tunapendana sana na waifu,tumetoka mbali na tumefanikiwa kupata watoto wawili.lakini waifu ananikaba sana,hataki kabisa niwe natoka,hata function za kazini huwa hataki niende.function za funga mwaka etc za kazini hataki kabisa niende,nikilazimisha utamkuta ananuna huyo hata kwa siku tatu na kubaki kulia tu,anadai eti kama nampenda nitamuachaje peke yake ndani.mbaya zaidi mi napenda sana mpira,basi hata kwenda kuangalia mechi ni tatizo.atakwambia huu ni muda wa kupumzika na kuwa karibu yake,nitaendaje kwenye mpira?mpira uwe mchana au usiku ananibana.kazini unaweza kupokea simu zake 3 ndani ya dk 20.wakati mwingine huwa nakaushia afu baadae namwambia nilikuwa bize.
wanamme wenzangu hebu niambieni,hivi hii ni hali ya kawaida kwenye ndoa au yangu imekuwa too much?
cc:akina dada wote mlioolewa na wale mnaotegemea kuolewa.