STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,075
- 17,237
Ilikuwa jioni moja tulivu,mwanamke mmoja alielekea kisimani kuteka maji,, alipokuwa huko kisimani Mara akatokea mwanaume mmoja na kumuuliza yule mwanamke "samahani dadangu hivi unaweza kunitajia visa vya mwanamke?".
Yule mwanamke ghafla akaanza kulia huku anapiga makelele kwa sauti sana, hali iliyofanya wanakijiji wengi watoke mbio wakiwa na mapanga na marungu kuelekea huko kisimani!.
Mara yule mwanamke akachukua ndoo ya maji na kujimwagia mwili nzima, wanakijiji walipofika wakauliza kwa hasira kuna nini hapa?. Yule mwanamke akajibu"nilikua nimetumbukia kisimani na huyu baba ndio ameniokoa".
Wanakijiji wakampa hongera yule mwanaume kwa alichokifanya kisha wakasambaa. Yule mwanamke akamgeukia yule mwanaume na kumwambia "hivyo ndivyo visa vya mwanamke, ukimchukiza anaweza kukuua na ukimpenda anaweza kukulinda''.