Waheshimiwa wabunge wetu kuweni serious | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waheshimiwa wabunge wetu kuweni serious

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 19, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wakuu bajeti inapowasilishwabungeni huwa ni kama hitimisho lamchakato mrefu na wa kisayansi ambao umehusisha wadau wengi sana na zaidiwaheshimiwa wabunge wenyewe. Kamati za kudumu za bunge hupitia bajeti za wizarahusika . Katika vikao baina ya kamati ya kudumu ya bunge na watendajiwaandamizi wa wizara husika wakiongozwa na waziri wao. Waziri huwasilisha rasmuya bajeti ya wizara yake, wabunge huuliza maswali na kutaka ufafanuzi katikamambo ambayo wanadhani hayaeleweki vizuri kwao. Lakini pia wabunge hutoamapendekezo kadhaa ambayo yanaingizwa moja kwa moja katika bajeti.Kamati ya kudumu ya bunge yafedha na uchumi ina jukumu la kuipitia bajeti kuu ya serikali katika kikao chapamoja baina ya watendaji waandamizi wa wizara ya fedha na wajumbe wa kamati yafedha ya bunge. Kwa msingi huo bajeti inayoendelea kujadiliwa bungeni hivi sasainafahamika vema kwa wabunge wote na wote wameshiriki katika kuiunda kutokanana michango ya wabunge katika vikao baina ya wabunge na watendaji wa serikali.Hii ndiyo sababu nikasema tangu mwanzo kuwa bajeti ni mchakato mrefu ambao umehusisha wabunge kwa kina kablahaijawasilishwa bungeni. Kila mbunge anaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamatiyoyote ya bunge hata ambayo haimhusu lengo likiwa ni kumpatia fursa kila mbungekujua kwa kina kinachoendelea serikalini.Jambo la kushangaza ni jazbainayoonyeshwa na wabunge wa pande zote wakati wa kujadili bajeti hii as if nijambo wanaloliona kwa mara ya kwanza. Wabunge wanatumia nguvu nyingi kupinga bajeti hii ilhali walipata fursaya kuipitia kwa kina kabla haijawasilishwa bungeni, huu ni usanii wa kiwangocha juu sana. Hivyo wabunge wetu acheni usanii hii bajeti mnaijua vema namlishaipitia kabla haijawasilishwa bungeni.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Well said Mkuu! umenijuza vizuri sana mchakato wa bajeti. Keep it up!!!
   
 3. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,285
  Likes Received: 10,316
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimekuelewa kabisa. Je kwanini sasa hawa wabunge wanapiga kelele? au wanataka tuwaone? au sifa za kijinga?
  Kwa nini sasa wasingetoa maoni yao kabla haijasomwa?
  Hii hainiingii akilini kabisa.
  Ninadhani kuna wabunge wengine ni wahuni tu.
   
 4. M

  MUNYAMAKWA Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aah! Hii ni dalili ya Waheshimiwa kukimbia vivuli vyao! Kama kweli hivi ndivyo basi hatuwaelewi wanataka kufanya bunge kama sehemu ya kunadi sera zao na kwa maslahi ya vyama vyao na sio ya watanzania!!? Maana haiingii akilini kufanya malumbano juu ya mambo ambayo tayari walishakubaliana kimsingi hapo awali katika kamati zao mbalimbali.Hatuhitaji kuona misimamo yao wala ya vyama vyao bungeni tunaomba waje na changamoto mpya ambazo hazijajadiliwa kwenye kamati zao sio kuprolong muda unneccessarily kwa interest wanazozijua wenyewe. Hii mbwembwe jazz band bungeni ya nini? Wanataka sisi watanzania tujifunze nini juu ya hili au wanathibitisha ukweli wa usemi usemao "wajinga ndio waliwao".Lakini inabidi waheshimiwa hawa wajue Tanzania ya leo sio ya miaka 20 iliyopita
   
 5. s

  swrc JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kiasi fulani uko sawa, lakini ingelikuwa mia kwa mia basi bajeti zisingepekwa kujadiliwa bungeni. Kwa maana nyingine kusingekuwa na haja ya mijadala inayohusu bajeti. Nijuavyo ni kamati za bunge zinazopitia rasimu za bajeti na bajeti zenyewe huwasilishwa kwa wabunge siku chache kabla ya kikao.:llama:
   
 6. a

  afaika Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ingekua hivo basi baketi ingekua inasomwa kama hotuba na kupita hata kwa radio na tv tu.
   
 7. R

  Rwey Senior Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hiz formalities tu, bajet huwa tunaandaa wizarani wabunge na na kamati zao wanakuja tu kusomewa kwenye vikao vya kamati zao, mbona huwa wanashindwa kucontribute idea zozote, wakienda huko bungeni ndo wanaongeea mpaka mambo yasiyohusiana hata na bajeti
   
 8. proisra

  proisra JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayo ni mawazo yako, hayana ukweli wowote na wenye akili tumeona ulichokuwa unalenga, ukakisema pale mwishoni mwa uwongo wako, 'Hivyo wabunge wetu acheni usanii hii bajeti mnaijua vema namlishaipitia kabla haijawasilishwa bungeni'... Nimekusoma kwamba
  Namba 1: Wewe ni kada wa CCM.
  Namba 2: Wewe ni miongoni mwavigogo wala rushwa nchini
   
 9. B

  Bob G JF Bronze Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni usanii 2 hutumika kushirikisha wadau alafu usifanyie kazi mapendekezo yao then uje useme watu walishirikishwa! na hu ndo udhaifu wa mtoa post na Udhaifu wa ccm na wabunge wake na wapambe wote wa Magamba
   
Loading...