Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,961
- 24,191
Mkuu, tatizo ni lako. Kama huwezi kuwavumilia maswaibu yao, fanya mpango uhaame au jenga kwako.Bonjour
Aisee , najuta kupanga na Hawa watu "Waha" nataka kuhama hapa
Ni Wabishi sijawahi kuona
Wachafu kinoma,
Wana makelele
Kujisifu Sasa, wakiwa ndani wanacheka utafikiri humo ndani Kuna matajiri
Wanasifa, kila muda ni simu za mihamala tu haha
Sasa, ukute Muha ni mshabiki wa Yanga,
Wanafua kila siku
Turudi kwenye uzi;
Ubishi ni hulka. Si waha tu wabishi, makabila mengine yapo. Na siyo waha wote ni wabishi.
Uchafu? Hilo ni tatizo.
Kujisifu? Kwa namna ipi? Kama mtu kafanikisha lake kwa viwango basi acha ajisifie.
Anayepaswa kucheka ni tajiri pekee? Maskini yao kununa? Nani kaweka hii principle? Hapana, kila mtu afurahi kwa namna yake.
Simu za miamala? Swadakta kabisa. Hujui furaha ya kupata muamala? Nafsi huwa inazuuzika na huponya magonjwa ya moyo ikiwemo sonona.
Baya ni hilo la UCHAFU tu. Na labda makelele pia. Mengine yote ni hayana mantiki.
Sijamaliza, umesema ni Wachafu huku ukisema wanafua kila siku. Huo uchafu ni wa namna gani? Kufua ni usafi.
Hiii contradiction yaweza tu kutoka kwa mtu mwenye chuki iliyopitiliza kwa waha .Acha upumbavu .

