Judgement
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 10,326
- 4,789
Jirani ninaishi na Mzee wa kihaya , (jina hifadhini).
Ni Mzee aliye attend shule vizuri.
Aidha baada kustaafu , tayari alikua ameshawekeza vitega uchumi vya majumba kadhaa.
Nyumba mbili amezipangisha watu binafsi , na mbili ni Guest House.
Mzee huyu amejipatia umaarufu ktk constituency yetu kufuatia uwezo wake , na pia vituko vyake.
Alishatalikiana na mkewe miaka iliyopita.
Watoto wake ni wakubwa wakiwa wamesambaa mikoa tafauti na shughuli zao.
Burdani ya Mzee huyu , mbali ya kua na nyumba kadhaa , bt hajabakiza ya makazi yake.
Anaishi kwenye chumba kimoja miongoni mwa guest zake.
Wakati flani binti yake aishie Ar alifika kumtembelea. Ikabidi afikie guest , ktk hali isiyo ya kawaida Mzee aliamrisha bintie tozo la pango such as normal customer.
Binti hakua na hiari zaidi ya kulipa , kwa 3days alizokaa na kuondoka zake.
Miezi kadhaa ikapita , akaja mwanae wa kiume toka Dar.
Nae alipofika akakwaana na dhahma kama aliyoikwaa dadie, akalipia room siku 2 akasepa.
Kijana huyu alipofika Dar, ikiwa imepita miezi kadhaa akabuni ni jinsi gani nae amtie adabu Mdingi.
Akampigia simu na kumwambia "Baba mimi naoa next wiki , fanya juu chini ufike , tumia nauli yako , na utarudishiwa ukifika"
Mdingi bila ajizi akafanya kama alivyoagizwa.
Akafika Dar siku aliyotakiwa afike.
Na kijana akafika kumpokea.
Wakachukua Tax na walipofika Mwembechai kijana akamwambia dreva asimame dukani akimuacha Mdingi garini.
Kilichofata kijana ndy akawa amesepa mazima!
Na simu yenye No zake ambazo Mdingi hutumia kumpata yeye akazima.
Kilichojiri huku nyuma Tax driver alimkomalia Mdingi ashuke na alipe kwani hakua na ramani ampeleke wapi !
Dingi hakua na hiyari zaidi ya kulipa , kisha akatafuta guest akajilipia malazi , na palipo kucha akaenda kata ticket kurejea alikotoka!
Hivyo ni baadhi ya vituko vya wahaya.