Mpaka sasa, kama alivyosema Polepole, wahuni wamefanikiwa kuteka kila kitu:
1. Wahuni wameteka dola, ndiyo maana tunaona hakuna chombo chochote cha ulinzi na usalama kikishughulika na kuwakamata wanaoteka na kuua wananchi. Badala yake, dola inafanya kila namna kuwalinda watekaji, wauaji na washambuliaji wa watu wanaokosoa uovu wa watawala. Polisi hawashughuliki kuwakamata watekaji bali wanawakamata wanaosema utekaji na mauaji ni vitendo viovu vya udhulumaji haki.
2.Wahuni wameiteka mahakama kwa kiwango ambacho leo hii inaonekana ni aheri tusingekuwa hata na mahakama. Uwepo wa mahakama umekuwa ni hasara badala ya kuwa faida! Leo hii ni aheri uende kwa mzee wa baraza la usuluhishi wa darasa la saba, unaweza kuipata haki yako kuliko kwenda mahakama kuu ukakutane na majaji mchongo ambao wapo kwaajili ya kulinda na kutetea uovu. Kama tungekuwa na mahakama za kweli, kwa uhakika wa 100%, Lisu kamwe asingekuwa jela wala asingekuwa na kesi. Lakini kwa bahati mbaya waovu wametumbukizwa mpaka mahakamani kwa lengo la kwenda kusimamia udhulumaji haki.
3. Wahuni wameteka jeshi la polisi. Ukitaka kuthibitisha hilo, kemea hadharani utekaji na mauaji, ukemee uporaji wa rasilimali za Taifa, ukemee sheria mbovu za uchaguzi. Haichukui mudà utakuwa umetekwa, ukiwa na bahati utakuwa kwenye vituo vya polisi kusubiria kubambikiwa kesi.
Wahuni wameteka Bunge, ndiyo maana unaona Bunge mpaka lilizuiwa kabisa kujadili wanaotekwa.
Wahuni wamefanikiwa kuwateka baadhi ya viongozi wa dini. Viongozi hao wa dini huwezi hata siku moja ukawasikia wakiongea dhidi ya uovu wa kuteka na kuwaua watu wanaokosoa.