Tetesi: Wagombea waliopitia JKT iwe kwa mujibu wa sheria au kwa hiari kupewa kipaumbele kura za maoni CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,150
Ukiondoa uzalendo binafsi ambao mtu huzaliwa nao uzalendo mwingine hupatikana kwa njia ya mafunzo yatolewayo katika Jeshi la Kujenga Taifa kwa kifupi JKT.

Inasemekana kupitia tetesi kwenye korido za Lumumba kwamba zamu hii kulitumikia jeshi la kujenga taifa itakuwa ni kipimo cha uzalendo wako kwa taifa.

Kwamba CCM haitaki wabunge makasuku bali wale wenye uwezo na utayari wa kusonga mstari wa mbele kwa ajili ya kulitetea taifa kwa hali na mali.

Ni hayo tu kwa uchache.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwenye Uchaguzi wa Serikal za Mitaa waliokataa kuchangia Mwenge walipigwa chini, hata wasio na vyeti vya JKT wasipewe form za kuwania uongozi na Tume ya Uchaguzi
 
Nchi inaenda kuwa chini ya jeshi na sio raia tena!!!yaani viongozi wa umma wataongea lugha za kijeshi ambazo raia hawajui!!!
Unaelewa maana ya Jeshi la Kujenga Taifa?

Muulize Halima James Mdee alipitia huko atakueleza uzuri wake!
 
Masikini wa fikra huwa na tabia ya kujitengenezea matatizo ambayo hayapo, na kuacha kutatua matatizo ambayo yapo.

Ndiyo maana nchi ina matatizo kibao, watu wanahamisha mji mkuu, kitu ambacho si tatizo.

Hili la JKT ni humo humo tu.

Kwanza ni discrimination, kuna wengine hawaendi JKT kwa sababu za kiafya, si kwa kukosa uzalendo.

Sasa hao nao unawabagua kwa kigezo cha uzalendo kivipi?
 
Hawawezi kuteuliwa kwa sababu hizo hizo za kiafya!
 
Kwa lugha nyingine wabunge lasaba hawatakiwi
Subutu! CCM na la saba ni kama chupi na kalio, hawawezi kuachwa hao maana ndio hutumika pale uuangaji mkono unaotaka kutokuwa na aibu unapotokea.
Hats hivyo mpango huo ni mipango mingi ya hovyo kama ya Makonda
 
Kwenye Uchaguzi wa Serikal za Mitaa waliokataa kuchangia Mwenge walipigwa chini, hata wasio na vyeti vya JKT wasipewe form za kuwania uongozi na Tume ya Uchaguzi

..Je, lengo lenu ni kumuengua HUSSEIN MWINYI?

..Just be careful msijekuwa mnatengeneza mtego wa panya mkanasa hata wasio walengwa.

Cc Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom