Wafanyakazi waliosambaza Video ya Dr. Slaa akiingia chumbani Serena Hotel wafukuzwa kazi

Kama hawajajieleza(Hearing) basi wawapeleke mahakamni na tundu lissue asimamie kesi na imani watashinda na watalipwa mamilioni ya shilolingi na pili waliofukuzwa waweke namba zao za X-Pesa tuwachangie,UKAWA watoe pesa kwa ajili ya kujikimu kila mwezi mpaka watakapopata kazi nyingine au kesi kuisha.

hizo pesa mngepeleka kusaidia familia ya Mwangosi.
 
KUfukuzwa kazi si hojs so kitu. Wasingeipata hiyo kazi wangekuwa mahala pengine pia. Unaweza kunadilisha naadhi ya vitu latika maisha ya mtu lakini sio hatima
 
Mimi nasema kwa wapenda mabadiliko hawa vijana watoe acc zao au no zao za simu tuwachangie. Wajitokeze kwny vya habari au ofc za chadema tuwachangie pesa. Nikitendo chakishujaa.
 
I knew this was coming, but ethically speaking they deserve a sack because their actions towards customers might scare them away hence destroying the business.

Ni kweli kabisa, hawana haki ya kutoa siri za mteja hata na iwe vipi. Ile ni hoteli kubwa siri za wateja hazitakiwi kuvuja kiovyo ovyo huo ni ukosefu wa nidhamu kazini.
 
Ni kweli kabisa, hawana haki ya kutoa siri za mteja hata na iwe vipi. Ile ni hoteli kubwa siri za wateja hazitakiwi kuvuja kiovyo ovyo huo ni ukosefu wa nidhamu kazini.

Hawajamaa wapo pabaya
 

Attachments

  • 1442680428744.jpg
    1442680428744.jpg
    29.2 KB · Views: 400
Ni kweli kabisa, hawana haki ya kutoa siri za mteja hata na iwe vipi. Ile ni hoteli kubwa siri za wateja hazitakiwi kuvuja kiovyo ovyo huo ni ukosefu wa nidhamu kazini.
Unasema hao wafanyakazi wametoa siri za wateja wao?

Hao ni whistle blowers ambao wametenda tendo la kijasiri na kishujaa kwa 'kutufunulia' waTz tutambue kuwa kumbe KITENGO kinachoendeshwa na kodi za wananchi wote ili wafanye majukumu yao ya Usalama wa Taifa, wao wamejigeuza na kujipa 'job descriptions' za ziada na kuwa ni watu wa Usalama wa Sisiem!
 
Inashangaza sana mtu kutetea hao kina neema na wenzake. Ninaikubali sana kauli ya Mkapa pale jangwani kuhusu wafuasi wa UKAWA.
Kwa taarifa yako hao ambao Mkapa aliwaita wapumbavu na malofa, almost wote wanavyo 'vichinjio' vyao mifukoni na wote watavibeba siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu ili 'wawachinje' Sisiem kwenye sanduku la kura na kuwapa ridhaa Ukawa kuongoza kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.
 
Sasa kama hizo habari zingekuwa siyo reliable source si tayari ungeshasikia Manejimenti ya Serena Hotel ikizikinusha?

Hivi unataka kusema Manejimenti nzima ya Serena Hotel, hakuna yeyote ambaye ni JF member?

Hivi kama kweli hizi habari zingekuwa za uwongo, wangeendelea tu kukaa kimya huku wakijua fika kuwa 'uwongo' huo unaendelea kupunguza confidence ya wateja wao kwa hiyo Hoteli na hivyo kuharibu business yao?


Unafikiri kila mtu Tanzania ana uwakilishi Jf au wanajali upuuzi wa kitoto kama ulioandika?

Kama huyo 'Neema' wako amefukuzwa kwa kusema ukweli, basi waende kwenye TV wakaelezee walivyoonewa au waende mahakamani sio wewe kuleta umbea usio na miguu mitandaoni.

Utumbo kama huu ndio unaoibua sheria za mitandao kudhibiti ujinga kama huu wa kupakana matope bila ushahidi. Funga domo na uombe msamaha kama huwezi kuweka reliable source wazi.
 
hata mimi nikimfuma housegirl wangu anatoa siri za nyumbani kwangu nje kwa majirani namtimua. swali anajua nilimleta nyumbani kwangu afanye nini???.je anajua wajibu wake???.anajua mipaka yake???. msimamo wake ukoje???. so kwa kilichofanyika ni haki kabisa tuache ushabiki maandazi. nchi nyingine wangefungwa na hata kunyongwa especially kama waliapa kutunza siri mbele ya hakimu.......
 
Waende CMA watapata haki yao faster

Kiongozi waangalie kwanza mkataba wao unasomekaje, moja ya kipengele ni kutunza siri za wateja. Hivyo hapo wao wamekiuka masharti ya mikataba hawatashinda. Ni kuwasidia kupata kazi sehemu nyingine. Na pia waajiri wengine wanaweza kuwaogopa kuwa hawana maadili kwani wanatoa siri
 
Kiongozi waangalie kwanza mkataba wao unasomekaje, moja ya kipengele ni kutunza siri za wateja. Hivyo hapo wao wamekiuka masharti ya mikataba hawatashinda. Ni kuwasidia kupata kazi sehemu nyingine. Na pia waajiri wengine wanaweza kuwaogopa kuwa hawana maadili kwani wanatoa siri
Ingawa mikataba ya Hoteli hiyo ina kipengele kinachosema kuwa Mfanyakazi anapaswa kutunza siri za wateja wake.

Hata hivyo kipengele hicho kinatoa option ya kuwa Mfanyakazi huyo hataonekana ametoa siri iwapo kufichua 'siri' huko kutakuwa kwa maslahi mapana zaidi kwa Taifa letu na Hoteli hiyo kwa ujumla wake.

Kwa mfano iwapo Mfanyakazi ataona Suspicious characters zinazofanywa na mteja ambazo zinahatarisha Usalama wa Taifa au usalama wa Hoteli hiyo anapaswa aziexpose ili zisilete madhara makubwa kwa Taifa

Ni dhahiri basi matendo yaliyokuwa yakifanywa na Dr Mihogo, Dr Mwakyembe na Kitengo kwa kuingia hapo Hotelini kwa 'kujificha ficha' kungeweza kuraise alarm kuwa hizo ni suspicious characters zinazopaswa kuwa exposed kwa maslahi mapana zaidi ya Taifa letu.
 
Kiongozi waangalie kwanza mkataba wao unasomekaje, moja ya kipengele ni kutunza siri za wateja. Hivyo hapo wao wamekiuka masharti ya mikataba hawatashinda. Ni kuwasidia kupata kazi sehemu nyingine. Na pia waajiri wengine wanaweza kuwaogopa kuwa hawana maadili kwani wanatoa siri
Lakini ni vyema tunapolijadili sakata hilo la hao wafanyakazi waliofukuzwa hapo Serena Hotel tusiangalie tu masharti waliyowekewa kwenye mikataba yao kuhusu utunzaji wa siri za wateja, bali pia tuangalie masharti wanayowekewa wawekezaji hao wanapoendesha shughuli zao za kibiashara wawapo nchini.

Miongoni ya masharti wanayopewa wawekezaji hao na kituo cha uwekezaji cha TIC ni wawekezaji hao kutojihusisha na mambo ya kisiasa wawapo nchini.

Sasa ni vyema tukatafakari hivi hiyo hali ya Utawala wa Serena kuonekana dhahiri kukiandaa kikao hicho cha Dr Mihogo na waandishi wa habari katika mazingira ya kutaka kuibeba CCM, hivi hiyo si uvunjaji wa dhahiri wa masharti ambayo Hoteli hiyo imepewa ya kutojihusisha na mambo ya kisiasa?

Ndiyo maana tunawaona wafanyakazi hao kama mashujaa na wazalendo wa dhati wa Taifa letu kwa kuifichua Hoteli yao kwa kujiegemeza upande wa maccm.
 
Back
Top Bottom