Wagagagigikoko News: Definition mpya ya muungano na Rais ajaye ZNZ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagagagigikoko News: Definition mpya ya muungano na Rais ajaye ZNZ!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lampart, Dec 6, 2009.

 1. L

  Lampart Senior Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BREAKING NEWS…..BREAKING NEWS!!!!!

  ·[FONT=&quot] [/FONT]Wagagagigikoko on top of news again
  ·[FONT=&quot] [/FONT]Safari hii kuhusu Rais ajae wa ZNZ baada ya Karume
  ·[FONT=&quot] [/FONT]Muungano kupata new definition

  (By a Special correspondent on Union matters)
  Nairobi, Kenya.
  Habari zilizoingia sasa hivi kwenye screen ya Satellite kupitia Nairobi kutoka kwa Wagagagigikoko zinasema kuwa CCM Zanzibar tayari ishampendekeza kwa siri kubwa sana (ambayo hata lile gazeti la udaku la Kulikoni hazijazipata bado) Dr Mohamed Gharib Bilal (a former Chief Minister in Zanzibar under former President Dr Salmin Amour) kuwa ndio pendekezo lao kwa Halmashuri Kuu ya Chama ya kuchagua Rais wa Zanzibar mapema hapo mwakani.
  Wagagagigikoko wanaeleza kuwa yale mazungumzo ya juzi ya Rais Karume na viongozi wa CUF yalikuwa juu ya mada hii. Wakifafanua zaidi walisema kuwa, " Karume alimwita Maalim Seif ili apate baraka zake juu ya Bilal na alizipata".
  Walivyobanwa zaidi juu ya hali hii yakutatanisha na kuulizwa vipi Rais wa CCM aulizwe Maalim Seif, Wagagagigikoko walisema kuwa" Serikali inayokuja ni serikali ya mseto na kama Maalim Seif hatomkubali huyo Rais wa CCM anaekuja, basi huo mseto hautosongwa. Ndio maana Karume akaona bora amuulize Maalim na mapema".
  "Katika wote waliofikiriwa Bilal ndio pekee mwenye msimamo wa kati" na huku wakiendelea kusema kuwa, " Japokuwa ni vigumu sana kumuona Bilal kama ni mtu wa katikati wakati yeye kafungana sana na yule alieitwa mbogo na Nyerere kwa ukaidi, yaani Kommandoo Salmin Amour, lakini siku nyingi zimepita na mambo mengi yamebadilika kisiasa pia"
  "Kwa ilivyo Bilal alikuwa ndio chaguo la Waznz miaka 10 iliyopita, lakini Chamwino ikatumia turufu, kwasababu Kommandoo bado alikuwa mwenye nguvu sana kule ZNZ siku zile. Kumkataa Bilal siku zile ilikuwa ni kumvunja nguvu Kommandoo ambae alionekana akitaka kuivuta ZNZ kidogo kidogo kuwa more independent from Mainland kuliko inavyotakiwa na CCM", aliezea mwanasiasa mmoja.
  "Kwa sasa hivi ZNZ haina mtu ambae ataweza kuchukua msimamo ule wa Salmin na kuiponya ZNZ kutokana na makucha ya kikoloni ya Bara, isipokuwa serikali ya mseto ya CUF with Bilal at the helm. Waznz sasa washajua kuwa wakifanya mchezo Pinda atawameza, kwahivyo 2010 wataungana pamoja ili kuliondoa tishio hilo la Pinda", aliendela muandishi huyo.
  Wagagagigikoko walipoulizwa kama huo mseto na Bilal at the top ni hatari kwa Muungano au vipi, walisema, "Hakuna hatari yoyote kwa Muungano. Kama kuna watu wanaouunga mkono Muungano zaidi hapa Tanzania leo basi ni CUF, kwasababu ambazo zinafahamika. Bila ya Bara demokrasia ZNZ haipo - hilo CUF wanalijua vizuri sana. Bilal na serikali yake ya mseto wanakuja kuipa msisimko na msimamo mpya ZNZ juu ya Muungano. Kwa mazungumzo yote ya mambo ya Muungano, mawaziri wa CUF katika mseto ndio watakaotumwa huko Bara kuipigania ZNZ, kwani itakuwa vigumu kazi hio kufanywa na mawaziri wa CCM katika mseto. In the end, after Bilal's 10 years' rule, Tanzania might be reduced to a Union with only two common (Union) Ministries between the Mainland and the Isles – one encompassing one military command and the other embodying one foreign policy, but with different other Ministries, such as Finance, Higher Education, Natural Resources, etc etc."
  "Itakuwa ni vita tupu, sio juu ya mafuta bali waznz watataka tena kujiunga na ule Umoja wa Kiislamu ili wasaidiwe, kwani huo msaada wa hivi sasa wa vijisenti vinavyotoka Bara pamoja na umeme wa bure haviwafikishi popote".
  Alipoulizwa Mgagagigikoko mmoja kama ni kweli babu yake Bilal anatoka Uganda, alicheka na huku akisema, "Who else is more destined to rule ZNZ than a Ugandan or a Malawian? Au mmemsahau yule Field Marshal – sio yule aliyekuwa akikata watu miguu kwa mapanga ukumbini hivi majuzi, bali yule aliyoongoza mapinduzi ya ZNZ ya 1964?"
  "Kusema kweli, tusitaje nani babu yake katoka wapi na nani katoka wapi. Waznz wote tunajua ni wageni. ZNZ ni nchi ya watu wa Bagamoyo na kwahivyo Pinda anayohaki kuichukua na kuirejesha ikawa part of Tanganyika", aliendela muandishi huyo wa Wagagagigikoko huku watu wapembeni waliokuwa wakisikiliza mazungumzo hayo wakipigwa na butwaaa na matamshi hayo ya kisaliti kutoka kwa Wagagagigikoko.
  "Atakae leta fujo katika huu mseto wa ZNZ atakuwa yule mfanya biashara wa ZNZ aitwae Raza. Huyu Raza ndio ataleta machafuko mengi kwa kujitia kwake kuwa yeye anawasemea waliyo wengi. CUF hawamtaki huyu Raza hata kwa dakika moja, ambae inasadikika kuwa yupo karibu sana na Bilal hivi sasa kuliko enzi zile za Salmin."
  "Raza must be banished from the Isles, else ataleta mvurugano mkubwa ZNZ. CUF lazima ihakikishe kuwa huyu jamaa yupo nje, kwani ni shawishi mkubwa katika siasa za ZNZ/CCM", walimalizia Wagagagigikoko huku wakiweka sawa malubega yao waliovaa na kuingia garini.

  Sources: Wagagagigikoko News Network (WANENE - The No.1 Authentic News Disseminators in Tanzania)
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pongezi !! kwani hata uzushi ni habari ndio maana kuna global publishers and associates (wanunuzi wa udaku).

  Ukipata na za maana zaidi ya hizi (......) utuletee pia.....!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Dec 6, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wagagagigikoko, asanteni sana.
  Ila Dr Mohamed Gharib Bilal namuona kama ni mtu wa kariba ya komandoo tu, mbabe,mbaguzi,ashauriki,mkatili.
  nahisi Znz ipo mbioni kurejea kule alikokuacna Komandoo, nakumbuka enzi za Wapemba kunya mavi visimani na kupaka vinyesi kwenye kuta za shule kisa hasira dhidi ya utawala Salmini.
  sasa leo anakuka kipenzzi chake cha damu, mwanafunzi wake wa utawalaaliefuzu.
  haya na tusubiri tuone.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Duh! Long live Wagagagigikoko News Network. With its breaking news no one is going to leave JF.
   
 5. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  I say, Nd. Lampart kwa mara yapili nakupa congratulations, kwani unapafanya hapa JF pawe pazuri.
  Kwa kweli unanifurahisha na hizo sarcastic zako. Ninajua unakusudia nini, lakini namna unavyozileta zinanifurahisaha sana japokuwa huwa sisomi makala ndufu kama hizi, lakini naahidi zako nitakuwa ninazisoma ili nifurahishe moyo wangu.

  >In the end, after Bilal's 10 years' rule, Tanzania might be reduced to a Union with only two common >(Union) Ministries between the Mainland and the Isles – one encompassing one military command >and the other embodying one foreign policy, but with different other Ministries, such as Finance, >Higher Education, Natural Resources, etc etc."

  Hii scenario ya 2 Union Ministries tu inanifurahisha sana and is very practical, kuliko hivi kushirikiana katika kila kitu na baadae tunashindwa kuhudumiana.
  Lakini mimi naona instead of 2 bora ziwe 3, ili na Home Affairs nayo iwe ya Muungano, else hao KMKM wenu watawamaliza Wapemba kuwachinja ikiwa Home Affairs ipo chini yenu peke yenu!

  >Bila ya Bara demokrasia ZNZ haipo - hilo CUF wanalijua vizuri sana.


  Hilo sote tunalijua, na ndio maana tukawapokea kule Ilala wakiogopa kurejea makwao tokea ile 2001.

  >Bilal na serikali yake ya mseto wanakuja kuipa msisimko na >msimamo mpya ZNZ juu ya Muungano.


  Hii inatisha, lakini usije huu msisimko na msimamo mpya ukawa kama ile nguvu mpya na......... ya Mhe JK na ikamalizikia barazani!

  >"Who else is more destined to rule ZNZ than a Ugandan or a >Malawian?

  Hahahahahahahahahahahahahahahaha!!!!
  Hapa umenivunja mbavu, kwasababu Okello katokea Uganda na Karume katokea Malawi, kwahivyo unaona hawa ndio wawe the rightful rulers wa ZNZ. Hii kweli inaumiza mbavu zangu!!!

  Anyway, wengine tungeliomba hii makala ya Wanene (sio wembamba kama sisi) tuwe tunaipata kila wiki kama itawezekana, ili roho zetu ziwe zinafurahi kila wiki.
   
 6. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Samahani Nd. Lampart, kwa hapo juu naona nilisahau kukueleza kuwa unawaonea ndugu zetu mayakhe, kwani huo umeme hawaupati bure. Umeme wanaulipia kama sisi sote huku Bara tunavyolipia.
  Pia, punde baada ya kusoma huu udaku wako nilipiga simu ZNZ kuulizia kwa jamaa zangu kuhusu huyu Bilal na hayo uliyoyaeleza hapo juu ndugu Lampart ni ya kweli, yaani Bilal anatajwa kisirisiri na wakubwa wa CCM ZNZ, lakini yatajulikana baada ya mwaka mpya.
  Wengi wanaeleza kuwa hii imekuja kama zawadi kwa Kommandoo kukaa kimya bila ya zogo baada ya chenga aliyopigwa Chamwino 10 years ago.
   
 7. L

  Lampart Senior Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Ngida1,
  Nimefurahi kufahamu kwamba ZNZ wanalipia umeme kama sisi sote huku Bara, je, lile deni lao la nyuma la Billioni 18 lipo vipi?
  Ningelipenda kujua kama wewe au mwana-ukumbi yoyote yule anayo habari yakuaminika kuhusu ulipaji wa hili deni kwa serikali yetu ya Tanganyika!
   
 8. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nd. Lampart,
  Naona leo umekusudia, as long as humgusi Mr......you are at peace hapa ukumbini, else utakuenda na maji!
  Lile deni la billioni 18 la umeme kwa ZNZ nimesikia kuwa wamesamehewa na serikali ya Bara. Usiulize kwa mintarafu gani, kwani ZNZ sacrificed its sovereignty na kwahivyo inafaa tuwapulizepulize every now and then, ili wasije wakatokea wabaya wetu wakawaamsha!
  Na wabaya naona tayari washawaamsha, kwani hii serikali ya mseto ya Bilal inayokuja naona tunaundiwa sisi wa Bara ituchemshe, kama vile akina Yussuf Himid walikuwa bado hawatuchemshi.
  Kila la kheri.
   
 9. L

  Lampart Senior Member

  #9
  Dec 6, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Jayfour_King,
  Rais wa ZNZ ni Makamo wa Chama cha CCM na CCM ndio inayoendesha serikali hivi sasa. Kutokana na mambo ya Chadema yanavyokuenda CCM itachukua hatamu ya nchi hii na mwakani pia. Sasa wewe huoni kuwa news za kupatikanwa Rais wa ZNZ ni za maana zaidi?
  Ikitokea fujo huku Bara kwasababu ya huu ufisadi, unadhania tutakimbilia wapi ambako hakuna ufisadi kama sio ZNZ?
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  yangu macho tu
   
 11. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  muwe mnatafuta magazeti ya kizushi mpeleke huko habari zenu za kizushi, CUF mna kazi kweli kweli kipindi hiki nawaonea huruma
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huu uzushi na udaku wa hali ya juu!
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Zanzibar ufisadi upo sema siyo at a large scale kama Bara kwa sababu serikali ya muungano obviously ina resouves na funds nyingi zaidi ya Zanzibar.
   
 14. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika utaratibu wa dunia ya Kistaarabu kuna mnyumburuko wa kusamehe madeni. Hivi wewe unaelewa madeni mangapi hiyo Serikali ya Tanganyika wamesamehewa na kufutiwa?
   
 15. mtwa mkulu

  mtwa mkulu JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2013
  Joined: Sep 11, 2013
  Messages: 2,318
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Eti Jamani Hizi Hekaya Za Wagagagigikoko Zilitimia Kweli?
   
Loading...