Wahandisi "non-civil engineers" tunahitaji chama chetu tofauti na IET

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Ndugu wahandisi wenzangu ambao taaluma zetu siyo Civil engineers tunahitaji kuunda chama chetu baada "institution for engineers Tanzania/ chama cha wahandisi tanzania kushindwa kusiamamia haki zetu na kupelekea sekita zetu kutokua.

IET imemezwa na civil engineers na haiko kusimamia maslahi ya profession nyingine ambayo yanakinzana au kutoendana na maslahi ya civil engineers.

ili taaluma nyingine ziku zinahitaji mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na serikali ili katika utekelezaji wa miradi iwepo miongozo ya kulinda taaluma hizo ili zishiriki kikamilifu.

mfano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakuta kuna miongozo inalinda maslahi ya Civil engineers mfano kuna miradi unakuta imeandikwa kiongozi wa mradi ni lazima awe na taaluma ya civil engineers kwa uzoefu usiopungua miaka kadhaa.

lakini tunapokuja kwenye miradi ya maendeleo isiyokuwa ya kitanesco hawa hawa ma civil engineers wanafanya kazi zao na kufanya kazi za taaluma nyingine

mfano mimi nimefanya miradi ya maji na kazi za substation ya umeme, pumping station, treatment plants hizi zinahitaji taaluma nyingine lakini unakuta asilimia 75 ya miradi inayofanyika nchini, kazi hizi zinafanywa na ma civil engineers kwa kutumia matekinesheni basi.

na matokeo yake ni dosari nyingi sana katika kazi.

mfano nenda miradi mingi inayofanywa, treatment plants zinaharibika haraka, ndani ya mwaka mmmoja kwa usiamizi mbovu. mbali ni ubovu wa kazi lakini sisi wataalamu wa taaluma hizi tunakosa ushirikishwaji.

Kibaya zaidi hatuna uwanja wa kuongelea haya mapungufu ambayo sisi tunaamini IET ndiyo ilitakiwa kuwa uwanja sahihi.
 
Kuhama na kujitenga siyo suruhisho!
Kwa sababu kanuni za ERB zinatambua uwepo wa taaluma zote za kihandisi!

Pamoja na kwamba civili engineer imedominate sehem kubwa!
Lakini ni ukweli uliyodhahili kwamba asilimia 70% ya kazi za kihandisi zinamhitaji na kumtambua civili engineer kama the king of land to maneuver!

Huwezi kujenga mnara wa umeme pasipo msingi wa civil engineer, huwez jenga hydropower bila msingi wa civil engineer, huwez jenga telecom tower pasipo kumshilikisha civil engineer!

Huwezi kutua na ndege pasipo landing iliyojengwa na civil, huwezi paki meli kwenye gati isiyojengwa na civil!

Kiufupi civil inaingia sehem kubwa sana na ndiyo maana hata kwenye chama anaonekana kudominate!
Kwahiyo kujitenga ni sawa na kutenganisha barabara na gari maana yake gari ipite porini?
Katika chama ziko departments/wings za kila taaluma! Tumieni hizo kufikisha kero,

Hata chama madakitali wako hivyo, pamoja na chama kikuuu, zipo wings za madakitali kulingana na taaluma zao!
Hakuna kinachoharibika mkuu!
 
ni kweli kujitenga hakujengi katika nadharia pana lakini pale unapokuwa ndani ya familia isiyotambua uwepo wako na kukupatia nafasi stahiki kujitenga kunaweza kuwa na faida.

tunatambua ukubwa wa field ya civil engineer na sisi hatuna shida na hilo shida yetu ni kuona tunaendelea kufanya kazi kama miaka ile taaluma nyingine hazijazaliwa.

hatuna shida na civil engineer kujenga jengo bali tunalalamika kuona civili engineer bado anajenga base ya mnara, anasimamisha mnara na kufanya kazi zte za kihandisi peke yake bila uwepo wa wahandisi wengine na kuhusishwa pale taaluma zao zinapohitajika.

tunachotaka civil engineeer ajenge jengo hatuna shida na hilo lakini kazi za umeme afanye mtu wa umeme, kazi za plumbing kuanzia consultant mpaka mkandarasi tunahitaji kuona wahandisi wa fani hiyo wakidesign, kufanya na kusimamia na siyo civil kubababaisha akimaliza kazi zake za kujenga.

kazi za electronics tunahitahitaji mtu wa electronics afanye kazi hiyo.

kila mtu afanye kazi yake na kuwepo na maelekezo ya kiserikali yanayosimamia kila taaluma ifanye kazi zake.

maelekezo ya serikali hayapo lakini kubwa ni kwa nini hayapo sisi tunaona vyombo vya kusimamia haya vimekaliwa na hawa wenzetu.

sisi tunachotafuta ni ama vyombo husika vifanye kazi zake kwa kuishauri serikali na vikikaa kimya hatuna namna bali kutafuta platform zetu wenyewe ili tupaze sauti.
 
Una hoja ya msingi, lakini yanazungumzika!. Tatizo linaanza kwenye usajili wa mradi!
Ilekebishwe sheria ya kusajili mradi, ili waondoe kitu kinachoitwa MAIN CONTROCTOR ! Ili wengine wasionekane kama sub kwamba wanaweza wajibishwa na main contractor.

Watafte utaratibu wa site ili kila mtu awe na usajili wake kwa mkataba wake separate na main contractor.
La sivyo civil atarndelea kushikilia kazi zote! Wengine mpewe day workers
 
mambo ya kufanya ni mengi mfano

ili taaluma zetu zikue tunataka kuanzia design, execution, supervision ya execution engineer yeyote asifanye kazi ambayo siyo profession yake.

Structural engineer afanye kaze zake za structure, water resorces afanye kazi yake, electrical afanye yake, mechnical afanye yake, computer afanye yake.

shida tuliyonayo mfano unafanya mradi wa maji umegharamiwa na serikali.

kazi ni kuvuta umeme wa tanesco, kuweka substation ya umeme, kujenga intake ya maji, kuweka pump za maji, kujenga matenki, kuweka mifumo ya kusimamia uzalishaji kama scada na camera, kujenga matenki ya zege ya kuhifadhi maji, kujenga mifumo ya kusafirisha na kusambaza maji kutumia mabomba.

unakuta consultant ambaye anasiamamia kazi anatumia wahandisi wa civil engineer tu, hakuna mtu wa umeme wala mechanical wala compyuta.

tunachotaka ni taratibu zinazosema zege ikifanyika lazima kuwe na mtaalamu wa zege kama ni civil sawa.

substation ya umeme inapofanyika lazima msimamizi awe na mtalaamu wa anayehusika na substation.

kama pump station inafanyika lazima ifanywe na mtaalamu anayehusika na pumpstation.

kwa sasa taaluma nyingine na kwa uchache zinaitwa kufanya commissioning tu wakati kila kitu kilishafanyika.

main contractor anaweza kuwepo ila kazi ambazo yeye hana utaalamu anaambiwa zifanywe na mtaaalamu wa fani husika.

consultant naye lazima awe na mtaalamu husika
 
Mkuu wewe umebobea kwenye uinjinia gani? Watu tumegonga COET petroleum engineering lakini saivi tunacheza ndombolo uswazi
kwanini ucheze ndombolo uswazi,ivi mtu aliyesomea Petroleum eng akifanya kazi ya Pump attendant kwenye vituo vya mafuta hapo anakuwa amejidhalilisha ama
 
Kuhama na kujitenga siyo suruhisho!
Kwa sababu kanuni za ERB zinatambua uwepo wa taaluma zote za kihandisi!

Pamoja na kwamba civili engineer imedominate sehem kubwa!
Lakini ni ukweli uliyodhahili kwamba asilimia 70% ya kazi za kihandisi zinamhitaji na kumtambua civili engineer kama the king of land to maneuver!

Huwezi kujenga mnara wa umeme pasipo msingi wa civil engineer, huwez jenga hydropower bila msingi wa civil engineer, huwez jenga telecom tower pasipo kumshilikisha civil engineer!

Huwezi kutua na ndege pasipo landing iliyojengwa na civil, huwezi paki meli kwenye gati isiyojengwa na civil!

Kiufupi civil inaingia sehem kubwa sana na ndiyo maana hata kwenye chama anaonekana kudominate!
Kwahiyo kujitenga ni sawa na kutenganisha barabara na gari maana yake gari ipite porini?
Katika chama ziko departments/wings za kila taaluma! Tumieni hizo kufikisha kero,

Hata chama madakitali wako hivyo, pamoja na chama kikuuu, zipo wings za madakitali kulingana na taaluma zao!
Hakuna kinachoharibika mkuu!
Ohohh.. Mbona kwenye kila barabara kuna yale bulldozer nayo si yanahitaji mechanical engineers pia?..

Mbona kwenye jengo lolote kuna umeme napo si anahitajika Electrical engineer pia.. Mbona kwenye kila airport kuna telecom Towers napo si anahitajika Telecom Eng pia?.. kwanini kusiwe na mutual distribution kwenye miradi sio kila mradi aongize Civil Eng.. yani nae apewe kitengo chake ndo nilivyomuelewa mleta mada yani
 
Aaah, kwanza inabidi wahandisi tuje tufungue uzi wetu ili tuwe tunapeana changamoto zetu, wale wanangu wa mechanical tukutane na jinsi ya kuzitatua.
 
wahandisi mbinu kama hizi muhimu sana katika ulimwengu wa leo
 
Back
Top Bottom