Manton
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,164
- 1,520
Wahaya ni kikundi cha watu wenye akili sana wanaopatikana katika mwambao wa ziwa Rwelu (Victoria) Magharibi. Mbali na kusambaa kwao dunia kote katika harakati za kuongeza ujuzi na wigo mpana wa maarifa, wamefanikiwa kutunza elimu kubwa katika majina yao, kwa mfano: 1. TIBAIJUKA; liki maanisha, hata watu uwatendee mazuri kiasi gani, daima uwa hawakumbuki chochote kile, japo washukuru tu. 2.TIBESIGWA; umaanisha watu hawaaminiki hata kidogo, chochote ufanyacho usije mwamini mtu. 3.TIBEMOGA, umaanisha watu uwa hawajirudi katika yale wanayokusidia kumtendea mwenzao kwa ubaya. 4. TIBASIIMA, yaani hata watu uwafanyie mema kiasi gani kamwe hawatoshukuru. 5.TIBEKANASHA, umaanisha watu walionuia kutenda jambo lolote kwa nia moja uwa hawakati tamaa hata wakishindwa mara kwa mara katika majaribio yao, mpaka wafikie hatima ya lengo lao. ZINGATIA: hayo ni baadhi tu ya majina, yapo maelfu ya majina. Tuwapongeza Wahaya kwa kuenzi elimu katika vizazi vyake kwa njia ya majina. Karibu, utoe mchango wa mawazo ya nyongeza.