAKAMA YA KADHI? HAPO HUONI KUWA WAISLAMU WANATAKA WAPENDELEWE? !!!![/SIZE][/COLOR]
   
 6. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiamua kuingia JF uwe tayari kuwa wazi na usionekane mtu anayetafuta huruma ya watu hapa. Me binafsi sina ugomvi na kikundi cha watu wa imani fulani kutaka nini kiwemo kwenye katiba ili mambo yao yaweze kwenda. Lakini tukumbuke katiba siyo ya dini fulani wala ya kikundi kidogo cha watu wanaohitaji matakwa yao yaingizwe ili waishi vizuri. Tukiuchukulia mchakato wa katiba kwa mtazamo huu hatuwezi kupata katiba ambayo italijenga Taifa, ila makundi ya watu. Kwa mfano, CCM wana mambo yao ambayo wangelipenda yawemo kwenye katiba ili waendelee kubakia madarani milele daima, CHADEMA nao wana yao ambayo wanapenda yaingie ili washike dola, CUF tayari walishawasilisha mswada wa katiba, siyo mawazo...no mswada wa katiba kwenye wizara ya Sheria na Katiba. Vivyo hivyo NCCR, Tadea, TLP, ADC, Wakatoliki, Waanglikana, Wasabato, AIC, TAG, Full gospel bible fellowship, waalimu, madaktari, wabunge, Wakulima, Wafugaji, Machinga, Mama lishe na kila aina ya kundi ambalo unalifahamu.

  Sasa fikiria tukigawanyika katika makundi haya na kila kundi likaainisha mahitaji yake na ndiyo kikawa kilio chao....tutapata katiba ya aina gani? Hapo kutakuwa na katiba kweli au utakuwa utani tunaleta. Maana kwenye madai ya waislamu haujasema kuwa UMILIKI WA ARDHI, MATUMIZI MAZURI YA RASILIMALI, MADARAKA YA RAIS, TUME HURU YA UCHAGUZI, MUUNDO WA MUUNGANO, MUUNDO WA SERIKALI, SERIKALI IWE NA WIZARA NGAPI ZA KUDUMU NA UKOMO UWE WIZARA NGAPI, KAMA NI MUHIMU KUWA NA WAKUU WA WILAYA, DAS, RAS, NA WAKURUGENZI KATIKA ENEO MOJA LA KUFANYIA KAZI, VIPI HAKI ZA WATOTO, na mengine mengi ya msingi. Haya hayahusiani na kundi lolote miongoni mwa makundi ambayo nimeyataja hapo juu. Tukisema kila mmoja alizungumzie kundi lake, nani atazungumzia masuala ya kitaifa kama ambayo nimeyaainidha kwa herufi kubwa hapo juu. Hauoni kuwa tutakuwa hatulitendea haki taifa letu?

  Hivi waislamu mkipewa mahakama ya kadhi ndiyo kero zenu zitaisha? Tanzania ikijiunga na OIC, muislamu wa Kagera na Kigoma vijijini wananufaika nini na OIC? Au ni ulaji wa Mashekh tu? Na najiuliza kama mtaruhusiwa kupumzika na kutokufanya kazi siku ya ijumaa kero zinakuwa zimeisha? Mbona mimi mkristu Jumapili napiga kazi kama kawaida? Dini ni mapokeo tu...hapo awali kabla ya waarabu na wazungu hatukuwa na Ijumaa, Jumamosi wala Jumapili, tulikuwa tunafanya kazi kila siku za juma na mambo yetu yalikuwa safi kuliko hata sasa ambapo tunajifanya watu wa Mungu ilihali hatuzifuati amri zake...nini dini bwana? Angalia nchi ambazo zimejipambanua kuwa za kidini, Iraq, Iran, Libya, na sasa Sudan kaskazini, Yemen, Syria, Afghanstan na nyingine nyingi, mambo siyo shwari huko...kila siku watu wanakufa kama mbwa...!

  Nashauri...tuangalie na tuchangie mambo ya msingi kwenye tume ya katiba. Tukileta mambo ya udini, wengine wataleta mambo ya ukanda, tutafika mbali na kuleta mambo ya ukabila ya Ukijiji, Hatutabaki salama. Tuzungumzie mambo ambayo yanatufanya kuwa wamoja kama watanzania. Dini kila mtu ana yake na wengine hawana kabisa na wanaishi, tena maisha mazuri bila stress, dini zenyewe za sasa, wachungaji, mapadri na mashehe wamekuwa wachumia tumbo...hakuna lolote...

  Mwalimu Nyerere alisema, najua utapinga kwa sababu wewe Muislamu...."Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi. Haiishi tu kusema wewe ni mkristo na mimi ni muislamu. Ukimaliza kusema mimi Mtanganyika na wewe Mzanzibar, tukifika pemba tutasema wewe Mpemba na mimi Muunguja, huku bara tutasema wewe wa Kaskazini na mimi wa kusini, Hata kwenye dini, leo unajiita muislamu na kuwaorganize waislamu mambo yenu...siku yakitokea ya kutokea, utasema wewe mshiha...na mimi msuni...wewe muislamu wa tabora na mimi wa mwanza....hadi makanisani....wote ni wakristo...lakini tutasema wewe mkatoliki, na mimi mlutheri...tutabaguana hadi kwenye familia zetu, na tukicheza na dhambi hii, tutaanza kubagua hadi viungo vya miili yetu....wewe mkono wa kushoto na wewe wa kulia." Dhambi ya ubaguzi siyo nzuri...

  Maji yanatuunganisha wote, Maliasili zetu kama misitu, wanyama, madini, gesi, mafuta na makaa ya mawe yanatuunganisha wote kama watanzania. Tukipata katiba nzuri yenye mgawanyo mzuri wa madaraka, kupunguza madaraka ya rais, kuunda tume huru ya uchaguzi kuondoa wakuu wa wilaya, kutengeneza serikalil za majimbo, wote waislamu na wakristo tutafaidika na haya mambo...siyo habari za mahakama za kadhi, kuvaa hijabu, kuabudu...haya nimapokeo tu, yajadiliwe misikitini yaishie huko...sasa tukifikia kuweka kwamba sasa kuvaa hijabu ruksa...kwenye katiba, inakuwa nchi ya Kiislamu sasa. Au tuseme sasa Mahakama ya kadhi hiyo, serikali itagharamia....na wakristo wakidai yao....? Nani atasema serikali haina dini tena? Tuache hii mambo....Asante, naamini utakuwa umenielewa vyema.

  TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED...YES WE CAN...TUACHE UDINI...TANZANIA MBELE KAMA TAI...MENGINE YANAFUATA.....
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kamata 5. Hapa sina la kuongeza, umemaliza yote.
  Ah! Nimesahau kuwa na Wapemba nao wana madai yao:
  "Msembwe ukeshe na wamanga wakopwe", hapo ndio katiba itakamilika.
   
 8. MDAU JR

  MDAU JR JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu una taka watanzania gani tena? waislamu wanaotajwa hapo ni wa hapa Tanzania, kwa hiyo yakiwekwa hayo yatakuwa tija kwa watanzania kama vile fedha zetu za walipa kodi wote wa tanzania zinavyopelekwa makanisani kupipitia MoU kwa hiyo wanaonufaika ni wa wakristo wa Tanzania, kwa hiyo ni tija kwa watanzania. hulijuwi hilo?
   
 9. mama yuva

  mama yuva JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Very well said. Nchi za kidini hata zile za kikiristu kama ireland na Ireland kaskazini pamoja na hizo za kiarabu wanachi wanaonja joto ya jiwe kwa ajili ya manufaa ya wachache tu. Nadhani hata serikali huenda iliingia mikataba na wakristu ili waislamu wawe na cha kusema. kama ikiondoka Vatican tusiwe na mahakama ya kadhi basi sie wakatoliki tunasema iondoke tu. tunahitaji uhusiano na Mungu si Vatican wala IOC. Mahakama ya kadhi sina shida nayo as long as haitatumia kodi yangu na ya familia yangu kujiendesha, ijiendeshe yenyewe kama vatican inavyojiendesha. tunaigomea kwa sababu mnataka kutumia kodi zetu kibinafsi lakini kama kwa hela za mafuta za waarabu basi endesheni tu.
  Hata uhuru wa kuabudu ni wewe binafsi, mie mkatoliki nasali Malaika wa Bwana saa sita, saa tisa na saa kumi na mbili, haina interference na kazi yangu wala nini, as long as kuna nafasi hata nilipokuwa hsule na kwenye mtihani, nikitaka kusali nilizali tu. nafanya kazi na waislamu na saa saba anayetaka kuswali anaswali anayeona inaingilia maslahi yake binafsi haswali. napangiwa safari kazini Jumapili na sikukuu naenda tu napanga muda wangu vizuri nasali kabla ya safari au baada ya safari ikishindikana nafanya ibada bedroom nikienda kulala.
  Nahdani watu wengine wanatakiwa ku stop whining na kuangalia issues za msingi kitaifa.
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Balozi wa OIC aje tu nchini, atapewa jengo apange (kama yupo lakini)
   
 11. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu ukitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe isije ikatokea badae serikali ikataka kuingilia utendaji wake manake hilo ndo hatari zaidi kuliko hata kushirikishwa sasa hivi. Think twice
   
 12. MDAU JR

  MDAU JR JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Mkuu kutokana na nukta zifuatazo hapa chini huoni kuwa mzani umeelemea upande mmoja?

  1.Uhuru wa ibada utambuliwe (hivi sasa kuna uhuru wa imani na si uhuru wa ibada kwani waislamu wanapotekeleza
  baadhi ya ibada wanabughudhiwa. Mfano, kusali sala tano kwa wanafunzi, maaskari na wafanyakazi, uvaaji wa hijabu,
  ufugaji ndevu, bunge kuendelea siku za ijumaa, mitihani kufanyika siku za sikukuu za Idi n.k.)

  2.Siku za mapumziko zizingatie imani za dini na siyo wakristo peke yao (Jumamosi – Wasabato, Jumapili – Madhehebu
  mengine ya Wakristo).

  Suala la waislamu kuomba MoU kama ulivyosema limefanyika bila mafanikio kwa taarifa yako, na uwezekano wa kuondolewa hiyo kitu kwa wkristo umeshindikana licha ya kupigiwa kelele kwa muda mrefu ya kwamba kodi zetu sote zinanufaisha sehemu tu ya watanzania ndiyo maana sasa tunakuja na hoja hii kwamba maadam nyie mna hiyo MoU siye tugharamiwe hiyo MAHAKAMA YA KADHI ambayo itakuwa ikishughulikia masuala yanayowahusu waislamu tu (Ndoa na Mirathi) maana kuna baadhi ya watu wanapotosha wengine kuwa mahakama hii itakuwa ikihukumu wezi kukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe hali inayopelekea wapinzani wa suala hili kuwa wengi( nina imani Lidoda si katika hao)

  Juu ya uanzishwaji:
  Ndg Lidoda, Waislamu hawaombi serikali ianzishe mahakama hii, Sisi tunachotaka mahakama hii IWEKWE NA ITAMKWE KWENYE KATIBA na igharamiwe na serikali kwa kuwa waislamu pia wanalipa kodi kama ilivyo kwa wakristo wanavyopata fedha kupitia MoU. Itaanzishwa na waislamu wenyewe na kuendeshwa na waislamu wenyeewe kwa mujibu wa taratibu za kiislamu.

  Kuhusu sala:
  Ninavyofahamu mimi ni kuwa sala zilizo za lazima kwa wakristo ni Jpili na Jmosi kwa wasabato sala zingine si za lazima.
  Kwa waislamu sala tano NI LAZIMA si Ijumaa pekee. kwa hiyo huwezi kulinganisha na sala zingine kwa wakristo ambazo ni nje ya zile za Jmosi na Jpili.
  Kutokana na hali ilivyo sasa mwanafunzi wa kiislamu anatakiwa kuopt either adhuhuri ande akasali or ahudhurie kipindi darasani, kadhalika kwa mtumishi; afanye kazi aliyopewa na bosi wake au aache aende kusali adhuhuri au la'asiri af aone kitakachomtokea.

  I hope Lidoda na wengine sasa mtakuwa mmefahamu uzuri kabisa.

  Asante.
   
 13. mama yuva

  mama yuva JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Hicho kipengele cha sala, na sisi wengine tunazo sala za lazima, ni kwamba hatuzipigii debe tu na kuzitumia kwa ajili ya manung'uniko. Tuna rosary tuna njia ya msalaba, na nyingine, si sawa kusemea wengine wrongly kwa ajili ya kupata sympathy vote, tunazo sala za lazima na za masaa mbalimbali na wengine tunazifuata wengine hawafuati its their choice, wanaozifuata wanazifuata bila kukwaza wengine kulinngana na nafasi zao. kuhusu MOU na nyie si mmeambiwa pelekeni mpewe hela mzitumie kwa mahakama ya kadhi lakini si kuwa na ajira special za makundi fulani yanayotaka kujinufaisha na kuwadhulumu wengine. kama kweli wakristu wanapewa hela hizo kwa kutengwa wengine hata mie sikubali, kwani ukristo ni upendo na kuheshimu watu wengine, na hiari pia, kama mtu anatak kuwa mkristo sawa kama hataki, matendo yangu yanatakiwa kumconvince kuwa mkristo na si force na negative seras. iambieni Serikali iwape kiwango sawa na wanachopewa hao wakristu, that is kama ni kweli, hata arears chukueni, na mzitumie hizo hizo kwa mahakama ya kadhi.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..

  ....
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe umejisalimisha kwa nani? kichuguu?
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuruhusiwa waanzishe mahakama inayojiendesha, maane yake kutakuwa na mambo yanayowahusu wao tu, sasa serikali kuenda kuingilia yasiyowahusu huko si ndio kujiingiza usipoitwa?
  Kama wataruhusiwa wapewe mahakama inayosimamiwa na serikali, kumbuka kuwa na dini namadhehebi mengine ya TZ nayo yataomba yafanyiwe. Seikali haina uwezo wa kutatua umeme, je tena kujibebesha gharama zisizokuwa za lazima?
   
 17. H

  Hute JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,042
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  huu ni upummbavu wa chuo kikuu cha morogoro. waislam wa aina hii akili zao ni za kipummmbavu sana....ndo maana mnadharaulika.
   
 18. Mzururaji

  Mzururaji JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,236
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Kiukweli sasa waislam mmchoka kweli kweli mahakama ya kadh kadh mkianza hayo na ss tuanaanza kudai vyetu hosptal shule na nk mbona mmepewa majengo na serikal wakristo wametulia ingekuwa ninyi mngepga makelele mwaka wote kwani kuna msaada mzur kama kukombolewa kielem haya makelele haya
   
 19. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  kwenye red haitatokea ndani ya nchi hii Tanzania labda uarabuni.Vatican ni nchi.Je OIC ni nini?Nchi imejiunga na vatican?
  kwenye blue unaleta vioja.ungefafanua.
   
 20. s

  sijambo Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ndio MPUMBAVU USIELEWA
   
Loading...