Wafuasi wa vyama vya siasa vya hapa nchini wanajua siasa nini?

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Habari saa wanachama wenza wa website hii ya jamii forums katika jukwaa la siasa.

Nilikuwa na machache ambayo ningeli penda kuzungumza na wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa vya hapa nchini.

Katika hayo machache ambayo nita zungumza na wanachama na wafuasi hawa, yata jikita zaidi katika mfumo wa maswali yenye kuhitaji majawabu kutoka kwao.

1. Ningelipenda kufahamu je wafuasi na wanachama wa vyama vya siasa vya hapa nchi. je wana elewa nini maana sahihi ya neno siasa ?

2. Je, wana fahamu historia za vyama vyao vya siasa ?

3. Je, wana fahamu msingi/kusudi la kuanzishwa kwa vyao hivyo vya siasa ?

4. Je, wanafahamu ni falsafa ipi vyama vyao wana zifuata ?

5. Je, wana fahamu ni mrengo upi wa kisiasa vyama vyao vinaufuata ?

6. Je, wana fahamu kusudi la wao kuwa wafuasi au wanachama wa hivyo vyama vya siasa ?

7. Je, wana fahamu sera kuu za hivyo vyama vyo vya siasa ni zipi ?

8. Je, mchango wao ni upi katika kuvisaidia hivyo vyama vyao vya siasa kutimiza malengo yake ?

9. Je, wana fahamu ni kipi chanzo kikuu cha umasikini wa taifa hili la Tanzania ? na kipi wao wanaweza kufanya kukomesha umasikini wa taifa hili ?

10. Je, wao wafuasi wa hivyo vyama wana zijua katiba za vyama vyao ? na je wanazi heshimu ?

Ni hayo machache kati ya mengi ambayo ningependa kujuzwa kutoka kwa wafuasi na wanachama wa vyama vya siasa vya hapa nchini.
 
Ninachojua siasa ni iman, same kabisa na dini! Ijapokuwa sijawah kuwa mwanachama wa chama chochote kile! Ila naamini baadhi ka watu kulinana na itikadi zao.
 
Wafuasi wa vyama vya kisiasa hapa nchini wana hitaji elimu kuhusu siasa kwa mapana zaidi.
 
Back
Top Bottom