Wagombea 45 kutoka vyama vya Upinzani Tanzania waenguliwa kugombea udiwani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
WAGOMBEA udiwani 45 kutoka vyama vitatu vya upinzani wameenguliwa kutokana na sababu mbalimbali, hali inayofanya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kwenye nafasi ya kushinda viti vingi kati ya 77 vinavyogombewa kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12.

Wagombea hao 16 wanatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), 9 wanatoka Chama cha Wananchi (CUF) na 20 Chama cha ACT – Wazalendo.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi wa Chadema, John Mrema, alisema hadi kufika jana, wagombea udiwani 16 wa chama hicho wameenguliwa kwenye uchaguzi huo.

Kwa upande wa CUF, inayomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma, Abdul Kambaya, alisema wagombea 9 wa chama hicho wameenguliwa, huku kwa upande wa Chama cha ACT- Wazalendo, Ofisa Habari wake, Abdallah Khamis, akisema wagombea 20 wameenguliwa.

Miongoni mwa sababu ambazo zilitajwa kusababisha wagombea hao kuenguliwa kwenye mchakato huo, ni kutojua kusoma, kukosea kujaza fomu, mihuri kugongwa juu ya picha na wengine kujitoa wenyewe.

Hali hiyo, imefanya Chadema kuomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutaka uchaguzi usogezwe mbele, ili malalamiko yao yashughulikiwe.

Wakati tume ikiwa haijatoa majibu ya suala hilo, jana Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Longido, Juma Mhina, alimwengua Mgombea wa Chadema wa Kata ya Kamwanga, Sakimba Nakutamb, baada ya pingamizi alilowekewa na mgombea wa CCM.

Akizungumzia kuhusu pingamizi hilo, Mhina alisema: “Mgombea alishindwa kujaza fomu namba10, hata alipopelekewa barua ya pingamizi hakuweza kuijibu hadi muda aliotakiwa kuresha majibu ofisini ulipomalizika. Kutokana na pingamizi hilo, mgombea wa CCM kwenye Kata hiyo, Elias Laizer, amepita bila kupingwa.”

Alisema katika uchaguzi huo, kata itakayofanya uchaguzi ni Olmolog pekee, ambayo Lomayani Laizer anagombea kwa tiketi ya CCM na Philipo Leng’ochai kwa tiketi ya Chadema.

Alisema katika kata za Langatadapash na Kamwanga, wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa, baada ya wagombea wa upinzani kushindwa kukidhi vigezo na kuwekewa pingamizi.

Hali hiyo ni mwendelezo wa wagombea wa upinzani kung’olewa. Alhamisi wiki hii mgombea udiwani wa Kata ya Mpona (Chadema), Iskaka Mlonge, alienguliwa baada ya msimamizi wa uchaguzi kujiridhisha na mapingamizi yaliyotolewa na mgombea wa CCM, Michael Siwingwa, aliyedai kuwa Mlonge si raia.

Kutokana na wagombea wengi wa Chadema kuenguliwa, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Reginald Munisi, aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusitisha uchaguzi kwenye baadhi ya maeneo na kuanza upya mchakato wa kupata wagombea, ili kila mtu mwenye haki apate nafasi hiyo.

Alibainisha maeneo ambayo chama hicho kinaona kimeonewa ni Tunduka, kwenye kata tano, ambako wagombea walinyimwa fomu.

Alisema kwa Mkoa wa Arusha, mgombea kwenye Kata ya Teratu alinyang’anywa fomu mbele ya msimamizi wa uchaguzi.

Na kwa Mkoa wa Iringa alidai wasimamizi katika kata mbili za Gangilonga na Kilosa walikataa kupokea fomu za wagombea wa Chadema, mazingira ambayo aliyaeleza kuwa yanawatengenezea ushindi wagombe wa CCM.

Chanzo: Mtanzania
 
Safi sana
Upinzani upi haujajipanga kabisa wao wapo ki ruzuku tu
Kazi kwao
 
Leo ktk gazeti la mtanzania kumeripotiwa kuwa jumla ya wagombea 45 wameenguliwa ktk uchaguzi mdogo unaoendelea nchini, wakati wagombea hawa wakienguliwa,, kwa upande wa ccm hakuna mgombea hata mmoja aliyeenguliwa pamoja na wao kiwekewa mapingamizi, hii inaonyesha ni kwa jinsi gani ccm isvyokuwa na uvumilivu wa ushindani wa vyama vingi. Haingii akilini kuwa wagombea wote wa upinzani (45) eti wana mapungufu, hizi ni hila na ni aibu kwa Demokrasia ya taifa letu, kwa haya ccm wanawaogopa wapinzani, kwa haya ccm hawana uwezo kukabiliana na wapinzani ktk majukwaa ya kisiasa, hii pia inadhihirisha kuwa ccm bila mbinu haishindi uchaguzi. Pamoja na haya, kuna umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi, yaliyofanywa na wakurugenzi wa ubungo na tunduma na iringa ni kielelezo cha umuhimu wa tume huru, wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi ndio chanzo na vurugu na uharibifu wa uchaguzi, wengi wao ni makada wa ccm ambao wamekuwa kimkakati kwa ajili ya kukisaidia chama cha Mapinduzi, ni wakati wa wadau wote kudai tume huru isiyokuwa na makada wa kisiasa, ma DC, ma RC, na wakurugenzi wasiwe sehemu ya tume, kwa makamishna wa tume uwalikilishi wa vyama vya siasa na asasi uwepo.
 
Chadema haikujipanga kuingia kwenye uchaguzi huu
tido aliendesha midaharo ya wagombea, tuliona wagombea wa chama gani ni mbulula hadi wakawa hawahudhurii midaharo kinachofanyika ni hasara tupu kwa nchi hii.
 
Si mnge waengua wote tu Tatizo ni nini ?.Mlishaamua Kutawala Milele na nyie ndio wenye Mamlaka ,fanyeni hivyo .
 
yaani waliobaki wanaenguliwa kwenye sanduka la kura...upinzani hata diwani mmoja hakuna...mark my words. tuko pabaya tayari, nchi iko mikononi mwa iblisi.
 
Hata hao waliobaki waache wasishiriki kwasababu Huu sasa ni uzuzu!

Yaani wa vyama upinzani tu Ndio hawajui kujaza form?
 
Back
Top Bottom