Waislamu mnijibu tafadhali

Waislamu mnijibu tafadhali

Ukweli mchungu

Haijuzu kwa muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na manaswara au mayahudi au makundi mengine katika sikukuu zao. Ni wajibu kuacha hilo kwa kuwa [Mtume amesema]:
“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao.”
. Ni juu ya muumini mwanamme na mwanamke kujiepusha na hilo wala wasihudhurie katika sikukuu zao kwa chochote

Huo ndio Ukweli mchungu
 
Waarabu kwa ubaguzi nimewavulia kofia.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mkristo na kama mjuavyo tutakuwa na sikukuu ya pasaka siku ya jumapili.
Sasa swali linaloniumiza kichwa ni hili, kuna rafiki yangu tunafanya kazi pamoja, pia ni majirani. Mimi nimeoa ila yeye yuko single na amefunga mwezi huu Ramadhan.
Je naweza kumwalika nyumbani kama kumfuturisha hiyo siku ya jumapili? Au naweza kumpelekea chakula hiyo siku jioni badala ya kuja home?
Au niksushe tu? Msaada wenu tafadhali.
Kuna uzi humu sikumbuki heading yake ila content ina ujumbe kuwa; muislam hatakiwi kula futari iliyoandaliwa na mke ambaye hajafunga nae ndoa, nadhani kwa mantiki hii unatakiwa usimpelekee kwakuwa haijaandaliwa na mkewe, ila mdau akauliza, je futari inayouzwa migahawani yote imeandaliwa na walioolewa kwa ndoa halali?

Hatimaye nimeupata👇
 
Hap

Hapo inategemeana na chakula chako umepika kwa ajili ya nini?kama ukimwambia hiki chakula ni kwa ajili ya pasaka,kama ni Muisilamu Kweli wa Imani na Elimu hawezi kula,sababu hapo imeshaingia shiriki,yaani umemuingiza Mwenyezi Mungu wake na sikuku ya kipagani.

Lakini kama utapika Simple tu,bila kukishirikisha na kitu chochote atakula,maana hamna tofauti na mtu anayepika chakula kwa ajili ya mizimu,hiyo pasaka siyo shere ya Mwenyezi Mungu
Ukweli mchungu

Haijuzu kwa muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na manaswara au mayahudi au makundi mengine katika sikukuu zao. Ni wajibu kuacha hilo kwa kuwa [Mtume amesema]:
“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao.”
. Ni juu ya muumini mwanamme na mwanamke kujiepusha na hilo wala wasihudhurie katika sikukuu zao kwa chochote

Huo ndio Ukweli mchungu
Je hatuoni kama tunabaguana wakati uislamu unahubiri amani na upendo ambayo ni maagizo ya Mungu?
 
Kuna uzi humu sikumbuki heading yake ila content ina ujumbe kuwa; muislam hatakiwi kula futari iliyoandaliwa na mke ambaye hajafunga nae ndoa, nadhani kwa mantiki hii unatakiwa usimpelekee kwakuwa haijaandaliwa na mkewe, ila mdau akauliza, je futari inayouzwa migahawani yote imeandaliwa na walioolewa kwa ndoa halali?
Ujamuekewa huyo aliecoment; kupikiwa futari na mwanamke usiemuoa hapa alikua na maana ya (Kimada).
Ambae kisheria huruhusiwi kukaa nae mpaka umuoe.
NB:
Kama huruhusiwi kukaa nae basi hata atakacho kupikia si ruhsa kukitumia wakati wa Ibada.
Kumbuka futari ni ibada ndani ya Funga.
 
Je hatuoni kama tunabaguana wakati uislamu unahubiri amani na upendo ambayo ni maagizo ya Mungu?
Tatizo sio kubaguani,ukinikalibisha katika siku za kawaida nitakuja kula,ugumu unaokuja kile chakula chá sikuku umeshakitolea kwa jili ya hiyo Miungu ya hizo sikuku
 
Tatizo sio kubaguani,ukinikalibisha katika siku za kawaida nitakuja kula,ugumu unaokuja kile chakula chá sikuku umeshakitolea kwa jili ya hiyo Miungu ya hizo sikuku
Nadhani tafsiri ya chakula cha wakristo ni kula na kufurahi pamoja, tofauti na ile ya Idd ya sadaka ya kuchinja

Pia naona kwa tafsiri uliyotoa hapo ni kama Mungu si mmoja, kola imani ina miungu wake na si Mungu mmoja kama ilivyo kwa Quoran na Biblia
 
Nadhani tafsiri ya chakula cha wakristo ni kula na kufurahi pamoja, tofauti na ile ya Idd ya sadaka ya kuchinja
Sikuku za Kiisilamu tumeamlishwa na Mwenyezi Mungu zipo toka enzi na enzi,mfano sikuku ya kuchinja tunamfuata babá yetu Ibrahimu
 
Sikuku za Kiisilamu tumeamlishwa na Mwenyezi Mungu zipo toka enzi na enzi,mfano sikuku ya kuchinja tunamfuata babá yetu Ibrahimu
Naam mafundisho hayo yapo kwa wakristo pia na Mungu wa Ibrahim ndiye Mungu wetu wote
 
Mimi ni mkristo na kama mjuavyo tutakuwa na sikukuu ya pasaka siku ya jumapili.
Sasa swali linaloniumiza kichwa ni hili, kuna rafiki yangu tunafanya kazi pamoja, pia ni majirani. Mimi nimeoa ila yeye yuko single na amefunga mwezi huu Ramadhan.
Je naweza kumwalika nyumbani kama kumfuturisha hiyo siku ya jumapili? Au naweza kumpelekea chakula hiyo siku jioni badala ya kuja home?
Au niksushe tu? Msaada wenu tafadhali.
Inategemea na akili ya huyo muislamu mwenyewe.

Ila kama ni mimi sioni tatizo kula chakula cha mkristo au akinifuturisha sioni tatizo kabisa.

Kwa sababu mtume alialikwa mbuzi na mtu asiyekuwa muislamu akaenda kula lakini haikuwa mwezi wa ramadhani.

Kitendo cha mtume kuitikia wito huo kinaonesha kwamba hilo ni jambo zuri hata kama halikufanyika ndani ya ramadhani.

Na jambo zuri linwlofaa nje ya ramadhani maana yake linafaa pia kufanyika ndani ya ramadhani..

Sasa mkuu sijui huyo rafiki yako yeye ana falsafa gani katika uislamu,msikilize yeye atalipokea vipi.
 
Tatizo linalokuja huyo mbuzi kachinjwa kwa ajili ya pasaka au xmass,maana sawa na kusema wewe Muisilamu ukale vyakula vya matambiko
 
Amesema Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
“Chakula kilichoandaliwa kwa ajili ya uzushi ni haraam kukila, kwa sababu hakikuandaliwa chakula hicho ila kwa ajili ya kuhuisha Bid-‘ah (jambo la uzushi). Kwa hiyo haifai kushirikiana nao, wala kula chakula chao kwenye siku hiyo, kwa sababu tendo la kushirikiana nao ama kula chakula chao, ni kuwapa nguvu kuwasaidia na kukiri juu ya jambo lao la uzushi wanalolifanya.”
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI

[Fataawaa Shaykh Swaalih Bin-Fawzaan Al-Fawzaan: Swawtiyaat Sabab Tahriym Twa’aam Al-Bid’ah Ka-Bid’ah Al-Mawlid An-Nabawiy]
 
Kama hutakua na chair fire waweza muita ukamfuturisha jamaa yako.
Kinachokatazwa kwenye dini ya haki ni chair fire na nyama ambayo mchinjaji sio mtu wa dini ya haki.
Haya mengine Kama pombe, kuhudhuria mikutano ya faragha gesti na kua na mchepuko yanazungumzika.
 
Toa ulichonacho, Mungu anakuona mpaka rohoni...
 
Ni msimamo wa waislamu walio wengi kuwa sikukuu za tofauti na dini zao kushiriki kwa namna yeyote ile ni dhambi
Waislam wajinga labda. Miaka ya nyuma huo ujinga haukuwepo. Wote kwa imani zetu tulishirikiana katika sikujui zetu. Huu Udini ni wa juzi juzi tu.
 
Mimi ni Muisilamu familia yangu ni wakristo,wanapokusanyika kwenye sherehe zao huwa siudhurii sababu sisi waisilamu tunasherehe zetu alizotupa Mwenyenzi Mungu,Iddy kubwa na Iddy ndogo

Wewe ni muislam wa hovyo tuu
IMG_0821.jpg
 
Tatizo linalokuja huyo mbuzi kachinjwa kwa ajili ya pasaka au xmass,
Mimi binafsi nakula hiko chakula kama ni cha halali kuliwa.

Sili kwa lengo la kusherehekea sikukuu hiyo bali nakula kwa lengo la kuitikia wema niliofanyiwa na ndugu huyo.

Wakristo wakiowana alafu wakasilimu basi hawaambiwi waowane tena kisa tu ndoa yao ilikuwa haikubaliki na uislamu hapana.

Ndoa yao itakubalika na hakuna haja ya ndoa mpya maadamu kitendo cha ndoa kwao kilifanyika hata kama kwa taratibu zao za kikristo.

Sasa kama uislamu unakubali ndoa za wakristo kwa taratibu zao inakuwaje leo uislamu ukatae chakula tu cha mkristo eti kisa kimepikwa siku ya sikukuu yao ?
 
Back
Top Bottom