Waislam wa Pakistan wachoma moto Makanisa na nyumba za wakirsto Tarehe 15 Agosti, 2023

Status
Not open for further replies.

joex

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
786
639


Fikiria Taifa la Pakistan ambapo Jamii ya Waislam ndyo wengi takribani 98% wakati Wakristo ni asilimia 1.5% tu, halafu bado Jamii hiyo ya Waislam walio wengi hawaonyeshi huruma hata kidogo kwa wenzao ambao wingi wao ni kama tone la maji kwenye ndoo ya lita 20.

Kwa taarifa tu ni kwamba nchi ya Pakistan ni moja kati ya nchi chache Duniani ambazo Katiba yake inaitambua kama Jamhuri ya Kiislam ya Pakistan.

Serikali ilipitisha Sheria ya Blasphemy Law (Sheria ya Kukataza kukufuru Mtume, Quran, Allah). Waislam wa Pakistan kwa kisingizio cha Sheria hii, hujichukulia Sheria mkononi hata kama hakuna ushahidi (na visa vingi vimeonyesha kutokuwepo ushahidi) kufanya VURUGU kwa Wakiristo na mali zao.

Hata kama tuseme Mkiristo wa Pakistani kweli amefanya Blasphemy, Hekima ya kawaida ya mwanadamu anayemuogopa Mungu wa Kweli atakabidhi kwa vyombo vya dola kuchukua mkondo wa kisheria; LAKINI siyo hivyo kwa hawa wenzetu.

Mfano katika matukio haya ya kuchoma moto Makanisa, Biblia zilizomo kanisani na majumba ya wakiristo, Waislam wanadai ati kuna Mkristo ALICHANA KARATASI ZA QURANI. Taarifa zinasema Mpaka matukio ya uchomaji makanisa unatokea, hakukuwa na ushahidi.

Swali ni Je kama kweli hao Waislam wanamuabudu Mungu wa kweli, huyo Mungu ataruhusu wampiganie yeye kwa kwenda kufanya vitendo vya KUFURU vya kuchoma Makanisa na Biblia ambazo Binadamu wenzao wanavithamini kama vitakatifu?

Hapa chini nimeweka video clips kwa ushahidi. Video moja ni ya Shirika la Utangazaji la Asia na video ya pili ni ya Aljazeera

 

Attachments

  • videoplayback (2).mp4
    21.2 MB
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom