Wahubiri kama vitu hamvijui bora kukaa kimya

Wahubiri kama vitu hamvijui bora kukaa kimya

chief72

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
627
Reaction score
309
Nimeshangaa kuona mhubiri mmoja akiwaambia waumini eti wakristo wakifa wanaenda mbinguni na sio peponi maana peponi ni sehemu ya mapepo na ni sehemu mbaya kabisa,na akaendelea kutoa discription chungu mzima kwa ubaya wa peponi, lakini inaonyesha hajasoma vizur bible, pale Yesu alipokuwa msalabani akiwa kahukumiwa na wale wanyang'anyi kwa injili ya LUKA 23:42-43 kisha akasema , Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia ufalme wako,Yesu akamwambia amini,nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.

Na si tu huyu mhubiri bali nimeona comment nyingi humu zikizungumzia peponi kwa style hii, jamani tusome, ujanja ujanja haufai.
 
".....Siku za mwisho watatokea makristo wa uongo nao watadanganya wengi...."

Source Jesus Christ.
 
pepo/mapepo/majini/jini/majinini/.mhubiri yupo sahihi huwez kuwa mcha mungu then uonde kwenye mapepo aka peponi
 
Tatizo wewe ukiona mtu ameshika BIBLIA pale posta au kituo cha daladala Temeke mwisho na amevaa tai na shati chafu huku ananukuu vitabu vya MUNGU wewe unamuita muhubiri. Wahubiri utawakuta. ndani ya makanisa ya Anglikan. katoliki na Lutheran huko kwingine ni kwako
 
Wahubiri wa kweli utawakuta Katoliki, Anglikan, lutherani? Hivi dini ya kweli unaijua kweli wewe? kwa mujibu wa Biblia takatifu.
 
Biblia haikuandikwa kwa kiswahili wakati Yesu alipoongea hayo..aliongea kiaramaik..waliotafsiri biblia kwenda kirumi na baadae kiswahili ndio walioweka maneno yaliyorahisi kueleweka kwa jamii wanayoitafsiria. Yesu alitoka na kurudi mbinguni na sio peponi.
 
Wahubiri wa kweli utawakuta Katoliki, Anglikan, lutherani? Hivi dini ya kweli unaijua kweli wewe? kwa mujibu wa Biblia takatifu.

Dini ya kweli siijui lakini hakika wale wanaohubiri kwenye vituo vya daladala si watu wa dini.
 
Mhubiri mmoja ndio nani? Acha kuleta hisia zako bana
 
nimeshangaa kuona mhubiri mmoja akiwaambia waumini eti wakristo wakifa wanaenda mbinguni na sio peponi maana peponi ni sehemu ya mapepo na ni sehem mbaya kabisa,na akaendelea kutoa discription chungu mzima kwa ubaya wa peponi, lakini inaonyesha hajasoma vizur bible, pale Yesu alipokuwa msalabani akiwa kahukumiwa na wale wanyang'anyi kwa injili ya....... LUKA 23:42-43 kisha akasema , Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia ufalme wako,Yesu akamwambia amin,nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.na si tu huyu mhubiri bali nimeona comment nyingi humu zikizungumzia peponi kwa style hii, jamani tusome, ujanja ujanja haufai

Ni kweli Mkristo akifa haendi peponi, hata Yesu hakusema peponi bali ni utafsiri mbaya kwa makusudi au kwa kutojua. Biblia ya kwanza kutafsiriwa hapa nchini iliwahusisha hata Wazanzibar ambao ni waislamu , kwa hiyo waliweza kupachika maneno yao ndiyo maana utakutana na maneno kama Sheikh, Kadhi, peponi nk.
 
Nimeshangaa kuona mhubiri mmoja akiwaambia waumini eti wakristo wakifa wanaenda mbinguni na sio peponi maana peponi ni sehemu ya mapepo na ni sehemu mbaya kabisa,na akaendelea kutoa discription chungu mzima kwa ubaya wa peponi, lakini inaonyesha hajasoma vizur bible, pale Yesu alipokuwa msalabani akiwa kahukumiwa na wale wanyang'anyi kwa injili ya LUKA 23:42-43 kisha akasema , Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia ufalme wako,Yesu akamwambia amini,nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.

Na si tu huyu mhubiri bali nimeona comment nyingi humu zikizungumzia peponi kwa style hii, jamani tusome, ujanja ujanja haufai.

ukiangalia kwenye biblia ya kiingereza hilo neno uliloita peponi wao wameita ni PARADISE.sasa hebu tuambiane hapa hapa nini tafsiri halisi ya paradise kwa kiswahili?
 
Nimeshangaa kuona mhubiri mmoja akiwaambia waumini eti wakristo wakifa wanaenda mbinguni na sio peponi maana peponi ni sehemu ya mapepo na ni sehemu mbaya kabisa.

Weka chanzo cha habari yako, mhubiri mmoja ndio nani huyo?
 
ukiangalia kwenye biblia ya kiingereza hilo neno uliloita peponi wao wameita ni PARADISE.sasa hebu tuambiane hapa hapa nini tafsiri halisi ya paradise kwa kiswahili?
Paradiso au kuna tafsiri nyingine?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom