Wageni Wako Wananuka?...

Ngabu vipi leo shoulder UMEPIGA?

Daah..babu basi juzi ile nimepiga 21s biceps basi hadi leo biceps zinauma kishenzi. Kwa hiyo leo na take it easy mtu wangu.....si unajua tena resting is gaining....
 
Nimewajua wakarimu na wasiowakarimu
Mgeni ni zawadi na baraka kwa Mwenyezi Mungu
Wako waJF hapa akija ndugu yake kilema basi kama siyo
kuhama basi atahamia baa!!!!:(
 
mi mgeni amabye hana kichwa wala mguu kwangu marufuku.
mgeni awe amekuja kusalimia atakaa siku si zaidi ya tano then achape lapa...labda awe mama yangu.

hawa cijana wanaosoma.....kama yup likizo basi awe anakaa kwangu ili asome sio aje vacation tuu!
Otherwise wageni wa kupita ruksa
wagei waliokuja kupata matibabu ruksa.
 
Inategemea na mazingira wajameni

nasikia kuna baadhi ya makabila wakija kwako hawaondoki ndo wamefika

na wanakua chanzo cha choko choko nyumbani

siye kwetu inafahamika kuwa aidha unakuwa mkaaji au ni mgeni kweli siku 3 max umeshaenda...kwani kila mtu anajua anatakiwa afanye kazi ndo ale!
 
Mkuu,
do, wewe nadhani umedhibiti haya mambo!
Lakini hii sifa ya ukarimu wa watanzania huoni unai'defy?

Wala sijaideny kwani mimi nawakaribisha na kuwapokea vizuri tu tena kwa moyo wote.Ila ni lazima wafuate principles za nyumba yangu na si vinginevyo mkuu.
 
hujaniwekea masharti nuymbani kwangu bado loh!! utachapa mwendo ASAP!!!
SHEMEJI TENA UKIJA KWANGU KEEP THIS IN MIND! !!
Bht, kumbe ndo mambo yenyewe?

Well, umakini wa hali ya juus sana unahitajiwa pale mtu unapoamua kuwa mgeni wa nyumba fulani...sio kujisahau ati, ujione kama mtoto wa kuzaliwa jana..huh!
 
mbaya zaidi awe ni wifi au shemeji, ukifanya kinyume na anvotaka akitoka hapo ujue ukweni utaeleweka vibaya.
Lakini na ieleweke kwamba si wageni wote ni wa baya. Kuna mgeni ambae utatamani aendelee kuwepo nyumbani! Yani anafit kila idara pale nyumbani, hadi siku anaondoka unatamani angeongeza wiki1.
 
Bht, kumbe ndo mambo yenyewe?

Well, umakini wa hali ya juus sana unahitajiwa pale mtu unapoamua kuwa mgeni wa nyumba fulani...sio kujisahau ati, ujione kama mtoto wa kuzaliwa jana..huh!

eeeh biggy hata wewe ukija kwangu next time jiandae nimeweka house rules!!!
 
eeeh biggy hata wewe ukija kwangu next time jiandae nimeweka house rules!!!
huh!
Hata mimi bht?..mi nikija kwako ni mwendo wa soseji tu...sitaki mamchelemchele ya kismas!
 
Katika website ya waynesthisandthat nimepata quote hii ambayo kwangu mimi hai'saund vizuri sana;

.."Like Fish, Guests Begin Smelling After Three Days"...!

Lakini pia, kwa waliosoma vitabu vya zamani primary, kuna habari ya mgeni isemayo:

Mgeni siku ya kwanza,
Mpe mchele na panza,
Mtilie kifuuni ,
Mkaribishe mgeni,


Mgeni siku ya pili
Pika wali kwa samli
Na nyama ratili mbili
Kaa ule na mgeni


Mgeni siku ya tatu
Nyumbani hamna kitu
Muna vibaba vitatu
Pika ule na mgeni

Lakini, ubeti wa nne(ambapo ni siku ya nne ya mgeni) unasema hivi:

Mgeni siku ya nne,
Mpe jembe akalime,
Akirudi muagane ,
Aende zake mgeni.


Mgeni siku ya tano
Mwembamba kama sindano
Hakuishi minong'ono
Asemwa yeye mgeni


Mgeni siku ya sita
Mkila mnajificha
Nani akimbiwaye
Akimbiwae mgeni


Mgeni siku ya saba
Si mgeni ana baa (hii nimesahau...)


Mgeni siku ya kumi
Kwa mateke na magumi
Nani afukuzwaye
Afukuzwa ye mgeni

Wadau, mmegundua lolote kwa wageni wenu majumbani wakaapo siku 3 na kuanza ya 4?

Nimekuongezea beti ninazokumbuka kutoka katika kitabu "Someni kwa Furaha" cha darasa la nne.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom