Waislamu tumekatazwa kuwaudhi wanawake, Abunuwasi na Vitimbi vya wanawake

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Ilikua jioni moja tulivu, mwanamke mmoja alielekea kisimani kuteka Maji..

Alipokuwa Huko Kisimani Mara Akatokea Mwanaume Mmoja Na Kumuuliza Yule Mwanamke "samahani Dada yangu Hivi Unaweza Kunitajia visa vya mwanamke?".

Yule mwanamke ghafla Akaanza Kulia Huku Anapiga Makelele Kwa Sauti Sana, HaLi Iliyofanya ndugu huyu akashikwa na hofu na Wanakijiji Wengi wakaanza kuja mbio Wakiwa Na Mapanga Na Marungu Kuelekea eneo hilo la Kisima!.

Mara Yule Mwanamke Akachukua Ndoo Ya Maji Na Kujimwagia Mwili mzima, Wanakijiji Walipofika Wakauliza Kwa hasira Kuna Nini Hapa??

Yule Mwanamke Akajibu "Nilikua Nimetumbukia Kisimani Na Huyu Baba Ndio Ameniokoa".

Wanakijiji Wakampa Hongera Yule Mwanaume kwa alichokifanya Kisha Wakasambaa!.

Yule Mwanamke Akamgeukia Yule Mwanaume Na Kumwambia "Hivyo Ndivyo visa Vya Mwanamke,

Ukimchukiza anaweza kukuua na ukimpenda anaweza Kukulinda"

maxresdefault.jpg
 
Mwanamke anatakiwa kuwa na Aibu katika jambo hilo, na hayo ndio maumbile yake. Mwanamke anayejileta kwako hutomchukulia thamani kama yule uliyempata kwa tochi na noti.
Mwanamke unayempata kwa noti ndio hutamuona wa thamani kwako. Si umemnunua utu wake! Mtumwa hana thamani kwa aliyemnunua.

Tongoza tu, habari za kuweka pesa wakati wa kutongoza zitakuharibia sheikh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom