"WAHENGA' Ni akina nani Hawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"WAHENGA' Ni akina nani Hawa?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kahabi wa Isangula, May 2, 2012.

 1. Kahabi wa Isangula

  Kahabi wa Isangula JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Maranyingi naona watu wanatumia hili neno 'Wahenga' hasa wanapotaka kutumia misemo yenye Busara.
  Je Wahenga ni akina Chifu Mangungo au Mkwawa?
  Au ni akina Nyerere au Sokoine?
  Na kwa nini tusitumie Jina na Mhusika aliyesema maneno hayo, kama tunavyofanya tunapoongelea maneno ya akina Martin Luther King au Gandhi?

  Je kwa kama hatuwajui majina yao halisi ina maana hata misemo hiyo pia ni ya kizushi au uongo?

  Nifafanulieni tafadhari
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 16,777
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Wahenga hao walisema lini??
  Na walimwambia nani??
  Kwanza sidhani hata Kama hao wahenga walijijua kua wanaitwa wahenga!!!
   
 3. Kahabi wa Isangula

  Kahabi wa Isangula JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Ndo hapo ninapopata maswali mengi Sir. Burn, tusijekuwa tunatumia 'umbea' kwa kisingizio kuwa ni maneno ya Busara ya 'wahenga'


   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,137
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Wahenga ni wazee wa jiji la Dar es salaam!
   
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,640
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani wahenga ni wazee waliotutangulia,ukiangalia wazee wa zamani kuna misemo yao mpaka leo tunatumia,haijulikani hao wazee ni kina nani ila wanaongelewa kwa ujumla.
   
 6. Kahabi wa Isangula

  Kahabi wa Isangula JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu kama hatuna uhakika nani kasema nini kwa maana ya credibility, then kwa nini tukiamini walichosema? Ndo hao hao walisema pole pole ndiyo mwendo?

   
 7. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 883
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  wahenga inabeba ujumla wa mapokeo ya misemo ya zamani kwa njia ya methali ama ya moja kwa moja. wahenga si mtu/watu ama mzee/wazee la hasha hili neno wahenga linabeba jumla yao wale watu wazamani.
  yaani maneno ya kimafunzo toka kwa wazee wetu tangu enzi na enzi.
   
 8. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani muulizaji alikuwa anataka kujua "Wahenga" ni akina nani na kwanini waliitwa hivyo, km nimemsoma vizuri.
   
 9. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  umeniacha hoi mkuu.

  una maana akina abbas Mzimba, Akilimali wanaotaka wakabidhiwe timu na akina Kitwana Kondo!?

   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,586
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  Agree with you 100%.

  Wahenga ni 'ancestors'. Unajua zamani kabla ya development of technology watu walikuwa wanajifunza mambo mbalimbali ya maisha kuanzia afya, ulinzi etc kutokana na matukio yanayowakuta. Mfano mama mjizo anapokula sana aina fulani ya chakula na matokeo yake kufanya mtoto kuwa mkubwa kiasi kwamba njia ya kawaida ya kujifungua ilikuwa haiwezekani na hivyo kupoteza maisha, basi wazee walikuwa wanakusanya matukio kama haya na kuangalia sababu wakigundua wanakaa chini na kuona jinsi ya kuzuia matukio hayo kwa kutumia taarifa tu. Unakuta wanaanzisha misemo kama 'Mama mjamzito akila mayai, mtoto atazaliwa bila nywele' - ujumbe huu ulikuwa na nguvu sana katika kuzuia excessive eating of eggs kwa wajawazito.

  Misemo mingi ilikuwa ikiwekwa na wazee kwa ajili ya kuzuia matukio mabaya waliyokumbana nao katika jamii. Wazee hawa walikuwa wanaaminika sana na jamii. Hivyo basi vizazi vijavyo navyo vinachukua maneno hayo na kuyaendeleza indirectly wanakuwa wanajikinga na majanga ambayo wazee waliisha yafanyia obervation research.

  Mfano tu ni 'Bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi' - ina maana kubwa sana, kama mtu ameepuka janga fulani basi usidhani kuwa ni guaranteed, ndiyo maana katika ajali kuna wanaopoteza maisha na kupona, kwenye ukimwi kuna wanaosahau kutumia co'ndom na kujikuta hawajaambukizwa kwa hiyo usichukukulie kuwa ni kawaida kutokea hivyo, Inawezekana methali hii ,enzi za mababu ikawa ilitokana na 'mwanajamii kusahahu kufunga mlango na usiku swala akaingia ndani na kujipatia kitoweo, ila wakati huohuo kuna mwingine alisahau akaingiliwa na simba na kuliwa'. Haya yote yalitokana na Observation za wazee hao waliokuwa wakiishi enzi hizo.

  'Noun

  wahenga

  1. ancestors (ancestors)

  '
   
 11. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,640
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe kabisa,hawa wahenga ni babu zetu in general
   
Loading...