1. Je, inafaa kula chakula ambacho nimeletewa na jirani yangu mkristo katika masiku ya kawaida?
Jawabu: Yafaa ndiyo, kula chakula cha watu wa kitabu {mkristo na myahudi} si jambo lililokatazwa katika UISLAMU, na juu ya hili kunapatikana dalili ya moja kwa moja
ALLAH (َسُبْحَانَهُ وَتَعَالَى) anasema:
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلُّ لَّهُمْ
English: “The food of the people of the book is permitted to you, and your food is permitted to them” (QURAN 5:5)
Swahili: “Na chakula cha waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao” (QURAN5:5)
Hivyo, muislamu anaruhusiwa kula chakula cha wakristo na wayahudi kwa sharti kuu moja la msingi: kiwe tu ni cha halali. Vyakula hivyo ni pamoja na wanyama waliowachinja mfano; ng’ombe, kondoo, kuku, mbuzi nakadhalika, na uhalali wa vichinjo vyao ni pale watakapolitaja jina la MUNGU wakati wa kitendo cha kunjinja, kuchinja kwao pasina kutaja jina la MUNGU au kwa kutaja jina jingine hufanya vichinjo vyao kuwa haramu na hivyo haitofaa kula. Hata muislamu akichinja pasina kutaja jina la MUNGU au kwa kutaja jina jingine hufanya kichinjo husika kuwa haramu na hivyo haitofaa kula.
Wakristo, Wayahudi na Waislamu pia wakikuletea chakula chochote ambacho ni haramu kwa mujibu wa misingi ya UISLAMU basi haitofaa kula chakula hicho, hivyohivyo haitafaa kula chakula haramu na halali vikiwa vimechanganywa kwani hukifanya chakula chote kuwa haramu.
2. Je, inafaa kula chakula ambacho nimeletewa na jirani yangu mkristo kilichopikwa maalumu kwa ajili ya kusherehekea sikukuu zao mfano; pasaka, krismasi na nyinginezo
Jawabu (a): Hapana, haifai kula chakula hicho kwa sababu kimeandaliwa/kimepikwa maalumu kwa ajili ya sikukuu zao. Unapokula chakula chao unawashaji’isha “unawaunga mkono” katika kitendo chao QURAN 5:2. Jawabu la SHAYKH FAWZAAN kwenye SHARH ‘UMDAT-IL-FIQH (29)
Jawabu (b): Haijuzu kwa muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na manaswara au mayahudi au makundi mengine katika kusherehekea wala kuadhimisha sikukuu zao kwa namna yoyote. Ni wajibu kuacha hilo kwa kuwa [MTUME ﷺ amesema]:
مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ, فَهُوَ مِنْهُمْ
English: “He who imitates any people (in their actions) is considered to be one of them.” (ABU DAWOOD 3401, GRADE: SAHIH)
Swahili: “Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao” (ABU DAWOOD 3401, DARAJA: SAHIHI)
MTUME ﷺ katukataza kushirikiana nao kwenye vitendo vyao vya kiibada ikiwemo sikukuu zao. Hivyo ni wajibu kwa muumini mwanamme na mwanamke kujiweka mbali na hilo na wala wasihudhurie katika sikukuu zao. Sikukuu zao zinakhalifu SHARI’AH YA ALLAAH na isitoshe wanampinga na kumpiga vita ALLAH.
Hivyo, haijuzu kushiriki humo wala kusaidizana nao wala kuwasaidia kwa lolote na chochote; si kwa kunywa hata chai, kahawa na kadhalika. Kushirikiana na wasiokuwa waislamu katika sikukuu zao ni aina ya kusaidiana katika dhambi na uadui.
ALLAH (سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى) anasema:
وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ
English: Cooperate “help one another” in righteousness and piety, but do not cooperate in sin and aggression (QURAN 5:2)
Swahili: “Saidianeni katika wema na uchaji MUNGU na wala msisaidiane katika dhambi na uadui/uovu” (QURAN 5:2)
Juu ya hili ni wajibu kuangalia mtu unalolifanya katika kufuata shar’ia za ALLAH na si kwa kuangalia watu wengine wafanyavyo, hakika watu wengi hawajali na SHARI´AH YA ALLAAH. ALLAH anasema katika kitabu chake kitukufu:
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ
English: If you obey the majority of those who live on earth, they will lead you away from ALLAH’s path (QURAN 6:116)
Swahili: “Ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na njia ya ALLAH.” (QURAN 6:116)
Wajibu ni kutekeleza SHARI´AH, haijuzu kuichukulia sahali - poa. Muislamu hufanya vitendo na kauli zake na za watu kwa mujibu wa QUR-AAN NA SUNNAH ZA MTUME WAKE (ﷺ). Ikiwa yataafikiana nayo (QUR-AAN NA SUNNAH) basi yatakubaliwa hata watu wakiyaacha. Na wakiyakhalifu au wakayachukia watu, yatarudishwa “hayatokubaliwa” hata watu wakiyafanya. Jawabu la IMAM IBN BAZ
(c) Shaykh AL UTHAYMEEN - amesema ni haram 'haifai', kuridhia vitendo vya kikafiri ni kufanya ukafiri
(d) Imam AL-ALBANI - amesema haifai
(e) Imam AL-MADKHALI - haifai
(f) Shaykh MUQBIL - haifai
(g) Imam IBN QAYYIM - amesema ni haram kwa itifaki ya maulamaa
Ziada muhimu: SUNAN ABI DĀWUD HADITHI NAMBA 1134, DARAJA LA HADITHI: SAHIHI
عَنْ أَنَسٍ قَالَ قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ وَلَهُمْ يَوْمَانِ يَلْعَبُونَ فِيهِمَا فَقَالَ مَا هَذَانِ الْيَوْمَانِ قَالُوا كُنَّا نَلْعَبُ فِيهِمَا فِي الْجَاهِلِيَّةِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَبْدَلَكُمْ بِهِمَا خَيْرًا مِنْهُمَا يَوْمَ الْأَضْحَى وَيَوْمَ الْفِطْرِ
English: ANAS IBN MALIK narrated: The MESSENGER OF ALLAH (ﷺ) arrived in MEDINA during two days in which they were celebrating. The PROPHET: arrived said, “What are these two days?”, They said, “We would celebrate these two days in the time of ignorance.” The PROPHET said, “Verily, ALLAH has replaced these two days with two better days: I’D AL FITR and I’D AL ADHA”
Swahili: ANAS IBN MALIK anasimulia kwamba MTUME MUHAMMAD (ﷺ) alipohamia MADINA, watu wa MADINA walikuwa na SIKUKUU zao ambazo walikuwa wanasherehekea katika zama za jahiliya – ujinga … … naye (ﷺ) akawaambia kuwa ALLAH (وَتَعَالَى سُبْحَانَهُ) amewabadilishia kwa siku ambazo ni bora zaidi, nazo ni: EID AL FITR na EID AL ADHA (SUNAN ABI DAWOOD 1134)
Hivyo, vilevile haifai kwa muislamu kusherehekea kwa kula wala kuadhimisha sikukuu ambazo hazina asili ‘basis’ katika dini ya UISLAMU - sikukuu zilizozushwa na baadhi ya waislamu wenyewe mfano; sikukuu ya uzao/mazazi ya MTUME “MAWLID”, sherehe za MI’IRAJ na sherehe za nusu ya mwezi SHA’ABAN – haya nayo yanaingia katika kusaidiana katika dhambi na uadui. Sikukuu halali za waislamu kwa mujibu wa SHAR’IYAH YA ALLAH ni mbili tu kama hadithi ilivyoeleza na si vingine.
AND, ALLAH KNOWS BEST