Sultani Kipingo
Member
- May 12, 2007
- 6
- 7
Nchi hii kwa kweli inafurahisha sana. Yaani kuna baadhi ya watu wanajiona wana akili sana kuliko wenzao, simply kwa sababu anaweza kuingia mtandanoni na kuweka mawazo yake humo, huku akijiaminisha kwamba watu wote ni wajinga kama yeye.
Hebu ona sinema hii; mjuaji mmoja wao hao wajuaji anamwamuru Rais wa Tanzania asimwongezee muda Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kadata, as if Rais hajui kitu. Yaani nimecheka sana. Inaonesha dhahiri huyu bosi wa TRA kawashika pabaya ndio maana wanaomba aondoke zake ili waendeleze madudu yao.
Kwanza walianza na upuuzi kwamba eti bosi wa TRA Alphayo Kidata anahaha kuongezewa muda, eti akianza na kumuondoa msaidizi wake Saidi Kondo na kumleta Mzanzibari JB Hassan ili kumfurahisha Rais. Yaani hawa wajuaji wanajua sana sana hadi kupitiliza na kusahau kwamba hatua kama hiyo katika sehemu nyeti haiamuliwi na mtu mmoja.
Vile vile hiyo kumtaja Bw. JB Hassan kama Mzanzibari ni dhahiri hao jamaa ni wale waleeeee wasiomtakia Mama jema! Halafu hao hao bila aibu wanataka kumfundisha kazi na wajibu Rais anayeongoza watu zaidi ya milioni 60.
Hii inanikumbusha ule usemi wa kitaa kwamba "Ukitupa jiwe gizani, atakayelia yallah! ujue limempata". Yaani jinsi Kidata alivyowadhibiti hao wajuaji hadi unawaonea huruma.
Hao wajua walianza kumjaribu Mama kwa kumchomekea hoja ya Paul Makonda. Wakasambaza umbea ati oooooh Makonda karudi na kukabidhiwa nafasi ya Sophia Mjema kuwa Katibu wa NEC ya CCM wa Itikadi. Yaani mradi tu wachanganye watu.
Mbaya zaidi hata kuongopa hawajui. kwani walitangaza hayo huku wakidai uamuzi umetoka katika mkutano wa NEC, jambo ambalo si la kweli kwani siku hiyo siyo tu CCM hawakukutana bali pia ilikuwa ni siku ya Miaka 60 ya JKT na uongozi wote wa CCM ulikuwa Uwanja wa Jamhuri kushuhudia sherehe hizo!
Wakaja pia na kwa Jaji Mkuu eti umri wa kustaafu Profesa Ibrahim Hamisi Juma umefika na hastahili kuendelea na wadhifa huo! Yaani mtu unajiuliza hawa wajuaji wa mambo wanajiona wao ni nani hasa. Wanakuwa hawana tofauti na Mfalme Huihui wa Wagagagigikoko.