Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,516
- 46,376
Serikali ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe imepokea baiskeli 279 kutoka kwa mdau wa maendeleo wa kampuni ya Buffalo Bicycles Tanzania kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya ngazi ya jamii.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi baiskeli hizo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje, Abdallah Mayomba, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya Farida Mgomi amewataka ‘Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW)’ kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia maslahi ya Taifa.
Mayomba amesema baiskeli hizo zitawasaidia wahudumu kuwafikia wananchi kwa wepesi zaidi na kutoa elimu na huduma za afya ikiwemo kuhamasisha wananchi kujenga na kutumia vyoo bora ili kuimarisha usafi na kuzuia magonjwa ya mlipuko kwa wakati.
Nao wawakilishi wa Buffalo Bicycles Tanzania wamesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya afya na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia jamii yenye afya bora.
Hatua hii ni sehemu ya ushirikiano unaoendelea kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kuimarisha sekta ya afya na kuboresha ustawi wa wananchi wa wilaya ya Ileje.