Waislamu mnijibu tafadhali

Waislamu mnijibu tafadhali

Ni msimamo wa waislamu walio wengi kuwa sikukuu za tofauti na dini zao kushiriki kwa namna yeyote ile ni dhambi
Sio kweli . Hakuna muislam yeyote anayekatazwa kusherehekea kuzalia kwa Isa Bin Mariyam(Yesu). Na hiyo Pasaka kwenye uislam ina jina lake nadhani inaitwa Ashura kama sikukosea.
 
Mimi ni mkristo na kama mjuavyo tutakuwa na sikukuu ya pasaka siku ya jumapili.
Sasa swali linaloniumiza kichwa ni hili, kuna rafiki yangu tunafanya kazi pamoja, pia ni majirani. Mimi nimeoa ila yeye yuko single na amefunga mwezi huu Ramadhan.
Je naweza kumwalika nyumbani kama kumfuturisha hiyo siku ya jumapili? Au naweza kumpelekea chakula hiyo siku jioni badala ya kuja home?
Au nikaushe tu? Msaada wenu tafadhali.
KAUSHA.....ATAKIMWAGA HUYO

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
haifai na haikubaliki kidini kufanya hivyo maana yake ameshiriki kwenye sherehe hiyo ambayo haimo kwenye biblia hata quraan hata tourati
 
uislam haujakataza kula wala kushirikiana na watu wa imani zingine na hata wasio na imani katika mambo mbalimbali

jambo kubwa ni kuzingatia sheria na kanuni tu mf.kuna baadhi ya vyakula na vinywaji ni haramu bila ya kujalisha umempa au kanunua mwenyewe

wewe huna elimu kabisa ya dini ya kiislamu acha kupotosha. nenda kashabikie simba na yako
 
Mzee wangu sisi waislam tumefundishwa upendo kwa kila mtu so hatuwezi kushelekea ckukuu zenu za kiiman tu lakin kumpelekea muislam chakula hilo liko gud kabsa wala hakuna shida!! Mpeleke na atapokea na kukila pia lakin hawezi kuja kwenye sherehe kma hii ya pasaka cjui xmass

kasome dini wewe hata chakula hakifai kula
 
Mimi ni Muisilamu familia yangu ni wakristo,wanapokusanyika kwenye sherehe zao huwa siudhurii sababu sisi waisilamu tunasherehe zetu alizotupa Mwenyenzi Mungu,Iddy kubwa na Iddy ndogo

very good
 
Mimi ni Muisilamu familia yangu ni wakristo,wanapokusanyika kwenye sherehe zao huwa siudhurii sababu sisi waisilamu tunasherehe zetu alizotupa Mwenyenzi Mungu,Iddy kubwa na Iddy ndogo

mungu azidi kukupa uelewa upo vizuri
 
Mimi ni Muisilamu familia yangu ni wakristo,wanapokusanyika kwenye sherehe zao huwa siudhurii sababu sisi waisilamu tunasherehe zetu alizotupa Mwenyenzi Mungu,Iddy kubwa na Iddy ndogo
Kwaio unadharau ndugu zako kisa mafundisho yakigeni
 
Je hatuoni kama tunabaguana wakati uislamu unahubiri amani na upendo ambayo ni maagizo ya Mungu?

amani na upendo lakini sio kushiriki sherehe zenu na chakula labda bakwata hao sawa hawana dini
 
Inategemea na akili ya huyo muislamu mwenyewe.

Ila kama ni mimi sioni tatizo kula chakula cha mkristo au akinifuturisha sioni tatizo kabisa.

Kwa sababu mtume alialikwa mbuzi na mtu asiyekuwa muislamu akaenda kula lakini haikuwa mwezi wa ramadhani.

Kitendo cha mtume kuitikia wito huo kinaonesha kwamba hilo ni jambo zuri hata kama halikufanyika ndani ya ramadhani.

Na jambo zuri linwlofaa nje ya ramadhani maana yake linafaa pia kufanyika ndani ya ramadhani..

Sasa mkuu sijui huyo rafiki yako yeye ana falsafa gani katika uislamu,msikilize yeye atalipokea vipi.

wewe nae mbumbumbu wa elimu mtume alikaribishwa mbuzi ilikuwa sherehe ya pasaka au xrismas ? jibu hapa alikaribishwa mbuzi kawaida ilikuwa sio sherehe hapo inakuja chakula cha sherehe yao ndio hairuhusiwi elewe wewe muislamu dhaifu
 
Waislam wajinga labda. Miaka ya nyuma huo ujinga haukuwepo. Wote kwa imani zetu tulishirikiana katika sikujui zetu. Huu Udini ni wa juzi juzi tu.

mjinga nani ni yule anaemuamini mtu kuwa mungu? na huyu mungu ndie alieteswa akashindwa kujikomboa hana nguvu mkafanya sherehe yake ya pasaka hata kwenye maadishi ya biblia hakuna hiyo sherehe sasa nani mjinga?
 
Hii fatwa ya sheikh fawzaan ina walaakinj mkubwa sana kwangu inanipa shida sana na hii fatwa..

Kwa sababu zifuatazo..

Uharamu wa kitu haufanyi vitu vya halali kuwa haramu mfano uharamu wa disco BAA haufanyi chipsi zinazouzwa pale ziwe haramu.

Mimi nikienda baa kununua chipsi au muuza baa akaniletea chipsi sitakiwi kula eti kwa kuwa nikila ninazidi kuipa nguvu ile baa izidi kukuwa ?

Uharamu wa bidaa haufanyi chakula kinachopikwa katika bidaa hhiyo kiwe haramu hata siku moja.

Wanaopika wali kwenye bidaa huo wali haujapikwa kwa ajili ya kuhuisha kwa sababu bidaa ipo hata kabla ya chakula.

Kuna bidaa zinafanyika kama vile adhkari za sauti baada ya sala na wala hakuna chakula pale lakini kila siku zinakuwa nyingi.

Kuna bidaa ya kunuti alfajiri katika sala wala hakuna chakula na bidaa hiyo ipo inahuishwa siku zote.

Kwa hiyo sio kweli kwamba hiko chakula kinapikwa kwa ajili ya kuhuisha bidaa.

Hata hivyo mtume anasema "matendo kuhukumiwa kwa nia..."

Kama mtu anakula chakula hicho sio kwa lengo la kuhuisha tatizo lake liko wapi ?
Mimi maadamu umeniletea nnakula

lakini pia kama wao lengo lao ni kuhuisha bidaa mimi nikila huku siikubali bidaa hiyo je lengo lao la kuhuisha bidaa linakuwa limefanikiwa kivipi ?

Hapa shekhe anaposema kwamba "NI KUKIRI" ina maana anawajibia wale wanaokula chakula.

Wakati huo ilitakiwa wao wenyewe ndio wajibu na sio shekhe fauzani.

Mimi leo ukiniletea chakula nitakula kwa sababu umeniletea na wala sitakula kwa kutia nia kwamba nakiri krismasi niko pamoja nayo.

Kama nia yangu sio kukiri vipi shekhe aseme k2amba ukila tu inakuwa automatiki umekiri ?

Katoa wapi uswlubu huu allaamah al fawzaan ?

uharamu unakuja pale unaponunua chips bar maana yake unawaongezea faida wazidi kununua vilevi na kuendelea kupiga disco wewe unashiriki katika kuongeza nguvu mfano wachagga akiwa na duka atauza unga wa sembe sabuni kila aina ya matumizi ya nyumbani hawaachi kuchanganya kwenye maduka yao na pombe kali na bia. sasa wewe muislamu ukienda duka hilo kununua sabuni ya kuogea na hali unaona duka kachanganya na pombe haifai kununua sabuni hapo maana unazidi wewe kumpa nguvu ya kuongeza pombe
 
Kwaio unadharau ndugu zako kisa mafundisho yakigeni

hakuna mafundisho ya kigeni haya ni mafundisho ya mungu. mbona wewe unavaa suruali jeans na shati si wageni ndio wameleta mavazi hayo . kwanini usitembee uchi au akavaa ngozi za mbuzi kama walivyokuwa wanavaa babu zenu
 
uharamu unakuja pale unaponunua chips bar maana yake unawaongezea faida wazidi kununua vilevi na kuendelea kupiga disco wewe unashiriki katika kuongeza nguvu mfano wachagga akiwa na duka atauza unga wa sembe sabuni kila aina ya matumizi ya nyumbani hawaachi kuchanganya kwenye maduka yao na pombe kali na bia. sasa wewe muislamu ukienda duka hilo kununua sabuni ya kuogea na hali unaona duka kachanganya na pombe haifai kununua sabuni hapo maana unazidi wewe kumpa nguvu ya kuongeza pombe
Unayo dalili ya kukataza kununua kitu cha halali kwa watu wanaofanya haramu ?

Dalili maana yake ni Qurani na hadithi zilizo sahihi,sio maneno matupu ya mtu
 
Sio kweli . Hakuna muislam yeyote anayekatazwa kusherehekea kuzalia kwa Isa Bin Mariyam(Yesu). Na hiyo Pasaka kwenye uislam ina jina lake nadhani inaitwa Ashura kama sikukosea.
Yesu na isa Bin Mariyam ni watu wawili tofauti, kwa hiyo usilazimishe kutafuta uhalali
 
Back
Top Bottom