Waingereza wamnanga Rais Kikwete!

Niliwahi kumwambia mwandishi mmoja wa Dar kuwa,africa ina laana,akakataa,udhaifu wa kikwete kushindwa kuongoza nchi ni moja ya sababu za laana ya africa kutimia,nchi gani ktk africa ambayo ina uchumi mzuri angalau tu kuifananisha na spain? au Turkey? africa yenye raslimali nyingi kuliko mabara yote duniani ndo pia maskini kuliko bara lolote duniani,hapo ukitafakari unaona nini? kwa nini nchi kama Finland isiyo na raslimali yoyote isaidie mataifa kibao africa? Zamani nikiwa na miaka 18 hadi 22,nilikuwa na ndoto za kuishi ulaya au marekani,leo hii ktk umri wa miaka 30,sitamani kwenda popote,moyo wa uzalendo umenikaa,ni nani atasimama kunipinga kuwa africa haina laana? kwa nini mataifa 54 yote ya africa yawe choka mbaya? south africa ilikuwa nzuri kiuchumi wakati wa utawala wa makaburu,leo hii choka mbaya,black skin,black brain,black future,MUNGU TUSAMEHE DHAMBI YOYOTE MBAYA TULIYOKUTENDA SISI WAAFRIKA.Central africa,mali,Rwanda,congo,Angola,misri,Libya,Liberia,Sierra Leone,sudan,are these blessed? Let me know.

Mheshimiwa Truth Guy, una ushahidi gani zaidi ya huo uliouandika hapo kuwa waafrika wana laana? Wa kwanza mie najitoa kwenye hiyo laana kama laana unayo mwenyewe tukirejea miaka mingi nyuma mkoloni wakati alipotutawala alihakikisha kutuwekea imani ya kuwa sisi ni mkia tu kwao na ndyo akili hiyo uliyonayo wewe na viongozi wako ndyo mataifa mengi ya afrika tupo hapa wanaamini bila kusaidiwa na mzungu hakuna maendeleo na yeye mzungu huku akiwa anatung'ong'a anatupa milion 100 kisha anachukua billion 100 mfano.

Hivyo mheshimiwa hiyo "colonial mentality" ondoa kabisa usijidharau kabisa haya mazungu yana tuchezea michezo michafu tukipata serikali isiyo sujudia watu wa magharibi utafurahi ndugu yangu

Angalia kwa bwana Gaddafi kwani wale ni weusi? Hapo utakuwa unapata picha kidogo kwa kile nnacho amini kabla ya ukoloni wazungu waliendelea sana kuliko sisi kutokana na mazingira yao na sisi tulikuwa na maendeleo kidogo kutokana na mazingira tuishiyo.. Angalia kama ugunduzi wa kalenda ulianzia wapi? Na vingine vingi ambavyo mimi sivijui inawezekana hata wewe huvijui na vimefichwa na kuonekana wamevigundua wao. Hivyo tusipotoshane hapa eti waafrika tuna laana.
 
Waafrika tuone hivi hivi, tunajuwa sana kuongea, kupanga na kupangua lakini hatujuwi kutekeleza. Leo mchukuwe Mtanzania yeyote umuulize kuhusu ligi ya mpira wa Uingereza, basi utamkuta anaijuwa hiyo ligi na namna timu inatakiwa iwe kuliko Mourinho. Hiyo si kwenye mpira tu, ni kila pahali, tunajuwa kila kitu kwa midomo yetu lakini kutenda? Ng'oo.

Nchi hii muumba dunia na ardhi alitujaaalia kila kitu chema, maji mengi, madini mengi, ardhi nzuri inayo-limika miezi 12 kwa mwaka, misitu mizuri, mbuga nzuri, milima mizuri, mabonde mazuri, watu wazuri, wanyama wazuri. Kwa ufupi katupa pepo ya duniani, lakini kitu kimoja hatukupewa, nacho ni AKILI. AKILI HATUNA.

Binaadam hakosi kasoro na kasoro yetu ni AKILI.

Rejea maandishi yenye herufi kubwa.
Wangapi mnakubaliana na hiyo kauli? Mimi wa kwanza sikubaliani nayo, na kama una amini toka moyoni huna akili ushawahi waambia familia yako? Amka dada hivyo ndivyo wazungu wanataka uwe ili waendelee kuzinyonya rasilimali zetu

Kwenye suala la uongeaji tunajua "debe tupu..... kupangilia na kushindwa na kushindwa kutekeleza kunachangiwa na mambo mengi huenda hakuna vifaa vya kutosha, pesa, ushirikiano na menejimenti kuna mengi saaana ila si AKILI.
 
Rejea maandishi yenye herufi kubwa.
Wangapi mnakubaliana na hiyo kauli? Mimi wa kwanza sikubaliani nayo, na kama una amini toka moyoni huna akili ushawahi waambia familia yako? Amka dada hivyo ndivyo wazungu wanataka uwe ili waendelee kuzinyonya rasilimali zetu

Kwenye suala la uongeaji tunajua "debe tupu..... kupangilia na kushindwa na kushindwa kutekeleza kunachangiwa na mambo mengi huenda hakuna vifaa vya kutosha, pesa, ushirikiano na menejimenti kuna mengi saaana ila si AKILI.

Tuoneshe akili zako umeshazifanyia nini? kama unazo.
 
sio wote walozaliwa Africa wana laana isipokuwa wachache ndo wenye laana mfano tuliowapa nafas ya kutuongoza kama jumuiya...wana laana za maisha mana wanaona maendeleo yao ndio ya msng wanasahau klichowaweka kwenye mfumo, wanasain makubaliano kwa kutolewa night katka hotel za bei ndogo majuu....hv nan alkwambia mzungu n mdogo wake mungu ,utalpa kwa kila.utakachopewa kama waitavyo walaj "msaada"
 
Mimi nafikiri tufike sehemu tukubali waafrika tuna matatizo, hatuna akili Kama za wazungu wengi mtanipinga ila ndio ukweli, lakini pia ktk akili kidogo tulizopewa tunaweza kutumia rasilimali zetu vizuri na zikatufanya Tuishi vizuri, unapokuwa na viongozi wapo tayari kuchukua 10% na kuwapa wazungu natural resources zetu za mabilioni ya dola na kuacha watu wake wakiishi kwa dhiki!! Sidhani kiongozi anahitaji rocket science kuliona hili, halafu anachukua pesa hizo hizo za kifisadi anakwenda kuweka kwenye Swiss bank, kesho na kesho kutwa anapata kisukari na shinikizo la damu anakufa na pesa hazirudi ng'ooo! Hizi ndizo akili za viongozi wetu, angalia Venezuela wanavyotumia mafuta kujenga nchi Yao na kuwapa watu wao maisha mazuri! Kwasababu walikuwa na kiongozi thabiti comrade Hugo Chavez unakuta taifa Kama marekani na nguvu zake wanashindwa kupenya kwenye serikali ya Venezuela, Hugo Chavez hakuwa mtu mwenye elimu kubwa hata alipokufa raisi wa sasa sio msomi alikuwa truck driver tu!! Lakini uzalendo wao ni uliotukuka, viongozi hujengwa na taifa, siku tukaposema tumechoka tunataka nchi iendeshwe na viongozi wazalendo ndio tutakuwa tumefanya mapinduzi ya kweli, tatizo ni sisi wananchi wenyewe hatujaamua, tumeamua kujenga taifa la omba omba, unakuta hatari nchi za kiaarabu ni hivyo hivyo wanajenga nchi zao kwa kutumia rasilimali zao, Ni kiongozi gani Tanzania anaweza kusema hapana kwa mataifa ya magharibi na akaweza kuhimili vitisho vyao? Akawa na vision ya kulitoa taifa hapa lilipo? Ikiwa raisi anayetuongoza amekiri hajui kwann nchi ni maskini! Lengo la kuwania uraisi ilikuwa nn? Nenda Nigeria pamoja na mafuta Yao lakini hakuna kitu, watawala ni mafisadi wanaweka pesa uswisi, waafrika tuna matatizo.
 
jk aliwakatalia ombi lao la kuwekeza kwenye urenium na kuleta balozi shoga llazima wamtukane kulipa kisasi

Hana jeuri ya Kuwakatalia..
JK ni Kama Bendera,pasipo upepo hiwezi kupepea..
Ben alikua Kidume hasa na hata kauli zake kuhusu watoa misaada tulizisikia..
Sasa Huyo umteteaye alitamka lini kuwapinga Live hao Anaowapigia magoti kila uchwao!?
Shame on u na JK wako,mnaishusha hadhi TZ!!
 
hawa walitaka kutucameron watanzania wote
hawana maana hata kuwasikiliza kuna agenda ndani ya kauli yao kwa jk

Wale waleeee, nadhani wewe ni mmoja kati ya wale wanaofaidika na hizo trip za muheshimiwa, kwa akili timamu huwezi tetea kitu katika hizo comments zilizotolewa. kila la kheri
 
Tatizo letu kubwa la Waafrica ni ubinafsi. tunaangalia matumbo yetu badala ya taifa letu. Mimi siwalaumu wazungu katika umasikini wetu wachawi ni sisi. Kwani EpA walikuja iba wazungu ? Kagoda, hao watumishi wezi wa halmashauri ni wazungu ?
 
wazungu ni wehu wao wanavyokuja wakabeba madini yetu na kutuachia mashimo walitegemea mafanikio na maendeleo tutayatoa wapi?

Wazungu wengi ni wakweli kwa nafsi zao.Wanapokuja kutafuta nafasi za kutengeneza fedha usitegemee huruma kutoka kwao.Wanajiapiza kutumia kila nafasi waipatayo kupata faida, ikiwa ni pamoja na udhaifu wa wanaojiita wasomi wetu.Usiwaite wao wehu kuiona kasoro yetu,tafakari ni nani kati yetu na wao anastahili kuitwa mwehu?
 
Kwa sisi wa simu za kichina hatuoni kitu hapa kwa yule anayeeza kucopy na kuueeka hapa plse
 
Wale waleeee, nadhani wewe ni mmoja kati ya wale wanaofaidika na hizo trip za muheshimiwa, kwa akili timamu huwezi tetea kitu katika hizo comments zilizotolewa. kila la kheri

Unafikiri anafaidika basi!... Hana AKILI tu, kila kitu kwake ni mizaha tu.
 
Ikiwezekana ifanyike hadharani, iwe fundisho.. Huwa najiuliza wakiziona comment zetu kama hizi huwa wanatufikiriaje au ndyo yale ya kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji
nafikiri huwa wanabinua midomo juu wakiamini hilo haluwezi tokea.
 
Ndiyo maana nasema siku zote, anayependa CCM na viongozi wake basi na achunguzwe akili kwani mtu mwenye akili timamu hawezi kamwe kuibeza CCM. Hawa viongozi ni majambza tu sema tu wamehalalishwa kwa sababu ni wao ndio wanaotawala nchi ila kwa makusudi wanaiba na kufirisi nchi kwa kisingizo cha kusema kwamba nchi yetu masikini. Misaada inakuja wanakula wao na familia zao. Rais mwenye akili timamu hawezi hata siku moja akasema haya ayasemayo Kikwete kwani kule ni kushindwa kazi. Tanzania with CCM kwa kweli tuache kudanganyana hatutafika popote bali kurudishwa nyuma huku wenzetu wanapiga hatua.
 
Acheni kuwa na akili fupi...huo ni uzandiki unaopandikizwa na waingereza kwenye fikra zenu, comment kama hizo huwekwa kwa malengo maalumu...mtaendelea kummuendekeza mzungu hadi lini...mnafikiri waingereza ni marafiki zetu kwa kiasi gani, yote ya kutuburuza na kutukandamiza hamu yaoni.

Rais wetu anamapungufu yake mengi lakini ni juu yetu kuyarekebisha kwa kubadilisha mfumo ila si kwa kumfurahisha Mkoloni.
 
Tatizo letu kubwa la
Waafrica ni ubinafsi. tunaangalia matumbo yetu badala ya taifa letu.
Mimi siwalaumu wazungu katika umasikini wetu wachawi ni sisi. Kwani EpA
walikuja iba wazungu ? Kagoda, hao watumishi wezi wa halmashauri ni
wazungu ?

NITONYE usiwe kama zzk,HAKUWATONYA MAFISADI WA CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTAL (CDM),ikala kwake.
 
Back
Top Bottom