USSR,
Mkuu tahariri yako yaonyesha unawatakia mema sana waislam. Hongera, basi tuishauri serikali ya ciciem, au chama chcht kinachotaka maendeleo ya watanzania wakiwemo waislam.
1. Kuondoa sheria kandamizi zinazowazuia waislam kuendeshea miradi yao ya maendeleo. Na sheria moja wapo ni ya ugaidi. Sheria hii imekuwa kikwazo kwa taasisi nyingi za kiislam kukosa misaada. Kwa kile kinachosemwa pesa hizo zitawafanya waislam wawe magaidi.
Mfano wa taasisi hizo ni al haramin tanga, na dhynurain iringa. Taasisi hizi zimetenzwa nguvu kutokana na jitihada zao za elimu na afya. Mfano dhynuran kila walipojenga msikiti waliweka kituo cha afya. Huko tanga taasisi ya al haramain ilijikita kutoa elimu bure, hii ndio hali ya taasisi nyingi za kiislam kuminywa na kutopewa ruhusa ya kupata misaada ya maendeleo.
Pia kuna hali ya viongizi wa bakwata kulazimishwa waombe kujengewa msikiti badala ya mahitaji mengine. Haya tunayaona wanapokuja viongozi kutokana nchi za kiislam duniani.
2. Serikali itoe ajira kwa alimu wa dini na yatambulike kwa ajili ya maadili mema mbadala ya kununua magari ya gharama kubwa kwa ajili ya wanasiasa
3. Serikali iajiri wahudumu wa afya na madakatri kwa hospitali zinazoendeshwa na taasisi za dini badala ya kununua ndege ambazo zinaendeshwa kwa hasara na 99% ya wanyonge hawafaidiki nazo.
4. Waislam wenyewe wajivue ktk ufinyu wa fikra kuwa mambo yanayohusu dini ni Yale yanayojulikana ni ya kiroho tu. Huu ni ufinyu wa fikra. Na ni Ushindi ambao wameupata wapinzani wa Uislam. . Wapinzani wa Vitabu Vitukufu vilivyotangulia walifaulu kufanya hila ya kuvitia mikono na kuviharibu Vitabu hivyo.
Lakini Wapinzani wa Quran wameshindwa katika jitihada zao za kuipotosha Quran. Hata hivyo, wamepata ushindi wa kuifungia Quran ndani ya wigo wa kitawa ambamo kila msomaji wa Quran ameondoka katika lengo lake la mwongozo wa maisha ya kila siku huku akiridhika kuwa anasoma Quran kwa wingi ktk kujenga misikiti kwa ajili ya kuswalia, kufunga nk
Laiti waislam ungefungamana na lengo lilelile lililoifikisha na Mtume (saw) na Maswahaba katika kilele cha mafanikio ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kitabia, kidiplomasia, basi uilsma ungeonekana kuwa ni mfumo kimbilio la wanadamu.
Leo waislam tumeyaacha mafundisho usahihi kuwa uislam unafungamana na matendo yote kwa ajili ya manufaa ya miwili yetu na matendo kwa ajili ya manufaa ya roho zetu. Na hivyo turudi kwenye uislam kamili kwa kujenga na kusimamia vyote,, msikiti, Madrasa, shule, hospitali, nk