Wagonjwa Muhimbili walia adha ya mgomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagonjwa Muhimbili walia adha ya mgomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Rodrick Kabangila, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu suala la maslahi kwa madaktari na kuitaka Serikali kutoingiza siasa katika taaluma ya udaktari na uuguzi.Picha na Joseph Zablon​
  Joseph Zablon na Ibrahim Yamola
  BAADHI ya wagonjwa na madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamesimulia adha wanazopata kutokana na kufukuzwa kwa madaktari wanafunzi waliokuwa wamegoma na wameiomba Serikali ifanye kila linalowesekana kunusuru hali hiyo.

  Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, walisema mgomo huo umefanya hali katika hospitali hiyo kuwa mbaya, kiasi cha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma.

  Mmoja wa wagonjwa hao Godliver Alfonsi aliyetokea mkoani Kigoma alisema ana wiki moja tangu afike hospitalini hapo lakini hajaweza kuonana na daktari.

  "Tangu nije leo (jana) tu ndio nawaona madaktari wakipita, lakini kwangu hawakupita kwa kuwa muda ni mdogo na wameniahidi kuwa watakuja kwangu kesho (leo)," alisema.

  Mama wa mtoto Fatma Iddi katika wodi ya jengo la watoto, Hidaya Idrisa alisema madaktari hawaonekani wodini hapo kama ilivyokuwa awali.

  Alisema kabla ya mgomo madaktari walikuwa wakikaa katika moja ya vyumba vya wodi hiyo, hivyo ilikuwa rahisi kuwapata kunapotokea tatizo.

  “Madaktari hapa walikuwa hawaondoki kila wakati wapo na wakati wowote ukiwa na shida unapata msaada lakini hivi sasa chumba chao kitupu, hawapo” alisema Hidaya.

  Hali katika wodi ya Kibasila pia ni mbaya na muuguzi wa zamu katika moja ya wodi za jengo hilo alisema; "Inawachukua muda wagonjwa kuonana na daktari kutokana na uchache wa madaktari."

  “Mfano daktari ambaye yupo sasa aliingia kazini jana (juzi) mpaka sasa ninavyoongea hajaondoka maana yuko peke yake,” alisema muuguzi huyo.

  Mgonjwa mwingine hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema: “Tangu asubuhi sijaonana na daktari sasa ni mchana (saa 12.30) na sina tumaini la kupata huduma”.

  “Kama ningekuwa mahututi pengine hata wewe mwandishi usingenikuta, tungekuwa tunaongea mengine hapa,” alisema mgonjwa huyo.

  Mmoja kati ya wanafunzi (jina limehifadhiwa), ambaye yupo katika mafunzo kwa vitendo tatu mwezi Desemba mwaka jana hosipitalini hapo, anasema hali si nzuri na kwamba ikiendelea hivyo huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

  “Idadi ya vifo vya sasa huwezi kuvihusisha na mgomo moja kwa moja lakini sina shaka kabisa kuwa vipo ambavyo vinachangiwa na hali hii,”alisema daktari huyo mwanafunzi.

  Alisema kwa sasa madaktari bingwa hawana wasaidizi hali ambayo inawafanya wafanye kazi muda mrefu na kushindwa kuwafikia baadhi ya wagonjwa.

  “Madaktari wanachoka, hata sisi wachache ambao tunasaidiana nao tunakuwa katika wakati mgumu” alisema na kuongeza kuwa hali hiyo inawafanya wawazungukie wagonjwa hadi saa nane mchana badala ya muda wa kawaida wa saa mbili asubuhi.

  Madaktari
  Katibu wa Chama cha Madakitari Tanzania (MAT) Dk. Rodrick Kabangila alisema tabia ya Serikali kuingiza siasa katika taaluma inaathiri huduma kwa umma.

  Alisema kila jambo hivi sasa linachukuliwa kisiasa kwa kupiga porojo badala ya utekelezaji na kwamba sasa siasa zimeingia katika taaluma ya udaktari na uuguzi.

  Kabangila alisema serikali inatumia mamilioni ya shilingi kuwatibu viongozi nje ya nchi lakini inashindwa kutumia pesa hizo kuwalipa madaktari stahili zao na kununua vifaa tiba vya kisasa.

  Alisema Tanzania inaongoza kwa kupeleka wagonjwa nchini India, sifa ambayo alisema si nzuri na kwamba hatari zaidi viongozi serikalini wanajivunia hali hiyo.

  Katibu huyo alisema wamekaa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na viongozi wengine wa serikali na wamewataadharisha juu ya mwenendo huo.

  Kabangila alisema chama cha madaktari kitafanya mkutano wake mkuu Jumamosi ijayo, ambao pamoja na mambo mengine utajadili masuala ambayo yamejitokeza katika mgomo huo na kufikiria hatua zaidi za kuchukua.

  Alisema wanaishangaa wizara ambayo baada ya kulipa posho za madaktari wanafunzi wamewaita wahusika wizarani na kwamba hatua hiyo ni kukwepa hoja ya msingi.

  Kauli ya Serikali
  Madaktari hao 229 walianza mgomo Jumanne wiki iliyopira, wakiishinikiza Serikali iwalipe posho zao za Desemba mwaka jana ambazo ni zaidi ya Sh179 milioni.

  Kwa mujibu wa madaktari hao, uamuzi huo ulifikiwa baada ya wizara kushindwa kuwalipa posho zao kwa wakati hali iliyowafanya waishi kwa tabu.

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, alikiri hali hiyo na kusema kuwa imesababishwa na ukata ulioikumba wizara hivyo kushindwa kuwalipa madaktari hao kwa wakati.

  Dk Mponda alisema kwa kawaida posho hizo hulipwa tarehe 22 ya kila mwezi na kwamba kiasi cha fedha ambacho hulipwa ni Sh900 milioni kwa madaktari wanafunzi nchi nzima.

  Pamoja na maelezo hayo, serikali iliwapa barua za kujieleza madaktari wote waliokuwa wamegoma licha ya kwamba baadhi yao walishaanza kurejea kazini baada ya kuwa wamelipwa posho hizo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Chanzo. Wagonjwa Muhimbili walia adha ya mgomo
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii tabu tupu hii, kweli politiks kila pahala hata kwenye afya na uhai wetu HAIKUBALIKI kabisa
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,106
  Trophy Points: 280
  nyoni kesha amua, unadhani tutapona?
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi nahisi hatuponi Kamanda wangu!
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  unacheki kwa background jinsi bluecool ilivyochakachuliwa na uhai? All in all, madaktari, walimu ni watu muhimu mno. Wasikillizwe
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  Nimemsikiliza nyoni BBC kweli ni jeuri ...
   
 7. C

  Claxane Senior Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mradi wa kupeleka wagonjwa appolo umeiva. Nendeni wizarani mpate barua kwenda india. Mungu atunusuru tusiumwe
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  huko huko Muhimbili kwenye habari jana kuna wagonjwa wamehojiwa na wakasema wanapata huduma kama kawaida...
   
 9. s

  saved Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  kwani nyoni kasemaje bbc leo?
  jana wagonjwa muhimbili walisema wanapata huduma kama kawaida...
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Muhimbili vifo vyaanza kutokea
  [​IMG] Taasisi ya Kansa Ocean Road hakufai
  [​IMG] Dodoma, Mbeya, Morogoro moto
  [​IMG]
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda


  Athari za mgomo wa madaktari zimeanza kujitokeza kufuatia wagonjwa kuanza kufa huku ukisambaa katika mikoa kadhaa nchini.
  Jana hali ilikuwa mbaya katika hospitali kubwa za serikali ikiwemo ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Saratani Ocean Road ambako huduma zilisimama kabisa.
  Uchunguzi wa NIPASHE katika hospitali hizo umebaini kusimamishwa kwa huduma katika idara zote muhimu na katika hospitali ya Muhimbili; kitengo cha magonjwa walio katika uangalizi maalum (ICU) ndicho kilichokuwa kinafanyakazi kwa ukamilifu.

  MWAISELA HOI
  NIPASHE iliingia kwenye wodi kadhaa za jengo la Kibasila na katika wodi namba 22 inayohudumia wagonjwa wa kibofu cha mkojo, hali ilikuwa mbaya na wagonjwa waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa hawajapewa dawa tangu juzi, madaktari walipotangaza mgomo.
  Mgonjwa mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema “hatujapewa dawa tangu jana (juzi) na hakuna dalili yoyote ya kupata dawa, ni bora tu waniruhusu niende nyumbani kwa sababu kwa ugonjwa wangu najua nitakufa mapema.”
  Katika wodi namba tatu ya jengo la Mwaisela zinazohudumia akina mama wa magonjwa mchanganyiko; mwanamke mmoja anayemuuguza ndugu yake hapo aliyejitambulisha kwa jina la Hawa Ramadhani alisema tangu juzi mgonjwa wake hakuwa amepewa dawa hivyo hali yake ilikuwa mbaya.
  “Manesi wamesema hawawezi kumsaidia kwa kuwa hawana vifaa na hata hivyo anatakiwa kuonwa na daktari kwanza,” alisema.
  Katika wodi namba nne; kwa mujibu wa ndugu wa wagonjwa ni kwamba watu saba walikuwa wamefariki tangu asubuhi ya jana na hadi NIPASHE ilipofika kwenye wodi hiyo, maiti moja ilikuwa haijaondolewa wodini hapo.
  Katika wodi namba tisa na 10, hali ilikuwa hivyo hivyo na daktari mmoja ambaye hakutaja jina lake aliiambia NIPASHE kwamba kitengo kinachofanyakazi kwa ukamilifu ni ICU tu wakati vitengo vingine madaktari walikuwa kwenye mgomo.
  Kwa upande wa Taasisi ya Mifupa (MOI), mgomo uliwalazimu wagonjwa kuondoka kwa kuwa hawapati huduma.

  WAGONJWA WRUHUSIWA
  NIPASHE ilizungumza na muuguzi mmoja ambaye alisema kinachofanyika hospitalini hapo ni kuwaruhusu wagonjwa wanaopenda kurudi nyumbani au kwenda kutafuta huduma kwenye hospitali nyingine kwa kuwa madaktari bado wanaendelea na mgomo.
  Wakati hali ikiwa hivyo, madaktari wametangaza kuendelea kushikilia msimamo wao wa kugoma na wameipa serikali saa 24 hadi leo saa 5:00 asubuhi iwe imeshughulikia madai yao ya msingi ikiwemo kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza mishahara na maslahi yao vinginevyo mgomo utaendela bila kikomo.
  Akizungumza kwa niaba ya madaktari, Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Muhimbili, Magesa Paul, alisema wameiandikia barua Serikali kuitaka kuwatimizia matakwa yao na wameitaka iwajibu kabla ya saa 5:00 asubuhi leo.
  “Hadi ifikapo kesho (leo) saa tano asubuhi serikali iwe imeshatoa majibu ya barua yetu, la sivyo tutaendelea kugoma,” alisema.

  OCEAN ROAD HALI TETE
  NIPASHE ilifika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kushuhudia wagonjwa wakiwa nje bila kupewa huduma huku kukiwa na matangazo kila kona ya hospitali yakieleza kwamba baadhi ya huduma zimesimamishwa kutokana na mgomo wa madaktari.
  “Tunasikitika kuwataarifu watu wote kuwa kutokana na tatizo la mgomo wa madaktari katika vitengo, baadhi ya vitengo havitaweza kutoa huduma za dharura hadi mtakapotangaziwa,” lilieleza sehemu ya tangazo lilikuwa limebandikwa hospitalini hapo.
  Tangazo hilo lilisisitiza kuwa vitengo vinne ndivyo vilivyokuwa vinatoa huduma za dharura ambavyo ni wagonjwa waliolazwa, Chemotherapy, Cancer Screening na Radio Therapy.
  Aidha, taasisi hiyo imesitisha pia kupokea wagonjwa wa rufaa kutoka hospitali nyingine kutokana na ukosefu wa madaktari uliosababishwa na mgomo huo.
  Juhudi za kumpata mkurugenzi wa hospitali hiyo ziligonga mwamba kutokana na kuwepo kwenye kikao na Ofisa Habari wa hospitali hiyo alikataa kuzungumzia tatizo hilo kwa maelezo kuwa msemaji ni mkurugenzi pekee.

  MBEYA MOTO
  Madaktari 75 wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya wamegoma kutoka huduma za matibabu kwa wagonjwa.
  Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dk. Eleuter Samky, alisema kati ya madaktari hao waliogoma jana 10 ni watumishi walioajiriwa na 65 ni madaktari wanafunzi ambao wametoka masomoni hivi karibuni.
  Dk. Samky alisema hali ni mbaya kwa wagonjwa kutokana na madaktari hao kugoma kufanya kazi.
  Alisema madaktari bingwa, baadhi ya wauguzi na kitengo cha upasuaji wa mifupa na wafamasia ndio wanaofanya kazi.
  Dk. Samky alisema uongozi wa hospitali hiyo unatarajia kuzungumza na madaktari waliogoma kwa lengo la kuwashawishi kurejea kazini kuendelea kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
  Kufuatia mgomo huo, wagonjwa nao walilalamika kukosa huduma katika Hospitali ya Wazazi Meta iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
  Baadhi ya wagonjwa wakizungumza na NIPASHE walilalamikia mgomo huo kwa madai kuwa unahatarisha maisha yao kwa sababu hawana fedha za kwenda kugharimia matibabu katika hospitali binafsi.
  Walisema waliwahi kufika katika hospitali hizo tangu asubuhi na kwamba wamekosa hata huduma za kuandikishwa mapokezi.

  DODOMA NAKO HALI TETE
  Mkoani Dodoma nako hali si shwari kwani zaidi ya watumishi 100 wa kada mbalimbali wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma jana waligoma kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuboresha mazingira ya mazuri ya sekta ya afya nchini.
  Watumishi waliogoma ni madaktari, wauguzi, maabara, wafamasia na wa kada ya afya ambapo madai yao ya msingi ni kuitaka serikali iboreshe mazingira ya kazi na afya.
  Madai mengine ni pamoja na serikali kuongeza vifaa, maslahi kwa madaktari na wauguzi, kukosekana kwa jenereta ya dharura pindi umeme unapokatika, huduma ya mama na mtoto, wazee na posho ya hatari kazini.
  Mgomo huo ambao ulikuwa wa siri ulianza juzi jioni na kuambatana na vikao vya mara kwa mara vya wauguzi na madaktari wa hospitalini hapo.
  Hata hivyo, jana asubuhi NIPASHE ilishuhudia hospitali hiyo ikiwa na wagonjwa wengi ambao walishindwa kupata huduma za matibabu na dawa kutokana na madaktari na wauguzi kuwa kwenye vikao.
  Vikao hivyo ambavyo vilisababisha wagongwa kutopata huduma na kuwa na msongamano, vilianza jana saa 3 asubuhi hadi 7 mchana.

  Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Katibu Tawala wa Mkoa, Rehema Madenge kuhudhuria kwenye kikao hicho ambacho alikaa na watumishi hao zaidi ya saa tatu, lakini hakupata muafaka wa mgomo huo.
  Akizungumza na NIPASHE, Rehema alisema: “Nimekaa nao zaidi ya saa tatu nikiwasihi wasiendelee na mgomo, ili wakaokoe roho za watu.”
  Rehema alisema pamoja na kuwa madai ambayo yanatolewa na watumishi hao ni ya msingi, lakini aliwataka waendelee na kazi huku yakiendelea kutatuliwa.
  Akizungumza na waandishi habari mara baada ya kikao hicho cha dharura kilichodumu zaidi ya saa sita, Katibu wa Kamati ya kushughulikia madai ya watumishi, Dk. Cassian Mkuwa, alisema lengo la mgomo wao ni kuweka shinikizo kwa serikali ili iboreshe mazingira ya hospitali.
  Dk. Mkuwa alisema serikali inatakiwa kuboresha mazingira ya hospitali nchi nzima, kuongeza dawa, vifaa pamoja na kipato cha madaktari na wauguzi.
  Alisema bado wataendelea na mgomo huo ingawa watatoa huduma kwa wagonjwa wa dharura hadi hapo madai yao yatakapotatuliwa.
  “Sisi madaktari hatujaja hapa kwa ajili ya kuua, tupo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa, hivyo nayo serikali inatakiwa kututambua,” alisema.
  Alisema wanatarajia tena kukutana leo katika kikao cha dharura kinachotarajia kufanyika saa 10 jioni kwa ajili ya kupitia masuala mbalimbali.
  Wakizungumzia hali iliopo hospitalini hapo, mmoja wa wagonjwa ambaye alikuwa wodini, Philip Remagi, alisema hali imekuwa ngumu kutokana na madaktari kutoingia wodini.
  Remagi alisema tangu alipobahatika kuhudumiwa na kusafishwa mguu wake hadi jana hakuna muuguzi wala daktari aliyetokea kwa ajili ya kumuhudumia.
  “Niliwaomba waje wanisafishe mguu wangu…lakini wamenijibu kuwa wapo kwenye kikao…hivyo nimeamua kukaa hivi hivi tu,” alisema.
  Naye mgonjwa, Abubakar Mputaputa alisema ameingia hospitalini hapo tangu Jumapili, lakini hadi jana hakupata huduma zozote.
  Mputaputa alisema serikali inatakiwa kuingilia kati mgomo kwa sababu wanaothirika ni wananchi.

  “Kwa nini huduma isiwepo…kwani serikali hailioni hili…wizara husika nayo ipo wapi? Rais je? Kwa nini watu wagome, maana kila sehemu kuna mgomo. Nchi inaelekea wapi jamani?” alihoji mgonjwa huyo.

  ARUSHA WACHAPA KAZI
  Wakati hali ikiwa hivyo kwenye hospitali hizo, mkoani Arusha katika hospitali ya Mt. Meru madaktari walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida.
  Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Omar Chande, akizungumzia hali kuhusu mgomo huo, alisema madaktari wote hospitalini hapo wanaendelea na kazi zao.
  “Niliondoka jana (juzi) huko Arusha, siku ambayo mgomo ulitangazwa kuanza, lakini madaktari wangu pale hospitali waliendelea na kazi na hata leo (jana) sijapata taarifa tofauti,” alisema.
  Hata hivyo, akizungumzia mgomo huo, Dk. Chande alisema baadhi ya madai yaliyotolewa na chama hicho ni ya msingi, lakini hayafanani kwa kwa kila sehemu.
  Alisema kila sehemu ina utaratibu wake wa kushughulikia malalamiko na madai na kwamba kwa upande wao yanashughulikiwa na ngazi husika.
  Uchunguzi zaidi wa NIPASHE jijini Dar es Salaam umebaini kwamba katika hospitali za Manispaa yaani Mwananyamala, Temeke na Amana, kulikuwa na mgomo baridi na madaktari hawakuwa wanatoa huduma kwa wagonjwa wote hususani wapya (OPD).

  PINDA AWAITA MADAKTARI
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaomba madaktari kwenda ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam wakati wowote kuanzia sasa ili wakazungumzie madai yao na kupata suluhu.
  Aliyasema hayo jana ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wahariri na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
  "Nimeona kabisa madaktari na Wizara ya Afya wamefikishana pabaya, hawaivi kabisa hivyo suluhu haitapatikana, mimi nipo ofisini naomba waje tuzungumze maana hali ni mbaya," alisema.
  Alisema kimsingi anakubaliana na madai ya madaktari hao kuhusu posho zao, lakini ni jambo zuri kukaa mezani na kuyamaliza badala ya kugoma.

  Alisema mgomo unaoendelea unawanyima haki ya kupata tiba wagonjwa wanaofika katika hospitali mbalimbali.

  “Najua mtu ambaye hajaajiriwa namna anavyopata shida posho yake ikichelewa maana hana mshahara, ni kweli posho ilichelewa ila tatizo naona ilikuwa usahihi wa taarifa za kuchelewa kwa posho hizo ndo sababu ya mtafaruku uliotokea,” alisema.

  “Najua wagonjwa wanapata shida sana kutokana na mgomo huu maana madaktari hawa ndio wanashinda wodini na wagonjwa, ndio sababu nasema waje tuzungumze kabla sijaenda Dodoma siku ya Jumamosi, haya mambo yanazungumzika kabisa,” alisema.

  MGAYA AKWAMA

  Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Shirikishi la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania (Tucta), Nicolas Mgaya warudi kazini ndipo wafanye mazungumzo na serikali wakiwa kazini.

  Mgaya alizungumza na madakati hao jana kwenye ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam wakati madaktari hao walimwomba kuzungumza nao kwa lengo la kuwapa mwongozo wa mgomo wao.

  Katibu huyo aliwaambia kuwa ilikuwa ni busara kuendelea na kazi na kuacha kuvunja miiko ya udaktari walioapa kwa kugoma licha ya kuvunja sheria za nchi na maadili ya udaktari wenyewe.

  Baada ya kushindwa kuwashawishi madaktati hao kuacha mgomo, alilazimika kuondoka katika ukumbi huo baada ya madaktari kukataa kata kata kukubaliana na ushauri wake.

  Dk. Ulimboka alimwambia Mgaya kuwa wataendelea kugoma hadi serikali watakapoamua kusikiliza madai yao.

  Dk. Ulimboka aliwapa taarifa madaktari hao ya kuungwa mkono kwa wauguzi na madaktati wengine kutoka mikoa mingine hapa nchini.
  Walidai kuwa Wauguzi walikuwa mbioni kuunga mkono mgomo huo kwa madai kuwa baadhi ya maslahi waliokuwa wakipigania madaktari hao yalikuwa yanahusu pia wauguzi hapa nchini.

  MAT WALIWASHA MOTO
  Mgomo wa madaktari nchi nzima ulitangazwa na Chama cha Madaktari (MAT) mapema wiki hii na ilielezwa kwamba hautakuwa na kikomo hadi madai yao yatakaposhughulikiwa.
  Mwenyekiti wa kamati ya muda ya jumuiya hiyo ya madaktari, Dk. Steven Ulimboka, aliitisha mgomo huo ambao pamoja na mambo mengine wanataka Rais Jakaya Kikwete kumwondoa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mpona na Naibu wake D. Lucy Nkya.

  Pia wanataka Rais Kikwete kumwajibisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Deo Mtasigwa pamoja na kuwaboreshea mazingira ya kazi.  Imeandikwa na Gwamaka Alipipi, Moshi Lusonzo, Tryphone Mweji na Joseph Mwendapole, Dar; John Ngunge, Arusha; Jacqueline Massano, Dodoma na Thobias Mwanakatwe.  CHANZO: NIPASHE
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  tunaubiri kujiuzulu kwa blandina
   
 12. k

  kiche JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naamini huyo atang'oka,jk hana utaratibu wa kumwajibisha mtu
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Serikali yetu haijufunzi hata kidogo. Mwaka jana tulishughudia uzembe wa kutisha wakati wa mgomo wa wauza mafuta. Serikali iligeuka bubu, haikujulikana kama nchi hii ina rais, makamu wa rais, waziri mkuu au baraza la mawaziri. Hakukuwepo na mpango wa dharura wa kutoa mafuta wakati mgomo unashughulikiwa. Sijui ingekuwa kama nchi ingevamiwa! Sasa miezi michache baadae mgomo wa madaktari, wapigania 'uhai' wa watanzania-wapiga kura na walipa kodi wamegoma lakini serikali inaendelea 'kurembua' kwa mtindo ule ule! Hakuna mpango wa dharura, watu wanakufa kwa kukosa huduma!

  1. Nilitegemea hadi sasa kuwepo na kikao cha dharura cha baraza la mawaziri na kujadili namna ya ku-deal na huu mgomo - NIL
  2. Waziri mkuu angekuwa amekutana na viongozi/wawakilishi wa chama cha madaktari kwa majadiliano ya kutafuta muafaka - NIL
  3. Waziri wa afya angekuwa ametangazia wananchi juu ya hospitali zilizokumbwa na huu mgomo na kusema nini serikali inafanya kwa kipindi hiki ili kuhakikisha wagonjwa (hasa wale walio mahtuti) wanapata matibabu - nayo NIL

  Jambo moja ni wazi, viongozi wengi serikalini are out touch, hawaonekani hata kidogo kujua nini wananchi wanataka? na mbaya zaidi hawajui kama watanzania wa leo sio wa miaka 47. Mikakati ya serikali (of lack of it) ni butu mno, inatia aibu kama sio hasira, e.g. serikali inawataka madaktari wote warudi kazini? really? serikali imekuwa inaboresha utoaji wa huduma za afya mwaka hadi mwaka! sasa kwanini madkatari wanagoma? au kwa nini mnapeleka watu India kama mmekuwa mnaboresha huduma za afya mwaka hadi mwaka?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nawaunga mkono madaktari
   
 15. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Regime change - regime change - regime change
   
 16. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni habari ya kusikitisha,

  Binti mmoja anayejulikana kwa jina la L. Njau amefariki ktk hosp ya muhimbili kwa kukosa huduma kutokana na mgomo wa madaktari.

  Binti huyo aliyekuwa ni mjazito na akisumbuliwa na ugonjwa wa nimonia alifikishwa muhimbili kwa refer kutoka hosp moja ya binafsi na maarufu iliyopo mitaa ya posta jijini. Bint alikuwa mfanyakazi wa kampuni moja maarufu kutoka nje (jina linahifadhiwa) iliyopo barabara ya mandela inayohusika na mambi ya logistics.

  Mungu ailze roho yake pema peponi.

  kiburi hiki cha serikali ya ccm na kutojali wananchi wake kinazidi kutuumiza watz.
   
 17. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  baba yao yuko davos anakunywa wine !
   
 18. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  No! emergency zinakuwa attended na kuna madaktari wanawaona wagonjwa waliozidiwa.
  Kama amefariki ni siku tu ilikuwa imefika sio kwa sababu ya mgomo.
   
 19. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Dah kakataa kula wakati ugali ndo umefikia kwenye chorus.
   
 20. j

  jigoku JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Poleni wafiwa,mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

  Tujiulize kwa kutafakari kwa kina juu ya serikali hii ya CCM.
   
Loading...