Wafanyakazi waliosambaza Video ya Dr. Slaa akiingia chumbani Serena Hotel wafukuzwa kazi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Mh Dr kaona aibu kakimbilia Marekani.God is great hakika kamvua nguo padri.Mungu awasaidie whistle blowers
Dr Mihogo amelazimika kukimbilia Marekani na 'mchumba' wake Mushumbusi, baada ya kuona ule mkakati wake wa kuibomoa Ukawa akishirikiana na washirika wake wa Sisiem ukiwa umebuma.
 
Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,151
2,000
wamekiuka cofidentiality agreements na mwajiri wao (kwa lugha ya chadema wanaitwa wasaliti), ni haki kufukuzwa kazi....kama walitumiwa na ukawa kutoa siri za wateja wa mwajiri, sasa ni zamu ya ukawa kuwapa fidia???
 
Hatujakataa kuwa kuna ulazima wa Wafanyakazi wa Hotel hiyo kutunza siri za wateja wao, ila kama wateja hao hao wanaonyesha dalili ya kufanya mambo yanayokwenda kinyume cha sheria za nchi yetu na wateja hao wanafanya mambo yanayoweza kuhatarisha Usalama wa Taifa, wafanyakazi hao wanalazimika kufichua 'siri' hizo za wateja kwa maslahi mapana zaidi ya Taifa letu.
 
Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,151
2,000
Hatujakataa kuwa kuna ulazima wa Wafanyakazi wa Hotel Industry kutunza siri za wateja wao, ila kama wateja hao hao wanaonyesha dalili ya kufanya mambo yanayokwenda kinyume cha sheria za nchi yetu na wateja hao wanafanya mambo yanayoweza kuhatarisha Usalama wa Taifa, wafanyakazi hao wanalazinika kufichua 'siri' hizo za wateja kwa maslahi mapana zaidi ya Taifa letu.

Sheria gani ya nchi imevunjwa na Serena hotel hapo mkuu....???

Hayo maslahi mapana ya nchi ni yapi....au au subcounciously unaita maslahi ya ukawa kuwa ni maslahi mapana ya nchi???
 
May 5, 2015
10
0
According to labour law walichokifanya no kosa kubwa kimsing walistahili either kuonywa,kufukuzwa na kushtakiwa pamoja,adhabu dhidi yao ni sawa baada ya kupewa nafasi ya kujitetea,mwisho walichokifanya ni sawa kwa maslahi mapana kwa mustakabari waTaifa kuliko kazi zao
 
KIJANA2013

JF-Expert Member
Jan 21, 2013
465
250
Ni sahihi kufukuzwa kazi, kwa sababu hata mimi sitopenda mambo yangu binafsi yaelezwe. Lakini kubwa zaidi haya ndiyo tuyategemee, unajifanya shujaa, then shujaa wa nani? Wamepoteza kazi, wanaopata shida ni waona sio wengine, wale waliokuwa wanashangilia ushujaa wao wamekaa pembeni wanakula bata, wanawacheka. Sasa hivi wanalalamika eti haki za binadamu, unafikiri hizo asasi zitamlazimisha mmiliki wa hotel kuwarudisha kazini? Katika uchaguzi ujao, wapo watakao andamana au kuleta fujo, lakini kabla hujafanya hivyo tafakari athari ya hicho unachotaka kukifanya, ama sivyo yatakuja kukuta ya Neema, utabaki peke yako ukilia chini ya mti. Kijana amka, usitumike kama kibaraka
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Hatujakataa kuwa kuna ulazima wa Wafanyakazi wa Hotel Industry kutunza siri za wateja wao, ila kama wateja hao hao wanaonyesha dalili ya kufanya mambo yanayokwenda kinyume cha sheria za nchi yetu na wateja hao wanafanya mambo yanayoweza kuhatarisha Usalama wa Taifa, wafanyakazi hao wanalazimika kufichua 'siri' hizo za wateja kwa maslahi mapana zaidi ya Taifa letu.

Hilo swala ni complicated zaidi ya hapo wapendwa. Kama uongozi umeamua kuwafukuza kwa kubreach confidentiality hilo ni sawa. Ila walitakiwa kupewa nafasi ya kujitetea. Kwa kipengele hicho wanastahili fidia.

Kuhusu wafanyakazi kuhisi kuwa kuna kitu ambacho kinahatarisha usalama wa nchi, I don't think kuwa wanaqualify kuamua hilo na ni wajibu wao kuripoti suspicion activities kwa watu qualified ili zithibitishwe. Hata kama wangekuwa na uelewa huo bado taratibu haziwatumi kuripoti matukio hayo kwa media! Bahati mbaya hata wangetaka kuripoti, wanalazimika kuripoti hukohuko lilikotokea hilo! That is a problem.

Hoteli ni biashara. Kila biashara inakusudia kulenga kupata faida. Katika biashara kila mteja ni mteja. No matter ni nani. Hata kama ni jirani yako, na kwake kaaga anaenda Marekani bado ni mteja. Katika biashara za aina hiyo hata taratibu za kushughulikia matukio ya uhalifu zinatofautiana. Kwa mfano, ukigundua mtaani kwenu kuna mtu anauza madawa ya kulevya unatakiwa kwenda polisi kutoa taarifa. Ukiwa hotelini ukajenga tabia za kupeleka wateja polisi, umepoteza hela za mteja huyo, umekosa business yote ya rafiki za huyo mteja, na umefukuza wateja wote wanaotegemea siri zao zitunzwe na hoteli. Kwa kifupi you are as good as bankrupt!

Kwa hiyo katika hili swala:

1. Wale walikuwa wateja halali bila kujali walikuwa kisiasa au la. Kwamba walipitia mlango wa nyuma au mbele, wako na wengine wengi huwa wanafanya hivyo. Ethically kutoa taarifa hiyo nje ni kosa.

2. Kuachishwa kazi inaweza kuwa adhabu sahihi kama inaangua katika makosa ya gross misconduct. Pamoja na hilo walitakiwa kufanyiwa hearing. Kama haikufanyika, hilo ni kosa na hivyo terminationa yao inaangukia kwenye kundi la unlawful termination na wakidai haki yao watapewa.

3. Kama hoteli imewafukuza wafanyakazi hao kwa shinikizo la serikali, bila kufuata sheria. hilo ni kosa pia. Bado serikali haikutakiwa kuingilia hilo swala kwani ni kazi ya hoteli kuangalia kama inahitaji wafanyakazi wa aina hiyo, au kama kosa walilofanya wafanyakazi hao ni la kustahili kufukuzwa kuonywa au kupewa karipio.

4. Kwamba hao wafanyakazi ni mashujaa kwa kuvujisha hizo taarifa hizo, inawezekana. Lakini ndani ya kufanya ushujaa huo wamekiuka taratibu za huduma. Hivyo pamoja na kuwa mashujaa kwa kufichua njama za "other parties kuhujumiwa" lakini it's obvious wanastahili adhabu kwa kuvunja confidentiality agreement. Walifichua njama, ni kweli imesaidia, lakini pia walitoa siri za mteja na ni kweli walikosea!

IT IS COMPLICATED!
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,765
2,000
Lakini ni vyema tunapolijadili sakata hilo la hao wafanyakazi waliofukuzwa hapo Serena Hotel tusiangalie tu masharti waliyowekewa kwenye mikataba yao kuhusu utunzaji wa siri za wateja, bali pia tuangalie masharti wanayowekewa wawekezaji hao wanapoendesha shughuli zao za kibiashara wawapo nchini.

Miongoni ya masharti wanayopewa wawekezaji hao na kituo cha uwekezaji cha TIC ni wawekezaji hao kutojihusisha na mambo ya kisiasa wawapo nchini.

Sasa ni vyema tukatafakari hivi hiyo hali ya Utawala wa Serena kuonekana dhahiri kukiandaa kikao hicho cha Dr Mihogo na waandishi wa habari katika mazingira ya kutaka kuibeba CCM, hivi hiyo si uvunjaji wa dhahiri wa masharti ambayo Hoteli hiyo imepewa ya kutojihusisha na mambo ya kisiasa?

Ndiyo maana tunawaona wafanyakazi hao kama mashujaa na wazalendo wa dhati wa Taifa letu kwa kuifichua Hoteli yao kwa kujiegemeza upande wa maccm.

Great Thinker....🙌 🎏 ✅✌💯.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Hilo swala ni complicated zaidi ya hapo wapendwa. Kama uongozi umeamua kuwafukuza kwa kubreach confidentiality hilo ni sawa. Ila walitakiwa kupewa nafasi ya kujitetea. Kwa kipengele hicho wanastahili fidia.

Kuhusu wafanyakazi kuhisi kuwa kuna kitu ambacho kinahatarisha usalama wa nchi, I don't think kuwa wanaqualify kuamua hilo na ni wajibu wao kuripoti suspicion activities kwa watu qualified ili zithibitishwe. Hata kama wangekuwa na uelewa huo bado taratibu haziwatumi kuripoti matukio hayo kwa media! Bahati mbaya hata wangetaka kuripoti, wanalazimika kuripoti hukohuko lilikotokea hilo! That is a problem.

Hoteli ni biashara. Kila biashara inakusudia kulenga kupata faida. Katika biashara kila mteja ni mteja. No matter ni nani. Hata kama ni jirani yako, na kwake kaaga anenda Marekani bado ni mteja. Katika biashara za aina hiyo hata taratibu za kushughulikia matukio ya uhalifu zinatofautiana. Kwa mfano, ukigundua mtaani kwenu kuna mtu anauza madawa ya kulevya unatakiwa kwenda polisi kutoa taarifa. ukiwa hotelini ukajenga tabia za kupeleka wateja polisi, umepoteza hela, umekosa business yote ya rafiki za huyo mteja, na umefukuza wateja wote wanategemea siri zao zitunzwe na hoteli. Kwa kifupi you are as good as bankrupt!

Kwa hiyo katika hili swala:

1. Wale walikuwa wateja halali bila kujali walikuwa kisiasa au la. Kwamba walipitia mlango wa nyuma au mbele, wako na wengine wengi huwa wanafanya hivyo. Ethically kutoa taarifa hiyo nje ni kosa.

2. Kuachishwa kazi inaweza kuwa adhabu sahihi kama inaangua katika makosa ya gross misconduct. Pamoja na hilo walitakiwa kufanyiwa hearing. Kama haikufanyika hilo ni kosa na hivyo terminationa yao inaangukia kwenye kundi la unlawful termination na wakidai haki yao watapewa.

3. Kama hoteli imewafukuza wafanyakazi hao kwa shinikizo la serikali, bila kufuata sheria. hilo ni kosa pia. Bado serikali haikutakiwa kuingilia hilo swala kwani ni kazi ya hoteli kuangalia kama inahitaji wafanyakazi wa aina hiyo, au kama kosa walilofanya wafanyakazi hao ni la kustahili kufukuzwa kuonywa au kupewa karipio.

4. Kwamba hao wafanyakazi ni mashujaa kwa kuvujisha hizo taarifa, inawezekana. Lakini ndani ya kufanya ushujaa huo wamekiuka taratibu za huduma. hivyo pamoja na kuwa mashujaa kwa kufichua njama za "other parties kuhujumiwa" lakini it's wanastahili adhabu kwa kuvunja confidentiality agreement. Walifichua njama, ni kweli imesaidia, lakini pia walitoa siri za mteja na ni kweli walikosea!

IT IS COMPLICATED!
Nimependa namna ulivyolichambua sakata hilo la wafanyakazi wa Serena Hotel katika angle ya sheria za kazi zaidi.
 
Kipigi

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
789
500
Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja.

Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.

Baada ya kikao hicho kwisha kesho yake ikatumbukizwa clip kwenye mitandao ya kijamii ambapo mfanyakazi mmoja wa kike wa Hoteli hiyo aliyatambulika kwa jina la Neema alisikika akielezea namna kikao hicho kilivyoandaliwa na kugharimiwa gharama zote na KITENGO na namna Dr Slaa alivyokuwa amepangiwa chumba katika Hoteli hiyo na KITENGO siku moja kabla na kuwa siku hiyo kabla ya kufanyika kikao hicho Dr Slaa alilala hotelini hapo akiwa na 'mchumba' wake Josephine Mushumbusi.

Dada huyo jasiri na shujaa aliendelea kueleza kwenye clip hiyo namna watu wa KITENGO wakishirikiana na idara ya usalama wa Hoteli hiyo ambavyo walikuwa wakimuingiza kwa kificho hotelini hapo Dr Slaa na mkewe pamoja na Dr Mwakyembe ambaye alikutana na Dr Slaa na kuongea naye kwa masaa matatu kabla ya kikao chake hicho na waandishi wa habari kwa kupitia 'mlango wa nyuma' ambao kwa kawaida hutumika tu na wafanyakazi wa Hoteli hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kuwa Mfanyakazi huyo Neema pamoja na Afisa Mkuu wa Usalama wa Hoteli hiyo pamoja na Msaidizi wake upande wa Usalama, tayari wamashafukuzwa kazi kwa 'maagizo' toka mamlaka za juu za nchi yetu.

Inasemekana pia kuwa wafanyakazi hao hawakupewa hata fursa ya kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo kwenye kikao cha Nidhamu kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Hoteli hiyo na ambavyo pia ni kinyume kabisa cha principle kuu ya Natural Justice ya right to be heard.

Hivyo basi kutokana na taarifa hizo za kutimuliwa kwa wafanyakazi hao kujulikana hivi sasa upo umuhimu mkubwa wa wakereketwa wa haki za binadamu,viongozi wanaounda muungano wa Ukawa na wananchi wengine kwa ujumla wao kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kuwa uonevu huo uliofanywa na serikali hii ya Sisiem dhidi ya wafanyakazi hao unakomeshwa na wafanyakazi hao warejeshwe kazini.

Ndio muwape ajira sasa sio unasema mamlaka za kisheria,mnaponza ajira za watu alafu unasema mamlaka za kisheria,nyinyi vipi?
 
bulama

JF-Expert Member
Dec 13, 2012
576
250
hakuna privacy kwenye mambo yanayohatarisha ustawi wa jamii. Faragha ya kuongwa haijawahi kuwa ethical hata siku moja. Ndo maana mimi nimeifanananisha na kubaka.
We ndo unahitaji elimu ya ziada. Ubakaji ni kosa la jinai. Watu kukutana kwa faragha ni kosa gani la jinai? Hiyo ni invading privacy ya mteja na unethical.
Usitake kulinganisha vitu tofauti. Be logical!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
80,356
2,000
Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja.

Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.

Baada ya kikao hicho kwisha kesho yake ikatumbukizwa clip kwenye mitandao ya kijamii ambapo mfanyakazi mmoja wa kike wa Hoteli hiyo aliyatambulika kwa jina la Neema alisikika akielezea namna kikao hicho kilivyoandaliwa na kugharimiwa gharama zote na KITENGO na namna Dr Slaa alivyokuwa amepangiwa chumba katika Hoteli hiyo na KITENGO siku moja kabla na kuwa siku hiyo kabla ya kufanyika kikao hicho Dr Slaa alilala hotelini hapo akiwa na 'mchumba' wake Josephine Mushumbusi.

Dada huyo jasiri na shujaa aliendelea kueleza kwenye clip hiyo namna watu wa KITENGO wakishirikiana na idara ya usalama wa Hoteli hiyo ambavyo walikuwa wakimuingiza kwa kificho hotelini hapo Dr Slaa na mkewe pamoja na Dr Mwakyembe ambaye alikutana na Dr Slaa na kuongea naye kwa masaa matatu kabla ya kikao chake hicho na waandishi wa habari kwa kupitia 'mlango wa nyuma' ambao kwa kawaida hutumika tu na wafanyakazi wa Hoteli hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kuwa Mfanyakazi huyo Neema pamoja na Afisa Mkuu wa Usalama wa Hoteli hiyo pamoja na Msaidizi wake upande wa Usalama, tayari wamashafukuzwa kazi kwa 'maagizo' toka mamlaka za juu za nchi yetu.

Inasemekana pia kuwa wafanyakazi hao hawakupewa hata fursa ya kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo kwenye kikao cha Nidhamu kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Hoteli hiyo na ambavyo pia ni kinyume kabisa cha principle kuu ya Natural Justice ya right to be heard.

Hivyo basi kutokana na taarifa hizo za kutimuliwa kwa wafanyakazi hao kujulikana hivi sasa upo umuhimu mkubwa wa wakereketwa wa haki za binadamu,viongozi wanaounda muungano wa Ukawa na wananchi wengine kwa ujumla wao kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kuwa uonevu huo uliofanywa na serikali hii ya Sisiem dhidi ya wafanyakazi hao unakomeshwa na wafanyakazi hao warejeshwe kazini.
Hivi mpaka leo bado wako hai ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom